Bunda: Mwanafunzi avunjwa mkono na mwalimu

Ketoka

JF-Expert Member
Sep 23, 2015
1,087
1,913
MKUU wa Polisi wa Wilaya (OCD) ya Bunda, E. Kamuhanda, ameingilia kati sakata la mwananfunzi Peter Richard (13) anayedaiwa kuvunjwa mkono na mwalimu wake baada ya polisi kituo kidogo cha Kibara kugoma kumpatia fomu namba tatu (PF-3).
OCD Kamuhanda ameingilia suala hilo baada ya baba wa mtoto huyo, Richard Wegoro, kwenda kumwona mkuu huyo baada ya kunyimwa fomu hiyo ili ijazwe na daktari katika hospitali ya misheni ya Kibara anakotibiwa.

Mtoto huyo anayesoma katika Shule ya Msingi ya Kasahunga, anadaiwa kupigwa hadi kuvunjwa mkono na mwalimu Joseph Buhija.

Kutokana na danadana hiyo, OCD alimwagiza kwa njia ya simu mkuu wa kituo cha polisi cha Kibara kuhakikisha wanampatia fomu hiyo na kumpeleka mtuhumiwa mahakamani haraka.

Pia alimwagiza daktari wa kituo cha afya Kasahunga aliyempokea mwanafunzi huyo kwa mara ya kwanza, pia achukuliwe maelezo yake kwa ajili ya ushahidi zaidi.

Akizungumza na mwandishi wa habari hizi wakati wakienda kituo kikuu cha polisi cha wilaya ya Bunda, kwa ajili ya kumwona OCD, mwanafunzi huyo alisema tukio hilo la kupigwa na mwalimu Buhija, lilitokea Julai 17, mwaka huu, asubuhi muda mfupi kabla ya mapumziko.

Alisema wakati akiwa darasani na wenzake, mwalimu huyo aliingia na kuwauliza ni kwa nini wanapiga kelele darasani na kuanza kuwachapa kila mwanafunzi viboko viwili viwili na kwamba baadaye alimrudia yeye na kumpiga na viboko hadi akavunjika mkono wake wa kulia na mwalimu huyo alimwacha darasani na kwenda katika ofisi ya walimu.

Richard alisema alisikia maumivu makali na alipofika nyumbani baba yake aligundua kuwa mkono wake umevunjika pale alipompatia kazi na kushindwa kufanya kutokana na maumivu makali aliyokuwa akiyasikia.

Wegoro alisema kutokana na hali ya mtoto wake, alitoa taarifa kwa uongozi wa kijiji, kata ya Neruma, mwalimu mkuu wa shule na mratibu elimu kata na mwalimu huyo aliitwa kwenye kikao kilichoshirikia viongozi mbalimbali na kukubali kumtibu na kumhudumia mpaka atakapopona.

Alisema mwanafunzi huyo alipelekwa katika kituo cha afya Kasahunga, ambako hali yake iliendelea kuwa mbaya na kuamuriwa apelekwe katika hospitali ya Misheni Kibara, ili kupatiwa matibabu zaidi na kufanyiwa vipimo vya X-Ray.

Mzazi huyo alisema baada ya kuona anapigwa chenga tofauti na makubaliano yao mwalimu huyo amhudumie, aliamua kutoa taarifa katika kituo kidogo cha polisi Kibara na mwalimu huyo alikamatwa na kisha akadhaminiwa kwa mujibu wa sheria.

Hata hivyo, alisema alishangazwa na polisi aliyekuwa katika kituo hicho pamoja na kuamriwa na mkuu wa kituo (OCS) ambaye hakuwapo muda huo kufungua jalada la kesi hiyo, askari huyo alikataa na alimwagiza askari mwingie aliyejulikana kwa jina la Hamisi ambaye aliwachukuwa maelezo na kufungua kesi hiyo.

"Nimeamua kumuona OCD kwani nimezungushwa sana na askari wa kituo cha Kibara sijui kuna nini nyuma ya pazia maana siku moja nilishuhudia mtuhumiwa wetu muda wa jioni akiwa kituoni hapo kwa muda mrefu, labda kuna jambo liko nyuma ya pazia sasa ni kwanini wananinyima PF-3 wakati ni haki yetu.

"Tena cha ajabu kingine eti wanasema wakinipa hiyo PF-3 twende nao hadi kwa daktari eti aijaze mbele yao wanaona.

Sasa hayo ulishayaona wapi PF-3 kujazwa mbele ya polisi? Hali hiyo itamwogopesha hata daktari mwenyewe kujaza jinsi wanavyotaka wao", alisema.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kwa tukio hili naogopa kulisadikisha mana Hakuna clip yyt ya kuisapot.watu Wa BUNDA ninawajua mabingwa wa majungu na unafiki hasa ilo Jimbo la MWIBARA kuanzia NYAMITWEBILI, KASAHUNGA, KIBALA, IGUNDU,CHISORYA N.K nimeish huko miaka 5
 
Piga chini hao
Ndio Waziri hawataki wafanyakazi kama hao

Sent from my SM using Tapatalk
 
Back
Top Bottom