Bulembo amaliza ziara Mkoani Kagera, kuunguruma na wajumbe wa Bukoba vijijini na Muleba

figganigga

JF-Expert Member
Oct 17, 2010
25,492
54,890

Mjumbe wa Kamati Kuu ya CCM Mwenyekiti wa Jumuia ya Wazazi Tanzania Alhaj Abdallah Bulembo akivalishwa Skavu alipokuwa kwenye mpaka wa Wilaya ya Bukoba Mjini na Wilaya ya Muleba, leo.

Mjumbe wa Kamati Kuu ya CCM Alhaj Abdallah Bulembo akitangulia kwenda kupanda gari baada ya kuvishwa skafu

Vijana wa Bodaboda wakiongoza msafara wa Mjumbe wa Kamati Kuu ya CCM Alhaj Abdallah Bulembo kwenda Mjini Muleba ukitokea Bukoba mjini, leo

Kaimu Mkurugenzi wa Manispaa ya Muleba mkoani Kagera, Bakari Juma, akitoa ufafanuzi kuhusu utekelezwaji wa miradi mbalimbali katika Manispaa hiyo, alipoalikwa kutoa maelezo kwenye kikao hicho, leo

Mjumbe wa Kamati Kuu ya CCM Alhaj Abdallah Bulembo akimvisha shati la CCM Njami Mabula, ambaye yeye na wenzake saba walipokewa na Alhaj Bulembo baada ya kutangaza kuihama Chadema na kujiunga na CCM, kwenye kikao hicho mjini Muleba mkoani Kagera, leo

Mjumbe wa Kamati Kuu ya CCM Alhaj Abdallah Bulembo akimvisha pama ya CCM Bushako Njami, ambaye yeye na wenzake saba walipokewa na Alhaj Bulembo baada ya kutangaza kuihama Chadema na kujiunga na CCM, kwenye kikao hicho mjini Muleba mkoani Kagera, leo

Mjumbe wa Kamati Kuu ya CCM Alhaj Abdallah Bulembo akiwa katika picha ya pamoja na wanachama wapya aliowapokea baada ya kutangaza kuihama Chadema na kujiunga na CCM, kwenye kikao hicho mjini Muleba mkoani Kagera, leo

Mjumbe wa Kamati Kuu ya CCM Alhaj Abdallah Bulembo akimpongeza Diwani wa Kata ya Karamba Felix France, kwa kufanikisha wanachama hao wa Chadema kuhamia CCM kwenye kikao hicho mjini Muleba mkoani Kagera, leo

Katibu wa CCM mkoa wa Kagera Rahel Ndegereka akifanya utambulisho wakati wa kikao hicho.

Mwenyekiti wa CCM mkoa wa Kagera Constasia Buhiye akifua rasmi kikao hicho

katibu wa Jumuia ya Wazazi Tanzania mkoa wa Kagera akimkabidhi kitenge Kwa Mama Buhiye ili akikabidhi kwa Alhaj Bulembo ikiwa ni zawadi kutoka kwa Nina Mama wa UWT wa mkoa huo.

Mjumbe wa Kamati Kuu ya CCM Alhaj Abdallah Bulembo akizungumza na wajumbe katika kikao hicho, mjini Muleba mkoani Kagera, leo

KIKAO CHA BUKOBA VIJIJINI

Mwenyekiti wa CCM Wilaya ya Bukoba Vijijini Novatus Mkwama, akizungumza wakati wa kufungua kikao cha Halmashauri Kuu ya CCM ya Wilaya hiyo, Wajumbe wa Mabaraza ya Jumuia za CCM, Mabalozi na Watendaji wa Serikali, kikao kilichofanyika Bukoba mjini leo. Kushoto ni Mjumbe wa Kamati Kuu ya CCM Alhaj Abdallah Bulembo na kulia ni Katibu wa CCM Mstaafu mkoa wa Kagera Faustine Kamaleki na Katibu wa CCM mkoa huo Rahel Ndegereka.

Mwenyekiti wa CCM Wilaya ya Bukoba Vijijini Novatus Mkwama, akizungumza wakati wa kufungua kikao cha Halmashauri Kuu ya CCM ya Wilaya hiyo, Wajumbe wa Mabaraza ya Jumuia za CCM, Mabalozi na Watendaji wa Serikali, kikao kilichofanyika Bukoba mjini leo. Kushoto ni Mjumbe wa Kamati Kuu ya CCM Alhaj Abdallah Bulembo na kulia ni Katibu wa CCM mkoa huo Rahel Ndegereka.

Kikosi kazi cha mambo ya habari kikiwa kazini nje ya ukumbi wakati wa mkutano huo.


Wajumbe wakimsikliza Mjumbe wa Kamati Kuu ya CCM Alhaj Abdallah Bulembo alipokuwa akizungumza wakati wa kikao hicho

Maofisa kutoka Makao Makuu ya Jumuia ya Wazazi Tanzania, wakiwa kwenye kikao hicho

Mjumbe wa Kamati Kuu ya CCM Alhaj Abdallah Bulembo akisisitiza jambo wakati akizungumza wakati wa kikao hicho. PICHA: BASHIR NKOROMO
 
Back
Top Bottom