Bunge kuelezwa sababu za matokeo mabaya 'form 4' | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Bunge kuelezwa sababu za matokeo mabaya 'form 4'

Discussion in 'Jukwaa la Elimu (Education Forum)' started by Rutashubanyuma, Feb 10, 2011.

 1. Rutashubanyuma

  Rutashubanyuma JF-Expert Member

  #1
  Feb 10, 2011
  Joined: Sep 24, 2010
  Messages: 157,748
  Likes Received: 415,867
  Trophy Points: 280

  Bunge kuelezwa sababu za matokeo mabaya 'form 4'

  Imeandikwa na Oscar Mbuza, Dodoma; Tarehe: 10th February 2011 @ 08:40

  BAADA ya kushitushwa na matokeo mabaya ya kidato cha nne yaliyotangazwa na Baraza Taifa la Mitihani (Necta) hivi karibuni, Serikali imesema itatoa tamko bungeni kuhusu kiini cha matokeo hayo.

  Msimamo huo wa Serikali ulitangazwa bungeni jana na Waziri Mkuu Mizengo Pinda, wakati akijibu swali la Kiongozi wa Upinzani Bungeni, Freeman Mbowe, aliyetaka kufahamu msimamo wa Serikali kuhusu matokeo hayo ambayo alisema ni hatari kwa uhai wa Taifa.

  Mbowe alisema katika matokeo hayo, zaidi ya asilimia 50 ya wanafunzi hao walipata daraja la 0 na daraja la nne, huku asilimia 11 tu ndio wakiwa wamefaulu vizuri.

  "Hili ni janga la Taifa, maana sasa hawa vijana zaidi ya asilimia 70 hawana la kufanya zaidi ya kuzagaa mitaani.

  Serikali ina mkakati gani wa kuwasaidia ili kuwajengea uwezo wa kukabiliana na maisha yao ya baadaye?" Alihoji Mbowe.

  Pinda alisema, ni kusudio la Serikali kuona inawasilisha tamko hilo katika Mkutano unaoendelea wa Bunge au ujao wa Aprili.

  Kabla ya Pinda kujibu swali hilo, Naibu Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (Tamisemi), Aggrey Mwanri, alisema Serikali tayari imeunda jopo kuchunguza kiini cha wanafunzi hao kupata matokeo mabaya.

  Mwanri alisema ingawa idadi kubwa ya wanafunzi wanaonekana kufeli mtihani huo kutokana na idadi kubwa kufanya mtihani huo ikilinganishwa na miaka ya nyuma, Serikali imeshitushwa na hatua hiyo na inalifanyia kazi suala hilo.

  "Jopo hili linaundwa na wataalamu kutoka Wizara ya Elimu na Tamisemi na wajumbe wake wanakutana Dar es Salaam ili kutathimini na kuchunguza nini chanzo cha matokeo hayo mabaya," alisema Mwanri.

  Alisema, baada ya uchunguzi huo, jopo hilo litaishauri Serikali nini kifanyike na kuiwezesha kutoa tamko bungeni.

  Katika hatua nyingine, Pinda aliwataka wazazi wa wanafunzi wanaosoma shule za msingi na sekondari ambazo zinawapa chakula kutoacha jukumu hilo kwa Serikali peke yake kwa asilimia 100.

  Pinda alikuwa akijibu swali la Mbunge wa Mbozi Magharibi, David Silinde (Chadema) na Godfrey Zambi, Mbozi Mashariki (CCM), ambao walitaka kufahamu msimamo wa Serikali juu ya wazazi kulazimishwa kuchangia fedha za chakula kwa wanafunzi.

  Waziri Mkuu alisema ni lazima mpango wa kuomba wazazi wachangie chakula kwa watoto wao upewe msukumo, kwani tathimini inaonesha, kwamba shule ambazo wanafunzi wao wanapewa chakula hicho, zinafanya vizuri zaidi kwenye masomo.

   
 2. Rutashubanyuma

  Rutashubanyuma JF-Expert Member

  #2
  Feb 10, 2011
  Joined: Sep 24, 2010
  Messages: 157,748
  Likes Received: 415,867
  Trophy Points: 280
  Bunge hili butu la CCM tusitarajie lolote la maana.................tunachohitaji ni katiba mpya ambayo itafuta uwakilishi huu haramu uliokitihiri katika kila sekta ya umma.......................
   
 3. M

  Matarese JF-Expert Member

  #3
  Feb 10, 2011
  Joined: Aug 30, 2009
  Messages: 519
  Likes Received: 10
  Trophy Points: 35
  halafu wakishawasilisha tamko, what next?, nadhani inabidi waende mbali zaidi kwamba kuna mkakati gani kama taifa kwa hawa 50% waliofeli
   
Loading...