Brucela ninini! | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Brucela ninini!

Discussion in 'JF Doctor' started by KYALOSANGI, Jan 30, 2012.

 1. KYALOSANGI

  KYALOSANGI JF-Expert Member

  #1
  Jan 30, 2012
  Joined: Jan 21, 2011
  Messages: 1,890
  Likes Received: 468
  Trophy Points: 180
  Kijana wangu (YUPO MBALI NAMI) ameniambai anaumwa ugonjwa unaitwa bucela (sins uhskiks ns spelling zake)
  Kwa kuwa nakaribia kunza mitihani ya semister ameshauriwa asianze dozi yake kwani itamleteamatatizo wakati huo;Naomba kujua huu ni ugonjwa gani na usababishwa na nini ,kuna tiba mbadala !
  je maelekezo ya huyo daktari wake ni sahihi(mitihani wanaanza tarehe 13 hadi mwisho wa mwezi wa pili!
   
 2. Ngongo

  Ngongo JF-Expert Member

  #2
  Jan 30, 2012
  Joined: Sep 20, 2008
  Messages: 12,155
  Likes Received: 3,632
  Trophy Points: 280
  Google muzee.
   
 3. n

  ngwana ongwa doi Member

  #3
  Feb 1, 2012
  Joined: Dec 26, 2011
  Messages: 75
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Brucella ni bacteria wanaosababisha ugonjwa unaoitwa brucellosis.bacteria hawa hupatikana kwa wanyama kama ng`ombe,mbuzi,kondoo,nk.

  Brucellosis ni ugonjwa unaosababishwa na kula nyama yenye brucella,au kunywa maziwa yenye brucella yanayopatikana kwa wanyama niliotaja hapo juu,au mtu anapokuwa na kidonda na kuwa na contact na wadudu hao kwenye kidonda mara nyingi wawindaji,mara chache sana kwa kuwavuta(inhalation).

  Dalili zake.
  homa,kutokwa jasho,kuumwa kichwa,kuumwa mgongo/shingo,mafua,joint kuumwa,uchovu.

  kujibu swali lako kwamba DK.amemwambia asianze kutumia dawa ni sawa kabisa kutokana na ukweli kwamba dozi ya kutibu brucella inachukua muda mrefu,kumbuka mtu akiwa anatumia dawa mwingine zinaweza kumchosha ukiachana na side effects ndogondogo ambazo zinaweza kumaffect ukizingatia ni wakati wa mitihani.Hakuna mbadala wa kutibu brucellosis.
  Matibabu yake.
  Matibabu yake ni antibiotics, kwa mtu mzima doxycycline 100mg mara mbili kwa siku+rifampicin 600mgx1(mara moja kwa siku) kwa wiki sita mfululizo,au streptomycine inj. i/m 1gm x1 kwa siku 14,au gentamycin 5mg/kg ,kama akitumia dox.peke yake 100mgx2 ni kwa siku 45.sasa itategemea dk.wake amemwandikia dawa gani.

  kinga.
  kuchemsha maziwa vizuri kabula ya kunywa,kupika nyama ziive vya kutosha badala ya kukimbilia mkono kwenda kinywani tehe tehe!
   
Loading...