Brig.Gen.Moses Nnauye akumbukwa na wanamuziki | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Brig.Gen.Moses Nnauye akumbukwa na wanamuziki

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by KIM KARDASH, Dec 13, 2011.

 1. K

  KIM KARDASH JF-Expert Member

  #1
  Dec 13, 2011
  Joined: Sep 21, 2011
  Messages: 5,083
  Likes Received: 60
  Trophy Points: 145
  [h=3]Wanamuziki wamkumbuka Brig Gen Moses Nnauye [/h]Na John Kitime


  Mzee Nnauye alikuwa mwanamuziki mzuri sana na alitumia sana muziki katika harakati za kupigania uhuru. Alianzisha na kuendeleza vikundi vingi vya kwaya, taarab na bendi na wasanii wengi sana waligunduliwa nae na kulelewa kama wanawe kutokana na kutaka waendelee katika muziki.
  [TABLE="class: tr-caption-container, align: center"]
  [TR]
  [TD="align: center"][​IMG][/TD]
  [/TR]
  [TR]
  [TD="class: tr-caption, align: center"]
  Mzee Nnauye wakati akiwa Mkuu wa Mkoa Singida
  [/TD]
  [/TR]
  [/TABLE]

  Kila nikisikia wimbo wa Guantanamela huwa namkumbuka Mzee huyu ambaye kwa mara ya kwanza nilikuwa karibu nae mwaka 1987, wakati niko katika bendi ya Tancut Almasi, wakati huo tukiwa tumepiga kambi ya miezi kadhaa Dodoma Hotel. Alitukaribisha wanamuziki kadhaa nyumbani kwake na kutuonyesha santuri(LP) ya wimbo original version ya Guantanamela. Kisha akamuita mwanae atupigie wimbo huo katika kinanda kuanzia hapo kila mara nilikuwa karibu na mzee huyu. Mzee Nnauye ndiye aliyegundua kipaji cha Mheshimiwa Capt John Komba na kumtoa katika kazi yake ya ualimu na kumuingiza jeshini kuendeleza kipaji chake cha uimbaji, matokeo yake wote tunayajua. Wakati akiwa Singida aliweza kuwavuta wanamuziki kadhaa kutoka Black Star na Lucky Star za Tanga, na wanamuziki kadhaa akiwemo Wazir Ally wa Kilimanjaro Band walihamia huko na kuwa wanamuziki wa bendi King'ita Ngoma iliyokuweko Singida wakati huo. Wote tunajua umahiri wa Waziri Ally.

  Katika mazungumzo yetu ya mara ya mwisho alikuwa anatamani sana kulileta lile kundi la Africando, mapigo ya Kilatino ya kundi hili yalimfurahisha sana na alikuwa anaona itakuwa bora kwa Watanzania kupata vionjo tofauti na vilivyozoeleka ambavyo vilikuwa ni kutoka kwa wanamuziki wa Soukus tu kutoka Jamhuri ya Congo.
  Mungu amlaze pema Mzee Moses Nnauye
  Amen
   
 2. O

  Ogah JF-Expert Member

  #2
  Dec 13, 2011
  Joined: Mar 10, 2006
  Messages: 6,229
  Likes Received: 71
  Trophy Points: 145
  sasa wewe Kitime inabidi ufanye kweli ulilete hilo kundi la Africando..........hapa bongo
   
 3. K

  KIM KARDASH JF-Expert Member

  #3
  Dec 13, 2011
  Joined: Sep 21, 2011
  Messages: 5,083
  Likes Received: 60
  Trophy Points: 145
  kweli mdau naungana na wewe JFK awalete jamaa mi mwenyewe nawakubali sana,lakini hata Nape Pia tunaweza kumuomba awalete kutimiza ndoto za mzee!
   
 4. Losomich

  Losomich JF-Expert Member

  #4
  Dec 13, 2011
  Joined: Nov 9, 2011
  Messages: 373
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  Inavyo onekane mzee Nnauye alikuwa active sana katika kuyasimamia yale anayoyaamini. Lakini huyu mwnaye aitwae Nape haelekei hata kidogo kufuata nyao zake. Huyu Nape ni mtu mwoga sana asiyejiamini wala kusimamia yale anayoyaamini, chukua mfano sakata la uanzishwaji wa CCJ, na kampeni za kuvuana magamba. Huyu Nape hasistahili kuitwa kuwa mwana wa Nnaye!!!
   
 5. K

  KIM KARDASH JF-Expert Member

  #5
  Dec 13, 2011
  Joined: Sep 21, 2011
  Messages: 5,083
  Likes Received: 60
  Trophy Points: 145
  Ni mwanae mzee na alimpatia huko huko singida alipokua mkuu wa mkoa huko!
   
 6. Ndahani

  Ndahani JF-Expert Member

  #6
  Dec 13, 2011
  Joined: Jun 3, 2008
  Messages: 14,314
  Likes Received: 1,784
  Trophy Points: 280
  Mzee Nnauye alikuwa mahiri wa nyimbo na kale kamchezo ketu kale...but was a very nice chap. I hope Musa atafuata nyayo za baba yake
   
 7. Matola

  Matola JF-Expert Member

  #7
  Dec 13, 2011
  Joined: Oct 18, 2010
  Messages: 36,045
  Likes Received: 13,265
  Trophy Points: 280
  Mkuu naomba kujuwa uhusiano wa kifamilia kati yako na familia ya Nnauye, maana naona hata huyo Nape hajajigeuza kuwa msemaji wa familia kama ulivyojipambanuwa wewe kwa takribani wiki nzima sasa.
   
Loading...