BULGARIA: Ng’ombe ahukumiwa kifo

BULGARIA: Ng’ombe ahukumiwa kifo

Ng’ombe ahukumiwa kifo ni?

  • HAKI

    Votes: 3 15.8%
  • SIO HAKI

    Votes: 13 68.4%
  • SIJUI

    Votes: 3 15.8%

  • Total voters
    19
  • Poll closed .

sky walker

JF-Expert Member
Joined
Feb 3, 2018
Posts
1,160
Reaction score
834
Guernsey.jpg


Ng’ombe mmoja mjamzito kutoka nchi ya Bulgaria amehukumiwa kufa baada ya kuvuka mpaka wa nchi yake na kuelekea Serbia kinyume na sheria zinazongoza wanyama pori nchini humo.

Ng’ombe huyo ambaye amepewa jina la Penka alifanikiwa kuvunja zizi lake lililopo katika kijiji cha Kopilovtsi nchini Bulgaria karibu kabisa na mpaka wa Serbia na kuingia kimakosa katika mipaka ya nchi hiyo.

Mmiliki wa ng’ombe huyo Ivan Haralampiev pamoja na mtoto wake wamekuwa wakimtafuta ng’ombe huyo bila mafanikio mpaka walipopata taarifa kuwa anashikiliwa nchini Serbia.

Ikumbukwe kuwa nchi ya Serbia sio mwanachama wa Umoja wa Ulaya hivyo ili mnyama aweze kuruhusiwa kuingia katika nchi hiyo kutoka nchi wanachama Umoja wa Ulaya inabidi awe na vibali maalumu ili aruhusiwe tofauti na hapo sheria inasema kuwa adhabu yake ni kifo.
 
March 3, 1998

Tanzania's justice department has made legal history after a Primary Court magistrate in Rukwa, Tanzania, sentenced a dog to death by hanging, the regional weekly newspaper "The East African" reported in Nairobi, Kenya, yesterday.

The dog's owner, John Kachela (25) was sentenced to a six-month suspended jail sentence and his dog, [named] "Immigration", sent to the gallows "to hang until it dies", after the court ruled that Kachela was guilty of scandalizing the department of immigration.

Stanley Anyitike, the prosecuting immigration officer, told the court that Kachela mischievously gave the name of this "highly respected and law-abiding" government department to his dog and almost every other day went to the immigration department and other public places proudly calling the animal by name.

The mongrel is on death row, with no appeal against conviction or sentence, application for stay of execution or petition to the High Court.

The Tanzania Society for Prevention of Cruelty to Animals has appealed to advocates of the court to take up the matter in the name of "kindness to God's creatures". This dog, "Immigration" is obviously an innocent participant in this act of free speech. But in a senseless act of cruelty by the magistrate, he orders this innocent animal to die for the guilty party, who got a suspended sentence.
 
Mbona na sisi tulimhukumu mbwa kunyongwa? Mbona tuna choma moto vifaranga? Kabla ya kushangaa ya wenzetu, tushangae ya kwetu kwanza.
 
Huyo mtoto anahatia wasubiri azae halafu wamfanye kitoweo
 
Wasubiri ajifungue maana wakimuua sasa watakuwa wameua ng'ombe wawili na mmoja atakuwa ameuawa bila hatia
 
I see wana Sheria kama za Tanzania kiaina... Tz Anapigwa Mnada kwa Raia wake
 
Back
Top Bottom