BUKOBA: Mke aua mume wake kwa wivu wa mapenzi

BUKOBA: Mke aua mume wake kwa wivu wa mapenzi

Hivi punde

JF-Expert Member
Joined
Apr 1, 2017
Posts
2,554
Reaction score
8,627
Victoria Salvatory (58), mkazi wa kata ya Katoma, Kagera anashikiliwa na polisi kwa tuhuma za kumuua mumewe, Salvatory Iteganira (62) kwa kile kinachodaiwa ni wivu wa kimapenzi.
Kamanda wa Polisi mkoa wa Kagera, Augustino Ollomi amesema mauaji hayo yalitokea jana saa 6:00 mchana.

Akizungumza leo Mei 28, Kamanda Ollomi amesema mtuhumiwa anadaiwa kumpiga mumewe kwa kitu kizito kichwani na kumsababishia jeraha lililovuja damu nyingi na hatimaye kifo.

“Wanandoa hao wanadaiwa kuwa na ugomvi ambao chanzo chake tunaendelea kuchunguza; baada ya ugomvi huo mtuhumiwa alimpiga mume wake kichwani kwa kitu kizito kilichosababisha jeraha lililovuja damu nyingi na kusababisha kifo chake,” amesema Ollomi.

Kamanda huyo amewaasa wanandoa na wapenzi kutumia njia ya majadiliano, usuluhishi na sheria kutatua tofauti miongoni mwao badala ya kujichukulia sheria mikononi.

Matukio ya hivi karibuni ya mauaji ya wanandoa ni pamoja na la Muuguzi mfawidhi msaidizi wa hospitali ya wilaya ya Mkuranga, Rosemary Magombora (43), anayedaiwa kuuawa na mume wake kisha kufukiwa shimoni.

Tukio jingine ni la mhadhiri wa kompyuta wa Chuo Kikuu cha Dodoma (Udom), Rose Mdenye anayedaiwa kuuawa na mume wake, John Mwaikambo.
 
At 58 wivu wa kimapenzi,nilijua tukifika 50 ni menopause kumbe nye ge Bado zinachemka,Kuliko kuuana si bora waachane tu jamani.
Waachane au achepuke..! Menopouse na nyege ni two different things!
 
Duuh! Hii hali inaelekea kuwa kawaida sasa.

Tupendane kwa kiasi jamani na tujitahidi kuzizuia hasira pia.
 
Ndoa za mke mmoja ambazo hakuna kuachana ndo matokeo yake,walioleta dini wenyewe wanaachana sembuse sisi tulioletewa?
Hutosikia kamwe wanaooa wake mwisho wanne wameuana,kwa kuwa wakiona mapenzi nehi nehi basi kila mtu kwake.sasa hao ambao hadi kifo kiwatenganishe! Kweli kinawatenganisha.
Pole kwa familia husika.
 
eti wanasema umri huo genye zinarudi kama ulivyokuwa bint
At 58 wivu wa kimapenzi,nilijua tukifika 50 ni menopause kumbe nye ge Bado zinachemka,Kuliko kuuana si bora waachane tu jamani.
 
Tuangalie tulipokosea na kulekebisha lkn si kuuwana kama wanyama,kama mtu umechoka achaneni hapo watoto ndo wanaumia maana watakosa muangalizi.
 
Kuna watu huwa hawanaga option ya kuachana, wao huwa na option ya kumuua mwenza wake au kujiua full stop, sasa mwisho ni jela maisha.
 
Nafikiri waziri mwenye dhamana aje hapa akemee tabia ya kuandika habari za wapenzi waliouana kwa kuwa zinachochea wengi zaidi kuendelea kuuana!
Wazir hatasaidia kwa lolote lile. Hili suala ni more deep, maana linahusisha watu wawili tu... na emotional attachment ya muda mrefu.
Mapenz yalivyo na nguv, hata huyo wazir akigundua kitu yake inaliwa. Ataoiga mtu risas..
Usichezee na power of love
 
Basi kwa kuwa suala la mapenzi limeendelea kuwa la kuogofya, na kwamba ni jambo linalohusisha watu wawili na kwamba laweza kutokea la kutokea wakati wowote basi nishauri pawepo na safety gear kwa maana ya wapenzi kutakiwa kuvaa helmet kichwani, vest za kuzuia risasi huku sheria ya kumiliki vitu vyenye ncha kali ikiwemo visu ikitazamwa upya!
 
Aiseee" Haya Mauaji "" Mbona "" Yamezidi Kiasi Hiki ""..Sasa ""....Haya Mapenzi Haya MweeeHhh
 
Aiseee" Haya Mauaji "" Mbona "" Yamezidi Kiasi Hiki ""..Sasa ""....Haya Mapenzi Haya MweeeHhh
 
Ndoa za mke mmoja ambazo hakuna kuachana ndo matokeo yake,walioleta dini wenyewe wanaachana sembuse sisi tulioletewa?
Hutosikia kamwe wanaooa wake mwisho wanne wameuana,kwa kuwa wakiona mapenzi nehi nehi basi kila mtu kwake.sasa hao ambao hadi kifo kiwatenganishe! Kweli kinawatenganisha.
Pole kwa familia husika.
Mkuu unamaanisha kwamba kifo kuwatenganisha maana yake ndo hii?
 
Wanawake nao wameanza ku lipiza... Wanaume tukae chonjo...hii sasa ni vita
 
Mauaji kisa mapenzi ndio yanatrend kwasasa, wapenzi kuweni makini
 
Back
Top Bottom