Bubu ni watu makini sana kwenye usimamizi wa kazi

na wewe

JF-Expert Member
Jan 4, 2019
231
397
Za muda huu usomapo huu ujumbe au Uzi.

Niende kwenye mada moja kwa moja. Katika siku chache zilizopita tuliamua kuzunguka hapa mjini Mwanza mimi na marafiki zangu ambao hawakai Mwanza. Baada ya kufurahia mazingira ya rock beach pale tuliamua kuvuka kwenda Kamanga na kurudi, nia ilikuwa wale marafiki wahisi usafiri wa majini/ziwani ukoje.

Sasa tulipofika Kamanga sehemu ya kuonesha tiketi Ili tuingie, yupo bubu pale ndio msimamizi getini na wako pande zote mbili za kivuko.

Kitu nilichowaza ni kwamba, kwa nini boss wa pale ameamua kuweka bubu na sio mtu wa kawaida ambaye anaweza kusikia na kujibizana na wateja kwa mdomo, kwa kuwaelekeza namna ya kusubiri ferry.

Kitu nilichogundua ni kuwa, bubu anachotaka ni wewe ufate maelekezo yaliyopo na sio vinginevyo. Bubu hana majadiliano nje ya kile alichoambiwa na bosi wake. Bubu hana muda wa makubaliano ya kupitisha jambo nje ya kuangalia stakabadhi hivyo ni lazima ulipe tu. Bubu hana lugha ya siri kama sisi kuwa "wewe niachie nitakupa vocha"

Bubu hana lugha ya kujificha hivyo rushwa kwake ni asilimia ndogo sana kufanyika. Bubu hana mambo ya kujuana. Mfano hai ni kwamba, kuna bubu mdada nilimkuta upande wa pili. Yule Dada ni mteja wangu pale kubandani kwangu na kila mara akitoka kazini huwa anapitia mahitaji yake pale dukani na huwa tunaogea naye na kucheka. Lakini nilipomuona hakuwa na kufahamiana muda wa kazi au kuniamini zaidi alitaka nifate sheria.

Mwisho natoa pongezi kwa uongozi wa Kamanga Ferry kwa kuliona hili na mimi pia nimejifunza kupitia wao.
 
Mkuu, ebu naomba namba ya sim ya huyo bubu mdada. Maana tayari kuna jambo nimejifunza kupitia uzi huu..
 
Back
Top Bottom