Bukoba Municipal Developmental Conference (BUMUDECO)

Joined
Dec 10, 2015
Posts
22
Reaction score
70
Wapendwa Ndugu, Wadau na Wazawa wa Bukoba,Kagera..

Nichukue fursa hii kuwakaribisha katika Bukoba Municipal Developmental Conference (BUMUDECO) Kongamano litakalowapa fursa ya kuijadili na kuijenga Bukoba Mjini Tuitakayo.
Kongamano hili limeandaliwa na Mbunge & Baraza la Madiwani kutegemea kufanyika 27 Disemba 2015 saa tisa Jioni. (tutawajulisha juu ya ukumbi hivi karibuni).

JUKWAA HILI LITAAMBATANA NA YAFUATAYO:

-Mbunge na Baraza la Madiwani kuwasilisha mpango kazi wetu wa miaka mitano 2016-2020.
-Mwakilishi wa Halmashauri kuwasilisha Fursa za uwekezaji zilizoko Bukoba Mjini.
-Kuzijadili changamoto za wananchi na wazawa wa Bukoba Mjini ili kuzitafutia ufumbuzi wa kudumu.
-Kuona ni namna gani wazawa wa Bukoba, Kagera walioko mbali wanaweza kushiriki katika maendeleo ya Bukoba Mjini.

BUKOBA MPYA TUTAIJENGA KWA KUWA NA UONGOZI SHIRIKISHI UTAKAOWAPA WANANCHI, WAZAWA NA WADAU FURSA YA KUSHIRIKI.

Kongamano hili haliko katika misingi ya uvyama,udini wala ukabila. Yeyote mwenye kutaka kuiona Bukoba Mjini ikisonga mbele kwa kasi anakaribishwa sana.
Tuendelee kuwasiliana kupitia ukurasa wangu wa Facebook: Wilfred Lwakatare na email: mbungebukoba2016@gmail.com au wilfredlwakatare@gmail.com

kufika kwenu ndiyo mafanikio yetu.

Wenu katika ujenzi wa Bukoba Mpya;
Wilfred M. Lwakatare
Mbunge Bukoba Mjini 2015-2020.
 
Sawa Mbunge, Lakini Mbona Inasemekana Huko Nyuma Ziliwahi Kuchangwa Pesa Alafu Zikapotelea Mikononi Mwako? . Mbona naona kama siku moja haitoshi, kwanini msingefanya tarehe 22 na tarehe 27 ili kujadiri kwa umakini, upana na mkaweza kuandaa vitu madhubuti?
 
Ahsante kwa maoni yako Ndugu Rweye,
Program ya Abaana Bashome ilikuwa chini ya Halmashauri ya Bukoba Mjini 2000-2005 mimi nikiwa Mbunge. Pesa zilizochangwa zilitumika katika kuboresha shule za serikali na kununua nyenzo zake. hakuna pesa iliyopokelewa na mikono yangu, zote zilielekezwa Halmashauri na records zipo. usipotoshwe na propaganda za kisiasa.

Tarehe 27 itakuwa ni fursa ya kujadili kwa umakini na upana agenda nilizoeleza hapo juu. pia tutatoa fursa ya ushiriki kwa mtandao na njia mbalimbali.
Karibu sana Tuijenge Bukoba kwa pamoja. SHUKRAN
 
Sawa Mbunge, Lakini Mbona Inasemekana Huko Nyuma Ziliwahi Kuchangwa Pesa Alafu Zikapotelea Mikononi Mwako? . Mbona naona kama siku moja haitoshi, kwanini msingefanya tarehe 22 na tarehe 27 ili kujadiri kwa umakini, upana na mkaweza kuandaa vitu madhubuti?

Nakumbuka zilikuwa za kusaidia watoto wa Bona Bana.
 
Nimejisahihisha, zilikuwa za Abaana bashome. Niliumia sana kusikia kuwa zimepotea kwenye mikono ya mh mbunge wangu japo kuwa miaka ile nilikuwa bado dogo. Nikawaza mh. kashindwa kulitendea haki jina lake la Muganyizi.
 
Nimejisahihisha, zilikuwa za Abaana bashome. Niliumia sana kusikia kuwa zimepotea kwenye mikono ya mh mbunge wangu japo kuwa miaka ile nilikuwa bado dogo. Nikawaza mh. kashindwa kulitendea haki jina lake la Muganyizi.

Program ya Abaana Bashome ilikuwa chini ya Halmashauri ya Bukoba Mjini 2000-2005 mimi nikiwa Mbunge. Pesa zilizochangwa zilitumika katika kuboresha shule za serikali na kununua nyenzo zake. hakuna pesa iliyopokelewa na mikono yangu, zote zilielekezwa Halmashauri na records zipo. usipotoshwe na propaganda za kisiasa.

Tarehe 27 itakuwa ni fursa ya kujadili kwa umakini na upana agenda nilizoeleza hapo juu. pia tutatoa fursa ya ushiriki kwa mtandao na njia mbalimbali.
Karibu sana Tuijenge Bukoba kwa pamoja. SHUKRAN
 
Asante mbunge wangu, kuna changamoto nyingi sana Bukoba tena ambazo ni pasua kichwa. Kumeibuka suala ya kunyofoa makoromea na sehemu za siri, naona kwa sasa limetulia kidogo.Hii ni changamoto kubwa sana kwako. Sasa sijui una mawazo gani, umejipanga vipi kushirikiana na kamati ya ulinzi ya wilaya kukomesha huu ukatiri.
 
Program ya Abaana Bashome ilikuwa chini ya Halmashauri ya Bukoba Mjini 2000-2005 mimi nikiwa Mbunge. Pesa zilizochangwa zilitumika katika kuboresha shule za serikali na kununua nyenzo zake. hakuna pesa iliyopokelewa na mikono yangu, zote zilielekezwa Halmashauri na records zipo. usipotoshwe na propaganda za kisiasa.

Tarehe 27 itakuwa ni fursa ya kujadili kwa umakini na upana agenda nilizoeleza hapo juu. pia tutatoa fursa ya ushiriki kwa mtandao na njia mbalimbali.
Karibu sana Tuijenge Bukoba kwa pamoja. SHUKRAN

Sawa mh. Sasa tunaamini Bk imepata mtu sahihi wakuifanya ikimbie kimaendeleo. Tuko pamoja nawewe bega kwabega, usikatishwe tamaa nawatu wenye nia ovu juu yamaendeleo ya Bkb nzima kwa ujumla.

Next time ningependa kama mungeungana wabunge wote mnaotoka Bukoba, mkaweka pembeni tofauti za kisiasa, mkaweka mkakati wakuifufua Bkb yetu kielimu, kiafya, kijamii nk.
 
Kazi nzur km litafanikiwa. Ila watu bado watu wana mashaka na hilo kongamano maana uliwahi kuchangisha hela za Abana Bashome zikaliwa.
Tokea umepata ubunge hujawahi kuonekana jmboni. Umeshndwa hata kuandaa mkutano wa kuwashukuru wananchi. Ss tuliokuwa washabiki wako ndo tunapgwa vjembe maana tunaambiwa tumemchagua mtu kapotea jimboni. Jirekebshe mzee kuwa karbu na wananchi wako ili ujue matatzo yao vngnevyo 2020 utapgwa chini. Nakutakia majukumu mema.
 
Kama ana makazi ya kudumu Kimara,watoto wote wamesoma Dar,mke yuko Dar naye anasoma mzumbe mbeya unategemea kweli aonekane Bukoba?
 
Nmeshampa tahadhari. Tumemchagua sio kwmb alikuwa anafaa bali ni kuwa tulikuwa tushamchoka xana Kagasheki. Watu wanakumbuka aliyoyafanya 2000-2005 kipndi akiwa Mbunge. Km akiyarudia ubunge ndo basi tena. Ndo maana nmempa ushauri.
Baada ya kushnda ubunge ameshndwa hata kuwashukuru wananchi. Watu wanalalamika xana. Ss tuliokuwa tunapga kampeini tumebaki kukejeliwa tu.
 
Kazi nzur km litafanikiwa. Ila watu bado watu wana mashaka na hilo kongamano maana uliwahi kuchangisha hela za Abana Bashome zikaliwa.
Tokea umepata ubunge hujawahi kuonekana jmboni. Umeshndwa hata kuandaa mkutano wa kuwashukuru wananchi. Ss tuliokuwa washabiki wako ndo tunapgwa vjembe maana tunaambiwa tumemchagua mtu kapotea jimboni. Jirekebshe mzee kuwa karbu na wananchi wako ili ujue matatzo yao vngnevyo 2020 utapgwa chini. Nakutakia majukumu mema.

ukiishi kwa propaganda utapata taabu sana. sherehe ya ushindi waulize wananchi waliokesha nyumbani kwangu Kibeta na kung'oa mahindi, maharagwe na mikungu ya ndizi. waulize wananchi tuliofanya nao usafi 9 Disemba 2015. Kaniulizie ofisi ya Mbunge Rwabizi. kaniulizie Ofisi za Halmashauri. na hivi sasa niko Bukoba tukijipanga na uchaguzi wa Mayor kesho Asubuhi.
siasa uchwara zinakwamisha maendeleo.
 
ndugu zangu, campaign zimeisha na sasa ni wakati wa kutekeleza sera na mikakati. tushikamane na kushirikiana ndo tutafanikiwa. ahsante
 
ukiishi kwa propaganda utapata taabu sana. sherehe ya ushindi waulize wananchi waliokesha nyumbani kwangu Kibeta na kung'oa mahindi, maharagwe na mikungu ya ndizi. waulize wananchi tuliofanya nao usafi 9 Disemba 2015. Kaniulizie ofisi ya Mbunge Rwabizi. kaniulizie Ofisi za Halmashauri. na hivi sasa niko Bukoba tukijipanga na uchaguzi wa Mayor kesho Asubuhi.
siasa uchwara zinakwamisha maendeleo.

Mzee tatzo sio sherehe, nisome vzuri! Ulipaswa kuweka mkutano wa hadhara wa kuwashukuru wananchi km mbunge. Sijaongelea sherehe hzo. Hata madiwani wengi baada ya kushnda walifanya sherehe lakn hilo halikuwazuia kupita kwa wananchi kuwashukuru.
Mbunge wangu usipokuwa mtu wa kupokea maoni ya watu wako mbeleni kuna tabu. Kagasheki kilichomuangusha ni hayo hayo ya kuamini kila anachofanya yy ni sahihi na hakuna mtu wa kumshauri.
 
Mh. nimekuelewa kama hivyo ndivyo. Sasa mkishaandaa agenda za mkutano mtufahamishe ili tuweze nasi kuchangia hizo ajenda. Tunaelewa ishu ni maendeleo lakini naamini mkishaiweka vizuri itatuwia rahisi. Ni jambo jema ila niwasihi wenzangu kwenye mambo haya tuachane na "emize" na "kabambone", okugaya, okushonesangana, okwanjalana na kamunobere haya mambo si ya kuchekea na kukumbatia. Ni bora sana wakati mwingine tukaukosa mchango wako kuliko kutumia lugha za hivi.
 
Kweli kabisa. Huu ni muda wa kurudsha heshima ya Bukoba kwmb ni "abashomi". Maana nshomile ni wengi lakn wameshndwa kuijenga Bukoba yao kutokana na tabia ulizozitaja. Mungu atutangulie. Mbunge wetu inabd awaunganishe watu wa Bukoba ili kufuta yale makundi ya siasa ili twende sawa kimaendeleo.
Nina imani na mbunge wetu.
 
Mheshimiwa mimi siyo mkazi wa Bukoba lakini nafika mara kwa mara hapo mjini kwa shughuli zangu binafsi nikitokea mkoani kwangu. Nashauri kama mtanzania mpenda maendeleo mjaribu kujadiliana kuhusu suala la kuihamisha stendi ya mabasi iliyopo hapo katikati ya mji maana ni ndogo sana na imezidiwa na wingi wa magari. Hii pia itasaidia kuutanua mji na kuongeza fursa. Nakutakia shughuli njema katika kuwalete maendeleo wananchi wako.
 
Mzee tatzo sio sherehe, nisome vzuri! Ulipaswa kuweka mkutano wa hadhara wa kuwashukuru wananchi km mbunge. Sijaongelea sherehe hzo. Hata madiwani wengi baada ya kushnda walifanya sherehe lakn hilo halikuwazuia kupita kwa wananchi kuwashukuru.
Mbunge wangu usipokuwa mtu wa kupokea maoni ya watu wako mbeleni kuna tabu. Kagasheki kilichomuangusha ni hayo hayo ya kuamini kila anachofanya yy ni sahihi na hakuna mtu wa kumshauri.

labda kama ni kubisha ki-ccm ujue baada ya uchaguzi wenye figisu mikutano ya hadhara imekatazwa kwakuwa itaamsha hasira za goli la mkono -si bukoba wala dsm hakuna mikutano over
 
Mimi ingawa ni mtu wa Kyerwa lakini nimewahi kufanya kazi serikalini hapo Bukoba na najua siasa za hapo Bukoba ....kwanza kwa location ya Bukoba ina advantage nyingi kuliko Mwanza ....Kagera ndio mkoa unaopakana kwa ukaribu na nchi nyingi tena nchi hizo miji yao mikuu ikiwa mbali kulinganisha na distance ya kufika Bukoba ......lakini Bukoba imeshindwa kuvutia wafanyabiashara wengi kutoka nchi jirani kutokana na vitu vingi ....nikipata wasaa nitaviainisha hapa ili serikali isaidie kuimarisha miji mikubwa ya mipakani inayoweza kuvutia biashara nyingi ...
 
Back
Top Bottom