Bunge kazi yake ni kupitisha sheria au kutunga sheria?

maonomakuu

JF-Expert Member
Jul 24, 2015
2,516
1,198
Leo nina miaka mingi kufuatilia bunge letu tukufu, ila kinachonishangaza ni pale kila serikali ikipitisha muswada bungeni basi bunge kazi yake ni kuibariki na kupitisha, sasa najiuliza
1.Kila mswada unaopelekwa bungeni ni kuwa serikali haikosei kuuandaa?
2.Je kuna muswada uliowahi kukataliwa bungeni?na kama hakuna je bunge linatimiza majukumu yake?
Ninapata shida pale ambapo kila kinachopelekwa bungeni na serikali lazima ipite kwa ndiyo kubwa.
 
Bunge halijawahi tunga Sheria. Bunge halijawahi andaa bajeti ya serikali wala kitu chochote cha kiserikali.

Kazi zote zinafanyika na maafisa wa serikali. Pia, kamati za mbunge katika hatua fulani wataalam wa wizara au taasisi husika huwasilishwa kwao kabla haijaenda baraza la mawaziri.

Kazi yao nikupitisha. Ndo maana wale na mimi wa kusizia na hawasomi huwa wanaishia kupongezana tu.

Ndo maana wanaposema wanasimamia serikali ni kule kwamba kabla sheria au bajeti haijaanza tumika wanaiangalia kwanza.

Hiyo sasa ndiyo HomeWork ya Wabunge.Kwani Nao watarudi Mitaani kwenye Maisha ya kawaida watakutana na hiyo Sheria.Ikiwa waliipitisha ilikuwa ina Mikanganyiko wataonja Joto la Jiwe.Niwaombe wawe makini katika kupitisha Hizo Sheria.Isiwe kila Mara Sheria inafanyiwa Marekebesho,Na kuna nyingine Wanazipitisha kwa kuwa kwa muda huo watakuwa madarakani ima wafuasi wao kwa manufaa yao na pindi pale wamejunufaisha na sheria husika Na wadau kuanza kupiga kelele Ndo hapo utasikia Sheria hii siyo Nzuri Tuibadili.Hivyo wabunge wawe makini watunge Sheria Nzuri pasi na mazagazaga
 
Tunaweza kupona fikra pale ambapo hivi vyeo vya uteuzi vitakapokoma maana imekuwa chanzo kubwa kujipendekeza ili kuwa waaminifu mwisho wa siku ubunge ukikoma basi wahamie kuteuliwa.
 
Tukatae tusikatae vyeo vya uteuzi ndiyo chanzo cha upigaji, rushwa, kujitoa ufahamu na hata watu kujifanya kuwa miungu watu
 
Bunge halijawahi tunga Sheria. Bunge halijawahi andaa bajeti ya serikali wala kitu chochote cha kiserikali.

Kazi zote zinafanyika na maafisa wa serikali. Pia, kamati za mbunge katika hatua fulani wataalam wa wizara au taasisi husika huwasilishwa kwao kabla haijaenda baraza la mawaziri.

Kazi yao nikupitisha. Ndo maana wale na mimi wa kusizia na hawasomi huwa wanaishia kupongezana tu.

Ndo maana wanaposema wanasimamia serikali ni kule kwamba kabla sheria au bajeti haijaanza tumika wanaiangalia kwanza.
umejibu sahihi sana...watu wengi hili neno 'kazi ya bunge ni kutunga sheria' huwa linawachanganya sana..
 
Leo nina miaka mingi kufuatilia bunge letu tukufu, ila kinachonishangaza ni pale kila serikali ikipitisha muswada bungeni basi bunge kazi yake ni kuibariki na kupitisha, sasa najiuliza
1.Kila mswada unaopelekwa bungeni ni kuwa serikali haikosei kuuandaa?
2.Je kuna muswada uliowahi kukataliwa bungeni?na kama hakuna je bunge linatimiza majukumu yake?
Ninapata shida pale ambapo kila kinachopelekwa bungeni na serikali lazima ipite kwa ndiyo kubwa.
Kuna aina mbali mbali za sheria:
Customary laws, hizi ni sheria zinazotokana na mazoe ya maisha ya kila siku,
Acts, Hizi ni sheri zinazotungwa na bunge, kwa mfano sheria ya kodi ya manunuzi, sheria ya manunuzi, sheria ya makampuni, etc.
Ordinances hizi ni sheria zilizorithiwa kutoka kwa mkoloni esp zile sheria zilizotungwa kabla ya mwaka 1920.
 
Nadhani libadili kauli mbiu badala ya kuwa Bunge la kutunga Sheria, liitwe Bunge la kupitisha Sheria.!
 
Awali ya yote nikupongeze kwa tafakuri mwanana.
Nina uhakika juu ya bunge kuwa halijawahi kutunga sheria na kama zipo mwenye uelewa atutajie japo chache tu. Nijuavyo miswada yote ya sheria tulizonazo huanzia kwa mwanasheria mkuu wa serikali na kuletwa bungeni kupitia wizara zenye uhitaji.
Niseme tu, bunge libadili kuitwa la kutunga sheria liwe la kupitisha sheria.
 
Kazi ya Binge no pamoja Na kutunga Sheria Na pia kuisimamia serikali lakini awamu hii ya tano sijui Kazi yake
 
Exactly kama ndiyo hivyo sasa kazi yao ni nini bungeni? Kumbuka ya kusimamia serikali nayo wanaenda kichama. Haya mambo yanakera sana
 
Kazi ya Binge no pamoja Na kutunga Sheria Na pia kuisimamia serikali lakini awamu hii ya tano sijui Kazi yake
Mkuu kweli sioni mwelekeo wa bunge na hili bunge litaharibu utawala wa Magufuli sana, nilitegemea bunge kuhoji vitu kwa nguvu ili kutengeneza serikali imara na yenye uwajibikaji. Ningefurahi sana hizi nafasi za uteuzi za rais zifutwe, wabunge wa viti maalum kazi yao ni kushangilia tu bungeni Nazo zifutwe na hao mawaziri wasitokane na wabunge maana ni chanzo kubwa za kujipendekeza kwa serikali.
 
Back
Top Bottom