Budget hapo baadae msaada

Budget hapo baadae msaada

Ndan ya box

Senior Member
Joined
Jun 2, 2014
Posts
159
Reaction score
44
Mchumba mtarajiwa mshahara laki nne, mimi laki tatu, nyumba kodi ni ni 150,000+usafiri +matumizi ya vitu vidogovidogo kwa ajili ya home+maji ya kununua coz maeneo nakoishi maji kutoka ni kwa nandra sana.

Wana JF msaada tafadhali bado sijaoana na huyu mtu ila tunatarajia na hatuishi pamoja,nampenda msaada kwa wenye ndoa nipange vipi badget hapo nipo tayari kuanzisha hata kabiashara lakin pia kabiashara kapi?
 
Usiwaze budget kabla hujaoa...hayo mambo madogo sana.
 
Hold on a bit. Wote sasa hivi mnajitegemea?
KAMA NDIO: Mkikaa pamoja nadhani kiwango cha fedha cha kuhifadhi(save), kitaongezeka...kama mmeweza kuishi na viapato hivyo hamuwezi kushindwa mkiwa pamoja.
KAMA SIVYO: Inabidi muangalie kama kila mtu anaweza kujitegemea kwa kipato chake. Kama mnaweza (Refer option one). Kama hamuwezi basi jadilini njia za kupunguza matumizi na kuongeza kipato kisha muanze kufanyia kazi mlichojadili wakati mipango ya kuishi pamoja ikiendelea.
Ila 700,000/- kwa familia ya kitz isiyo na makuu mnaweza survive.
 
Unaweza kuoa ila siyo lazima muishi pamoja...kama unaona kuoa ni dili oa then kila mtu awe na kwake mtakuwa mtatembeleana na kukutana popote mtakapopanga mkitaka tendo la ndoa baada ya ndoa.
 
Mmmh nyumba inakula nusu ya mshahara wa mmoja wenu... labda waweza liangalia hilo upya.
Pili anzisheni biashara... aina ya biashara inategemea na opportunities za mahali mnapoishi na kama una savings au unaweza kupata mtaji mpaka wa sh ngapi
 
Kwa dar es salaam huwezi pata nyumba stardandard chin ya bei hiyo ukipata ndo ile hata akija mgeni wako hutataman anapoishi hapo naposema mm hata leo hii nikipata mgeni kama kikwete pale anaweza hamia kabisa
 
kwa hiyo we unaangalia watu!!!!!!!!!!!!!!!!
 
Hapana sitazami watu ila hapana kwa kweli kuna nyumba dar hutaman hata kuziangalia kwa macho
 
tafuta another income...uzeni barafu au juice hivi kidogo kidogo au fugeni kuku
 
Buni miradi midogo midogo haraka iwezekanavyo
 
Mchumba mtarajiwa mshahara laki nne, mimi laki tatu, nyumba kodi ni ni 150,000+usafiri +matumizi ya vitu vidogovidogo kwa ajili ya home+maji ya kununua coz maeneo nakoishi maji kutoka ni kwa nandra sana.

Wana JF msaada tafadhali bado sijaoana na huyu mtu ila tunatarajia na hatuishi pamoja,nampenda msaada kwa wenye ndoa nipange vipi badget hapo nipo tayari kuanzisha hata kabiashara lakin pia kabiashara kapi?

yaani kipato cha laki saba familia alafu unaogopa kuowa? ni watanzania wangapi wanapata kipato hicho na wameowa? kwa wastani watanzania wanaishi chini ya dola moja kwa siku sasa wewe unayepata zaidi ya dola 15 kwa siku hujioni uko mbali sana?

watu hawachelewi kuowa kwa sababu ya garama bali ni mambo tu ya ubize na tamaa ya vibinti tofauti tofauti mtaani. watu tuna mshahara wa laki moja unusu tunalea familia zaidi ya 10 yrs , wewe laki saba unajiuliza? embu kaulize wanaofanya pale kwa backresa wakuambie wanalipwa kiasi gani? hakuna anayepata zaidi ya laki na nusu lakini wanalea familia.
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom