Bundini wako ni nani? Kuwa Bundini wa wengine

Bundini wako ni nani? Kuwa Bundini wa wengine

Bujibuji Simba Nyamaume

Platinum Member
Joined
Feb 4, 2009
Posts
78,679
Reaction score
167,641
Katika video hii unaisikia sauti moja kubwa mahususi na inayojirudia rudia ya mwanaume mmoja Mmarekani mweusi. Mtangazaji wa pambano anatambua uwepo wa mtu huyu anayezungumza kwa sauti akielekeza anayosema kwa Muhammad Ali. Jina lake ni Drew Brown Bundini. Bundini alikuwa pembeni mwa Muhammad Ali katika maisha yake ya ndondi karibu mapambano yake yote - katika kushinda kwake na hata pale mwili wake ulipofikia ukomo na kushindwa kupigana tena. Jukumu lake lilikuwa: kutamka kwa sauti kubwa maneno ya kumpa Ali moyo wakati wa pambano na kumkumbusha umuhimu wa kushinda na kwa nini uwezo wa kushinda anao, kitu ambacho kilikuwa kinampa Ali nguvu ya kisaikolojia kupambana kabla na wakati wa pambano.
Alikuwa rafiki, mtu wa kumpa moyo, mtu wa faraja, mtu wa kumpa maneno ya kumpa nguvu Ali wakati wote wa maisha yake ya ndondi. Alikuwa pia mshairi na wakati mwingine ndiye aliyeandika hotuba za Ali. Bundini ndiye aliyekuja na ule msemo wa Ali wa “float like a butterfly, sting like a bee” akimaanisha “elea kama kama kipepeo, ng’ata kama nyuki”, ikiwa ni mbinu ya kupambana ulingoni. Msemo huu Ali aliutumia sana kuwavunja moyo wapinzani wake ulingoni.
Mwaka 1964, Ali akiwa na miaka 22 na wakati huo akijulikana kama Cassius Clay, alipanda ulingoni huko Miami Florida, kumkabili gwiji wa ndondi aliyeogopwa na bingwa wa wakati huo Sonny Liston. Inawezekana Bundini alikuwa mtu pekee katika ulimwengu wa masumbwi ambaye aliamini Ali angeweza kushinda pambano lile, na muda wote wa mtanange alikuwa akipaza sauti kwenye ukumbi mzima Ali akisikia, “the world is watching”, “sting him” akimaanisha, “dunia inakutazama”, “mmalize”, na kadhalika. Ali aliushangaza ulimwengu alipomshinda Liston na kunyakua ubingwa wa dunia kwa mara ya kwanza.
Kwenye video hii, Ali anapigana na mkali mwingine wa enzi hizo, Joe Frazier, hii ikiwa ni pambano lao la pili. Hakuna ubishi kuwa Frazier ni mojawapo ya mabondia nguli zaidi ambao Ali aliwahi kupambana nao. Alimshinda Ali mara moja, na ilibidi wapigane mapambano matatu tofauti kuamua nani alikuwa bora zaidi. Unamsikia Bundini akipaza sauti kumtia moyo Ali, wakati alipokuwa anafanya vizuri. Frazier alimpompiga Ali, Bundini alikuwa anapaza sauti vile vile akisema, “It’s okay, champ, it’s okay”, akimaanisha “usijali gwiji, usijali”. Kwenye mapambano mengine niliyotazama video zake, Bundini alikuwa akipaza sauti na kusema, “ keep dancing, keep dancing champ”. Kuna mpambano mmoja ambao kwa saa nzima, Bundini alikuwa anapaza sauti na kusema “Fight like Sugar Ray” akimaanisha pigana kama Sugar Ray. [Ali na Bundini walikuwa mashabiki wakubwa wa moja ya mabondia mashuhuri kuwahi kutokea katika historia, Sugar Ray Robinson. Alikuwa katika ndondi kati ya mwaka 1940 hadi 1965 na alishinda mapambano 173 kati ya 200 aliyowahi kushiriki]. Baada ya kupaza sauti kwa saa nzima, “Fight like Sugay Ray”, sauti ya Bundini ilikauka, lakini aliendelea kusema kwa sauti ya kufifia, “Sugar Ray, Sugar Ray” huku Ali akimmaliza mshindani wake. Wakati mwingine Bundini alikuwa akimkera kocha wa Ali, Angelo Dundee. Kuna wakati Dundee hakuhitaji kusema chochote kwa Ali muda wa mapumziko kama jinsi ambavyo makocha husema, kwa sababu Bundini alikuwa tayari ameshasema kila kitu ambacho kilitakiwa kusemwa.
Katika maisha, kila mmoja anamuhitaji Bundini wake. Bundini wako ni nani? Mtaje Bundini wako. Mtafute Bundini wako. Kuwa Bundini kwa mwingine.

By January Makamba
 
Sasa kama anaongea muda wote Dundee alikua anaongea muda gani?
 
Kapicha kahuyo bundini naagalia video za ally sijawahi kumtilia maanani mtu huyu
 
kipindi hicho watu tunalala huku tukiset alarm ituamshe saa kumi na moja tuchek pambano......noma sana
 
Back
Top Bottom