Buku 5(5,000) ya Comoro 20,000 ya Tz

Buku 5(5,000) ya Comoro 20,000 ya Tz

KIM KARDASH

JF-Expert Member
Joined
Sep 21, 2011
Posts
5,139
Reaction score
1,150
Nilikua naangalia Ayo tv on u tube ambao walikwenda Comoro kuripoti game Yanga na Ngaya...nimeshangazwa kidogo kusikia hela ya Comoro nchi inayo import almost everything toka nje hela yao iko juu kuliko shilingi yetu,

Elfu Tano ya Comoro-zambia-champions ni sawa na Tshs. 20,000.
Wachumi hebu tiririkeni,hii inawezekana vipi kwa wacomoro wasiozalisha na kuexport chochote zaidi ya ku-import tu
 
M nilishangaa msumbiji kutuacha mbali kwenye thamani ya ela..
kumbe hadi Comoro
 
Malawi kwacha shilling million moja sawa n.a. 3 Tanzania millions shilings.
 
Comorian Franc inatuzidi mbali sana
Euro moja ni sawa na Comorian Franc 491.623

Hapa kwetu euro moja ipo juu ya 2000.

Soma hapa chini uone wataalamu wa uchumi wanavyoisaidia Comoro kuipa thamani pesa yao.
The stability of the Comorian franc is founded on tight monetary and credit discipline, underpinned by two specific safeguard measures: the central bank is required
to maintain 20% foreign-exchange cover of its sight liabilities, and the government is not allowed to draw more than 20% of the previous year's budget receipts.
from their central bank funds.
 
JIULIZE YEN YA KIJAPAN INA BADILISHWA KWA TSHS. NGAPI ZA KITANZANIA, HALAFU LINGANISHA NA RAND YA AFRIKA YA KUSINI INABADILISHWA KWA SHILINGI NGAPI? KISHA LINGANISHA UCHUMI WA NCHI HIZO. JE NI KWELI KUWA UCHUMI WA NCHI UNATOKANA NA THAMANI YA FEDHA?
 
Mbona mnaumiza vichwa kuwaza wasiyoyataka watawala na wataalamu wa nchi yetu?! Siku hizi kipeumbele ni siasa kwanza, na kama unaona nadanganya niambie zile habari za kilimokwana wapi au bigresult now!
Unawaza na kuzungumzia mbali huko wakati kenyan sh. 5000 ni sawa na tz sh. 100000+,siasa na kukomoana tu tunaweza, ajira zimebaki za wateule tu, viwanda tunaambiwa vimeongezeka kumbe vya mikate! Unategemea ukauze mkate marekani au??! Mabadiliko kweli tuliyaomba lakini siyo haya ya kukomoana, tulitaka ya uchumi, means ajira, viwanda na biashara super.
 
Kuna wakati thamani ya pesa haimaanishi hali nzuri ya uchumi.

Shilingi 1 ya Kenya ni Sawa na Yen 1 ya Japan.

Shilingi 1 ya Kenya ni sawa na Won 11 za South Korea

Lakini Kenya haifikii uchumi wa Japan au Korea ya Kusini hata kwa 1/10.

Tuje kwetu

Kwacha 1 ya Malawi ni sawa na Shilingi 3 ya Tanzania

Shilingi 1 ya Tanzania ni sawa Kwacha 4 za Zambia (kabla ya Rebase ya 2012)

Kwacha 1 ya Zambia (Kwacha Mpya kuanzia January Mosi, 2013) ni sawa na Shilingi 230 ya Tanzania.

Lakini uchumi wa Zambia na Malawi si mkubwa kwa Tanzania
 
Sina ujuzi na haya mambo ngoja nikae kimya hata kwenye kuagiza vitu nje mfano Magari kwao wanauafueni kidogo au?
 
Ni Kweli Sisi Tuliosoma ForEX, Mambo ya hedging, Money Markets tunajua hilo.
 
sarafu za kiafrika huwa zinafumuka kwa kasi ndio tofauti iliyopo...hiyo shilingi ya kenya dhidi ya Yen zipo sawa sasa ila miaka 10 iliyopita shilingi 1 ya kenya ilikuwa na value almost mara 2 ya hiyo Yen 1 ya Japan
point kuu ipo kwenye stabiliy na sio value ya sasa
 
Global business iliyopo ni betting kweli tuko makini kwa mwendo wa kubeti tukuze uchumi.
Sasa hivi per capital income imeshuka sana. Kifupi ni kwamba idadi ya watu inaongezeka lakini ukuaji wa uchumi unasuasua. Hii maana yake ni kwamba tunazidi kuwa dependent day by day.

Serikali iweke vipaumbele vizuri.

If I were the president of the country ningefanya yafuatayo

Mosi, ningesisitiza uzazi wa mpango. Hii inasaidia kupunguza watu dependent

Pili, ningekazania kuimarishwa kwa sekta binafsi. Kama nchi hatuto piga hatua bila kuipa nafasi private sector ili ku-diversify economy

Mwisho, ningeimarisha utawala bora. Yes transparence and accountability ni muhimu sana kwa nchi ili mambo mengine yawezekane
 
>>> hii ni AIBU kwa Watawala na Wachumi Wetu Kushindwa kushughulika vema na UCHUMI ni AIBU >>
 
JIULIZE YEN YA KIJAPAN INA BADILISHWA KWA TSHS. NGAPI ZA KITANZANIA, HALAFU LINGANISHA NA RAND YA AFRIKA YA KUSINI INABADILISHWA KWA SHILINGI NGAPI? KISHA LINGANISHA UCHUMI WA NCHI HIZO. JE NI KWELI KUWA UCHUMI WA NCHI UNATOKANA NA THAMANI YA FEDHA?
CHINESE YEN moja ni sawa na T. shilingi 350
 
Ila kenya muda mrefu wameweza kuidhibiti thamani ya sarafu yao
 
Back
Top Bottom