Bukina Faso wangeshinda AFCON.

Bukina Faso wangeshinda AFCON.

Jacobus

JF-Expert Member
Joined
Mar 29, 2011
Posts
4,709
Reaction score
1,735
Nimeangalia mechi ya fainali ya kombe la Africa 2013 huko South Africa ni katika tathmin yangu kama Bukina Faso wangeandaliwa kisaikolojia kushinda mechi hiyo sasa hivi wangekuwa mabingwa wetu. Uwezo walikuwa nao.
 
uwezo gani siku waliyoigunga ghana walicheza zaidi ya kiwango chao cha kawaida na pamoja na kushinda mechi ile bado walikuwa wanafanya mambo ya kizembe sana ningeshangaa kama wangechukua kombe.
 
Nimeangalia mechi ya fainali ya kombe la Africa 2013 huko South Africa ni katika tathmin yangu kama Bukina Faso wangeandaliwa kisaikolojia kushinda mechi hiyo sasa hivi wangekuwa mabingwa wetu. Uwezo walikuwa nao.
Fafanu hapo kwenye red, mabingwa wenu wewe na nani?
 
Fafanu hapo kwenye red, mabingwa wenu wewe na nani?
Mkuu mashindano haya ni ya bara la Africa, kwa hiyo kuwa mabingwa WETU ni kuwa mabingwa wa Africa, Tanzania ni moja ya nchi ndani yake!!!!!!!!
 
Mkuu mashindano haya ni ya bara la Africa, kwa hiyo kuwa mabingwa WETU ni kuwa mabingwa wa Africa, Tanzania ni moja ya nchi ndani yake!!!!!!!!
Ha ha haaa, the way unaongea ni kama vile wewe ni mutu ya bukina ndo maana inakuwa ngumu kumeza..!
 
Fafanu hapo kwenye red, mabingwa wenu wewe na nani?
hujaelewa mabingwa wetu sisi wasindikizaji (TZ) maana kuingia huko ni ndoto kazi yetu kuangalia wenzetu waocheza kwenye TV.
 
hujaelewa mabingwa wetu sisi wasindikizaji (TZ) maana kuingia huko ni ndoto kazi yetu kuangalia wenzetu waocheza kwenye TV.
Sawa kabisa, na wanaoichukia Bukina Faso ni wale wanaorejea historia kuwa hawa tuliwafunga, wakati wenzetu hawalali kwa kufikiria maendeleo ya kesho sisi tunabaki kuwarejesha wachezaji "washikaji" kwenye timu tule nao vizuri. Kama japo kidogo tungefuata program ya Maximo na sie tungeenda South Africa.
 
Huyu mfungaji Sunday Mba,kweli ni sunday,maana kila sunday(j2) anafunga goli,aliwafunga Ivory Coast pia J2 iliyopita
 
Back
Top Bottom