Nicolas J Clinton Gabone
JF-Expert Member
- Mar 13, 2014
- 897
- 559
Mradi huu siyo mkubwa sana lakini umetumia miaka mitano!
Mradi huu unahusisha Barabara za Kilwa, Bandari na Kawawa, miaka mitano sasa unajengwa na kampuni ya Kichina ya SINOHYDRO na la zaidi kampuni hii imepewa kandarasi ya kujenga BRT PHASE III!
Kinachoshangaza sasa ndani ya miaka hiyo mitano ya mradi huu, barabara hizi tayari zimejaa mashimo kwenye baadhi ya maeneo na wanaziba hata pale wanapoziba bado panapasuka ikizingaitiwa barabara hii bado kuanza kwa matumizi yake, kwa sasa barabara hii eneo la Mbagala lote wanaweka viraka na kukata maeneo yenye mashimo mashimo ili kufanya repair Imagine!
Tuliambiwa mradi huu mpaka March 2023 utakuwa umekabidhiwa lakini sioni dalili hizo kukamilika kwa mradi huo ndani ya kipindi hicho, kwenye station za Bus wanajenga na kuvunja!
Sijui tatizo ni Viongozi wetu hawa waliyo pewa dhamana ya kulinda maslahi ya Taifa kuwa wazembe katika kusimamia maslahi ya Taifa au nao wanahusika katika uozo huu au wanatoa kandarasi kwa RUSHWA! Fedha ni zetu Ardhi yetu bado miradi inayotekelezwa na makampuni ya kigeni wanafanya ujinga huu kwa nini?
Mkandarasi huyu anaendelea na ujuzi wa BRT PHASE III barabara ya Nyerere na Uhuru, sasa Viongozi wetu wanaotakiwa kusimamia maslahi ya Taifa hawaoni haya madudu ya kampuni hii ya
SINOHYDRO? kwa nini Viongozi hawafuatilii kwa ukaribu sana hii miradi mizuri inayotumia fedha nyingi sana, mradi wa BRT ni mzuri sana tena sana ila kuna mambo ya kuyasimamia kutoka kwa walinzi wa maslahi ya Taifa ila wako kila mtu bize sijui kufanya nini?
Niwaombe sana Viongozi wetu kusimamia maslahi ya Taifa letu kwa wivu mkubwa sana mtu asicheze na maslahi yetu kama Taifa, kama kampuni inajenga ijenge kwa standard, lakini siyo haya ya BRT PHASE II! sijui baada ya miaka kadhaa ya matumizi ya barabara hiyo itakuweje ukilinganisha na BRT PHASE I.
Nimeona serikali imepata fedha za BRT PHASE 4&5 tafadhali sana tutumie fedha zetu kwa thamani yake na muda uzingatiwe kwa makampuni yanayopewa kandarasi.
Ningekuwa kwenye nafasi ya maamzi wanaosimamia mradi huu na Kampuni yenyewe wangatafuta pa kwenda tu.
Tusiwe wazembe kiasi hicho Watanzania na hasa nyie Viongozi wetu, SINOHYDRO ni kampuni kubwa sasa sijui kwa nini kwenye huu mradi imeboronga?