Responded Ukienda BRELA bila kucheza na Mawakala wakati wa kusajili Kampuni, Biashara... n.k HUTOBOI

Candela

JF-Expert Member
Joined
Aug 12, 2021
Posts
909
Reaction score
2,485
BRELA imekuwa mwiba kwa sasa, hawatoi huduma kama hujawapa kakitu, kumekuwa na hawa mawakala wanaosajili makampuni na majina ya biashara, sasa ukiwatumia wale wanakwambia weka na Sh 50,000 ya ku-push kule ndani.

Ikitokea hujawatumia hawa mawakala ukienda BRELA ORS mwenyewe ukatuma maombi yatasubiri sana aisee, yaani wale walioko kule ndani hawa deal na maombi ya kwenye mfumo kama huja-push na njia pekee ya kupush ni lazima uwape mawakala wakufatilie jambo lako.

Hii inakera sana hasa pale unapokuwa umelipia gharama zote zinazohitajika. Bora ingekuwa unalipia baada ya kupatiwa huduma unaweza kuahirisha.

Kibaya zaidi mfumo wa BRELA haukuruhusu kufanya maombi mapya kama la zamani halijamalizwa, so hata ukitaka ulifute utafute watu wakusaidie bado utakwama.


MAJIBU YA BRELA



 
Habari, BRELA haina Wakala kwa ajili ya huduma ya usajili wa kampuni, huduma ya kusajili kampuni hutolewa moja kwa moja kwa njia ya mtandao kupitia bos.brela.go.tz, malipo ya huduma za BRELA hufanyika kupitia kumbukumbu namba ya malipo (control number) inayotolewa na mfumo wa malipo ya Serikali GEPG.
 
Vipi kuhusu kutoshughulikia maombi ya mfumo kwa wakati?
 
Vipi kuhusu kutoshughulikia maombi ya mfumo kwa wakati?
Habari, BRELA hufanyiwa kazi maombi yote kwa wakati, tunaomba namba ya ombi lako ambalo bado hujapokea majibu yako kwa wakati kwa ajili ya msaada zaidi.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…