Bulembo: Uchaguzi wa marudio Zanzibar utakuwa huru na haki kama ule uliopita

Molembe

JF-Expert Member
Dec 25, 2012
9,898
11,745
Mwenyekiti ya Jumuiya ya Wazazi ya Chama Cha Mapinduzi (CCM), Abdallah Bulembo ametoa maoni yake kuhusu hotuba ya rais wa Zanzibar, Dk. Ali Mohamed Shein iliyosisitiza kuhusu marudio ya uchaguzi visiwani humo.

Akiongea na kituo cha runinga cha ITV leo, Bulembo amewataka wananchi kutokuwa nawasiwasi na kujitokeza kushiriki uchaguzi wamarudio pindi tarehe ya uchaguzii takapotangazwa na Tume ya Uchaguzi ya Zanzibar, kwani utakuwa uchaguzi huru na haki kama ulivyopita.

“Cha kwanza amani. Rais ameonesha kwamba nchi itabaki kuwa kama vile vile ilivyo… Ndani ya miaka 52 tumeishi kwa amani. Hilo ndilo kubwa sana ambalo watu wanalitilia mashaka. Na kawahakikishia kwamba lazima uchaguzi utakaofanyika utakuwa huru na haki kama ule uchaguzi mwingine ulivyopita,” alisema Bulembo.

“Kwa hiyo hicho ndicho unaweza kukishika mkononi ni amani. Na uchaguzi unafanyika ili tupate uongozi halali ili tuendelee kuwa na amani,” aliongeza.

Aidha, Bulembo aliwataka watanzania kwa ujumla kufahamu kuwa uchaguzi wa Zanzibar utawahusu wote kwa kuwa utahusu Jamhuri ya Muungano. Lakini aliwataka wenye haki kikatiba na waliojiandisha kupiga kura visiwani humo kujitokeza kwa wingi kupiga kura tarehe itakayotangazwa.

“Katiba yetu inaongelea Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Wapo wenzetu wanadhani labda uchaguzi unahusiana na Zanzibar, hapana. Uchaguzi huu (wa marudio) unahusiana na Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.”

NB: Kama uchaguzi uliopita ulikuwa huru na wa haki kwanini ulifutwa hivi CCM wamekosa msemaji.
 
Hivi Bilembo ndie msemaji wa Tume ya Uchaguzi Zanzibar siku hizi?? Lazima Ccm muwe na msemaji wa Chama sio kila mwenye mdomo aseme. Ndipo tunaona mabango ya ajabu kwa vile hakuna msimamizi. Tunapenda kuona chama kikongwe kama Ccm kikiwa mfano wa kuigwa na sii vinginevyo.
 
Bulembo bhana hahahahaa yaani anaifahamu sana zanzibar kuliko wazanzibari wenyewe
 
Hivi Bilembo ndie msemaji wa Tume ya Uchaguzi Zanzibar siku hizi?? Lazima Ccm muwe na msemaji wa Chama sio kila mwenye mdomo aseme. Ndipo tunaona mabango ya ajabu kwa vile hakuna msimamizi. Tunapenda kuona chama kikongwe kama Ccm kikiwa mfano wa kuigwa na sii vinginevyo.
muulize aliomhoji hakufanya kosa kutoa maoni yake
 
CCM, uchaguzi wa marudio utakuwa Huru na Haki kama ule uliofanyika tarehe 25 October , 2015. Sasa mbona mliufuta? Tatizo la bulembo ni kuwa kampeni meneja WA Magufuli basi anajiona kila kitu anajua. Haya sasa kachemka!!
 
Hivi alikuwa anajua anachosema kweli huyu!! Kama ule uliopita ulikuwa huru na wa haki kwanini wanarudia uchaguzi!
 
Shida moja kubwa ya ccm ni kwamba wanaishi kwenye ulimwengu wa kufikirika kuliko uhalisia... Wanahubiri wasichokiamini huku wakiamini wasichokihubiri....!!!
 
Back
Top Bottom