Buddha 3 | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Buddha 3

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by Andrew Nyerere, Dec 3, 2009.

 1. Andrew Nyerere

  Andrew Nyerere Verified User

  #1
  Dec 3, 2009
  Joined: Nov 10, 2008
  Messages: 3,025
  Likes Received: 1,206
  Trophy Points: 280
  .ExternalClass .ecxhmmessage P{padding:0px;}.ExternalClass body.ecxhmmessage{font-size:10pt;font-family:Verdana;} .
  Kama alivyotueleza ,Gautama alikuwa na njia nyingine ya kuuelekea ukweli,njia iliyoitwa''Njia ya Katikati.'' Uzoefu alioupata Gautama ulikuwa kwa hakika wa aina mbili;alizaliwa kama mwana wa mfalme na starehe na anasa za aina yote,na uwezo wa kupata wanawake wengi wacheza dansi[macho ya Mwalimu wa Kihindi yalionyesha hamu!] na chakula chote alichoweza kula,na raha zote alizoweza kustarehe,halafu kutokea hapo,akawa fakiri kabisa,na mateso mengi,kufikia karibu afe kwa kukosa mahitaji ya msingi na kwa njaa. Lakini,kama Gautama alivyoelewa vizuri,siyo utajiri au matambara yalikuwa na ufunguo wa tatizo la milele la Binadamu. Jibu lazima liwe mahali fulani kati kati yake.

  Ubuddha mara nyingi unaonekana kama ni dini,lakini siyo dini kama ukichukua maana halisi ya hilo neno. Ubuddha ni njia ya maisha ,kanuni ya kuishi ambapo,kama tu mtu akiifuata kanuni hiyo kikamilifu,matokeo fulani yatatokea. Kwa kurahisisha mambo Ubuddha unaweza kuitwa dini,ingawa kwetu sisi ambao ni mapadre wa kweli wa Kibuddha'dini' siyo neno sahihi,jina sahihi ni '' Njia ya Kati Kati '' tu.

  Ubuddha ulianzishwa kutokana na Mafundisho ya dini ya Kihindu. Wanafalsafa wa Kihindu na Walimu wa dini walifundisha kwamba njia ya kuifahamu nafsi,kuifahamu roho,na kazi zilizokuwa zinawakabili binadamu ni kama mtu anaetembea kwenye ncha ya wembe ambapo ukiegemea kidogo tu upande mmoja au mwingine utaanguka.

  Gautama aliyafahamu mafundisho yote ya Kihindu kwa sababu mwanzo wa maisha yake alikuwa Mhindu. Lakini kwa juhudi zake mwenyewe akagundua Njia ya Kati Kati.

  Kujinyima kupita kiasi ni mbaya, inasababisha maoni yaliyopotoka;kustarehe kupita kiasi pia ni vibaya kwa sababu pia inaleta maoni yaliyopotoka. Mtu anaweza kufaidika kwa kutazama hali ilivyo katika kurekebisha nyuzi za chombo cha . Kama ukikaza sana nyuzi ya chombo kama gita,hatimaye itafikia kiwango cha kukatika kiasi kwamba ukiigusa kidogo tu inakatika,na inakuwepo, katika hii hali ya kukaza sana, ukosefu wa muafaka.

  Kama mkazo ukilegezwa sana katika nyuzi za chombo utaona tena kwamba hakuna muafaka,unaweza tu kupata muafaka wakati nyuzi zimerekebishwa sawa na zimekazwa kwa kiasi fulani. Hivi ndivyo ilivyo katika dunia ambapo anasa au mateso kupita kiasi zinaondoa muafaka.

  Gautama alialiianziasha mfumo wa imani katika Njia ya Kati Kati na akatunga kanuni ambazo mtu anaweza kuwa na furaha,kwa sababu moja ya misemo yake ulikuwa kwamba'' Furaha yule anayeitafuta ataipata,kama akifanya mazoezi ya kuipata''

  Kati ya swali la kwanza kabisa mtu analouliza ni,''Kwa nini sina furaha?'' Ndilo swali linaloulizwa mara nyingi kuliko yote. Gautama Buddha aliuliza kwa nini hana furaha,alifikiria na kufikiria,na akawaza kuhusu jambo hili,na akawaza kuzunguka jambo hili. Akafikia uamuzi kwamba hata mtoto aliyezaliwa leo anateseka,mtoto alieyezaliwa leo anateseka kwa ajili ya mateso ya kuzaliwa,kwa sababu ya maumivu na kukosa kustarehe wakati wa kuzaliwa na kuiacha dunia ya raha aliyokuwa anaifahamu. Wakati watoto hawana raha wanalia,wanapokuwa wakubwa,labda hawawezi kulia lakini wanaweza kutafuta njia ya kuonyesha kwamba hawapendezwi,kwamba hawaridhiki au kwamba wako katika mateso kweli. Lakini mtoto hafikirii kwa nini analia,analia tu,anafanya mambo kama mashine. Mambo fulani yanamfanya mtu alie,mambo mengine yanamfanya mtu acheke,lakini-maumivu-yanakuwa tatizo pale tu watu wanapouliza kwa nini nateseka,kwa nini sina furaha?
  .
  Utafiti umeonyesha kwamba karibu watu wote wameteseka kiasi fulani kabla ya kufikia umri wa miaka kumi na pia wameshangaa kwa nini imewabidi kuteseka. Lakini katika hali ya Gautama hili swali halikutokea mpaka alipokuwa na umri wa miaka thelathini,kwa ajili wazazi wa Gautama walifanya kila waliloweza kuzuia asivumile mateso ya aina yoyote yale. Watu ambao wamelindwa kupita kiasi au wamedekezwa kupita kiasi hawajui jinsi ya kukabiliana na kukosa furaha,kwa hiyo wakipata masaibu hawako katika hali ya kuyatanzua na mara nyingi wanachanganyikwa akili.

  Kila mtu unafika wakati ni lazima atakumbana na mateso,na kukumbana na sababu ya kuwepo mateso. Kila mtu lazima avumilile mateso ya mwili,akili au roho,kwa sababu bila mateso haiwezekani duniani kuwepo kujifunza kokote,haiwezekani kuwepo utakaso au kuondoa utandu ambao sasa umeizunguka roho ya mtu.

  Gautama hakuanzisha dini mpya , mafundisho yote ya Gautama,mchango wake wote katika elimu ya binadamu,umelengwa au unahusu tatizo la maumivu au furaha. Wakati alipokuwa anatafakari,wakati wanyama wa porini walipokaa kimya ili aweze kutafakari bila kusumbuliwa,na wakati konokono walipokipooza kichwa chake kilichounguzwa na jua,Gautama alihisi maumivu,alielewa sababu ya maumivu,na akaamini kwamba anajua jinsi ya kuyashinda maumivu. Aliyafundisha haya kwa wale wafuasi wake watano,na mambo aliyofundisha yamekuwa yanaitwa nguzo nne ambapo Ududdha wote umejengeka. Ndizo Kweli Nne Tukufu,ambazo tutazijadili baadaye.

  Vivuli vya usiku vilikuwa vinashuka,giza lilikuwa linaingia upesi kiasi kwamba hatukuweza kuonana. Yule Mwalimu wa Kihindi alikuwa dirishani na ,umbo lake lilikuwa linaonekana kwa mwangaza wa nyota. Aliendelea kuongea,huku amesahau au hajali kuwa sisi watoto ilibidi tuamke kwa ibada ya saa sita usiku,ilibidi tuamke kwa ibada ya saa kumi usiku,halafu ilibidi tuamke tena saa kumi na mbili asubuhi.

  Baadaye akaonekana kama amegundua kwamba ameanza kuchoka,akaanza kuona kwamba alivyokuwa amesimama pale dirishani amezipa mgongo nyota labda alikuwa anapoteza muda wake kwa sababu hakuweza kutuona,hakuweza kujua kama tunamsikliza ,au kama tumelala tulivyokaa.

  Ghafla akaipiga fimbo chini kwenye meza kwa nguvu,''THWANG''. Kelele ilikuwa kubwa na haikutegemewa kiasi kwamba labda kulikuwa na inchi kadhaa kati ya miili yetu na sakafu. Halafu wote tukaanguka chini,kwa sauti kubwa na kutoa milio ya mshangao.

  Yule Mwalimu wa Kihindi alisimama pale kwa muda,halafu kasema ''Dismiss,''na akaondoka kutoka kwenye chumba. Ilikuwa ni rahisi kwake,nikafikiria,yeye alikuwa ni mgeni tu,alikuwa na privilege maalum,hakuna mtu aliyekuja kumuuliza swali lolote. Aliweza kwenda sasa katika chumba chake na kupumzika usiku kucha kama akitaka. Lakini sisi ilibidi twende kwenye ibada katika Hekalu.
   
 2. MziziMkavu

  MziziMkavu JF-Expert Member

  #2
  Dec 3, 2009
  Joined: Feb 3, 2009
  Messages: 39,616
  Likes Received: 4,617
  Trophy Points: 280
  Ni kweli usemayo Mzee ganesh nakukubalia Budha sio Dini
   
Loading...