Bsc in Environmental Engineering at ARU | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Bsc in Environmental Engineering at ARU

Discussion in 'Jukwaa la Elimu (Education Forum)' started by mujoma2011, Mar 6, 2012.

 1. m

  mujoma2011 Member

  #1
  Mar 6, 2012
  Joined: Jun 2, 2011
  Messages: 6
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Naomba kujua hasa kuhusu hii course ya BsC in Environmental Engineering inayotolewa hapa ARDHI UNIVERSITY (zamani UCLAS).
  Kwa hapa bongo ni kazi gani hasa hawa watu wanafanya na vipi kuhusu market yake hapa tanzania(je inalipa?).ipi tofauti kati ya Civil engineer na Environmental engineer maana hapa course zake hazina tofauti sana na hawa civil ingineer.
  Naomba kueleweshwa wadau,hasa hasa wadau ambao wanfanya kazi katika fani hii, waliosoma au wanaosoma hii course katika hiki chuo,wana ARU.
  Mawazo kwa yeyote anayejua pia yanakaribishwa.
   
 2. M

  Mpigaji JF-Expert Member

  #2
  Mar 6, 2012
  Joined: Feb 6, 2011
  Messages: 386
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Ina soko katika makampuni ya kuchimba madini!
   
 3. Foundation

  Foundation JF-Expert Member

  #3
  Mar 6, 2012
  Joined: Nov 25, 2010
  Messages: 1,458
  Likes Received: 256
  Trophy Points: 180
  Ungetuwekea course outline ya civil na environment tungeweza kutoa majibu sahihi. Ila ninachojua hizi course zina mwingiliano lakini sio mkubwa sana kama ilivyo architecture na civil au building economics na civil. Ukumbuke civil yenyewe ni pana sana, kuna water,highway na structure. Sidhani kama environment engineer anaweza akawa anajua kugusu design and detailing ya madaraja,majumba,minara,matank ya maji,Finite element analysis nk, sidhani kama anajua kuhusu steel,timber and concrete. Sidhani kama anajua kuhusu design ya barabara( Hapa nazungumzia pavement na geometrical design).
  Sijui kama anajua kuhusu water and waste water system, hasa kuhusu closed and open channel system.

  Kwa ufupi progamme nyingi WAMEZIGATUA toka Civil engineering(Soma historia ya civil)

  Ushauri: Tafuta course outline ya environmental engineering then linganisha na haya uone kama vinaendana
   
 4. k

  kongabh New Member

  #4
  Mar 6, 2012
  Joined: Feb 14, 2007
  Messages: 1
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Environmental Engineering course ipo very wide na kwa Tz wengi waliosoma hii course wanafanya kazi ktk sehemu zifuatazo;
  1. Mamlaka za Maji kama Water Engineers or Sewerage Engineers
  2. Wizara ya Maji kama Wahandisi wa maji pia wahandisi mazingira
  3. Wizara ya Kilimo na Chakula ktk idara ya umwagiliaji kama wahandisi mazingira
  4. NEMC kwa ajili ya Environmental Impact Assessment
  5. TAMISEMI kama wahandisi wa maji wa wilaya, DWE
  6. Migodini kama Environmentalists
  7. Kwa Consultants wanaofanya designs za miradi ya maji huwa wanakuwa involved kama Water Supply/Sewerage Engineers kwa ajili ya water supply/sewerage network design and system modelling.

  Wengi wa hawa ni wale waliosoma kipindi cha UCLAS, ingawa baada ya kuwa ARU course hii imegawanyika sana kuunda idara zenye specializations tofauti lakini kama uta specialize ktk Environmental Engineering ujue utaangukia ktk moja ya hizo idara hapo juu.
   
Loading...