Bukoba vijijini bado yashika mkia kielimu ..............


Rutashubanyuma

Rutashubanyuma

JF-Expert Member
Joined
Sep 24, 2010
Messages
169,611
Likes
633,719
Points
280
Rutashubanyuma

Rutashubanyuma

JF-Expert Member
Joined Sep 24, 2010
169,611 633,719 280
Bukoba vijijini bado yashika mkia kielimu
Monday, 06 December 2010 22:12

Phinias Bashaya, Bukoba

WILAYA ya Bukoba Vijini ambayo aliyekuwa mkuu wa wilaya ,Albert Mnali alitimuliwa kazi mwaka 2008 na Rais Jakaya Kikwete kwa madai ya kuwacharaza viboko walimu, imezidi kuboronga katika matokeo ya darasa la saba baada ya kushika mkia kwa miaka minne mfululizo.

Mwishoni mwa mwaka juzi, aliyekuwa mkuu wa wilaya hiyo alimwamuaru mwanajeshi kuywachapa vibokjo walimu kwa kuzembea kufundisha akidai wanapokea mishahara ya bure. Mkuu huyo aliachishwa kazi kwa kosa hilo.

Wilaya hiyo ambayo matokeo mabaya yalidaiwa kuchochea hasira za mkuu huyo wa wilaya,imekuwa ya mwisho kama ilivyokuwa miaka mitatu iliyopita kati ya wilaya nane za mkoa wa Kagera.

Hata hivyo kiwango cha ufaulu katika wilaya hiyo kinaonekana kupanda ikilinganishwa na matokeo ya mwaka jana kutoka asilimia 33 hadi 50.4

Kwa mujibu wa Ofisa Elimu Taaluma, Renatus Bamporiki wilaya iliyoongoza ni Ngara, ikifuatiwa na Biharamulo ambapo wanafunzi 2,127 hawatajiunga na kidato cha kwanza kutokana na upungufu wa vyumba vya madarasa.

'Mwaka huu kuna mafanikio ikilinganishwa na matokeo ya mwaka jana, tulihamasisha walimu wafanye kazi, mtu usimuulize amepata ngapi,muulize amepataje” alibainisha Bamporiki akitetea matokeo ya wilaya hiyo.

Pia alisema, pamoja na wanafunzi wengi kufaulu hawataweza kujiunga na masomo na kudai mazingira magumu yamesababisha wasipangiwe shule zilizoko mbali na maeneo yao.

Pia alibainisha kuwa baadhi ya halmashauri za wilaya zina nafasi ya wanafunzi kujiunga na kidato cha kwanza,na kutoa changamoto ya jamii kuongeza nguvu za ujenzi wa vyumba vya madarasa ili wanafunzi waliofaulu wapate nafasi ya kujiunga na kidato cha kwanza.
Katika kikao cha wadau wa elimu mwezi Machi mwaka huu, ilibainishwa kuwa matokeo mabaya katika wilaya hiyo yanachangiwa na mazingira magumu ya kazi kwa walimu,huku baadhi yao wakidaiwa kuiba muda wa kufundisha ili kufanya biashara baada ya kupata mikopo kutoka katika taasisi za fedha.

Aidha katika mchakato wa kampeni za ubunge,Jasson Rweikiza ambaye ni mbunge wa jimbo hilo kupitia CCM, aliiambia Mwananchi kuwa miongoni mwa mipango yake ni kufanya utafiti ili kubaini chanzo cha kudorola kwa elimu katika wilaya hiyo.
 

Forum statistics

Threads 1,236,524
Members 475,191
Posts 29,260,785