Building a business Model-Kuna umuhimu?

Masokotz

JF-Expert Member
Nov 26, 2018
3,470
5,468
Habari za wakati huu;
Moja kati ya ya changamoto zinazowakaili wajasiriamali wengi huwa zinasababishwa na kutokuelewa hasa msingi wa muundo wa biashara yao(Business Model) Wengine huanza biashara ila kuwa na business model na wengine hujikuta wakianza vizuri ila wakifika katikati wanaacha kuzingatia kutengeneza model nzuri na matokeo yake ni kujikuta wakiwa katika changamoto za kibiashara.

Business Model inahusisha mfumo wa usimamizi(Management)Mfumo wa uendeshaji(Operation and Production)Mfumo wa masoko na mfumo wa fedha.Kwa pamoja hii mifumo inapofanya kazi kwa kushirikiana vizuri inatengeneza Business model.Biashara yako inaweza kuwa ni B to B au B to C au B to B to C ambapo B ni Business na C ni Consumer.Unapotaka kuanzisha biashara yoyote ile kuwa au ndogo,business model ndio inaweza kukuhakikisha mafanikio yako.Kama business model yako sio sahihi basi uwezekano wa kufanikiwa ni mdogo.

Karibu tujadili hapa umuhimu wa kuwa na business model na namna ambavyo tunaweza kutengeneza mfumo wenye tija katika biashara zetu.

Karibuni
 
Kuwa na business model ni muhimu sana hasa kama utahitaji investors wa kuwekeza katika biashara yako hiyo ndo inawapa uhalisia wa kutengeneza faida kutoka katika biashara yako .
 
Business model nini kwa maana ingine? Ni kuweza kupunguza cost ili kuongeza profit? Au ni kuweza kuongeza sells ili kuongeza profit? Au ni nini??
 
Business model nini kwa maana ingine? Ni kuweza kupunguza cost ili kuongeza profit? Au ni kuweza kuongeza sells ili kuongeza profit? Au ni nini??
Ni vyote kwa pamoja.Mwisho wa siku ni lengo kuu ni kutengeneza faida.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom