BRELA: Faida na hasara za kusajili 'partnership' ukilinganisha na za 'company'

No_Worries

Member
Sep 27, 2016
69
23
Wakuu,

Hivi kwa wale wenye ujuzi naomba kueleweshwa faida na hasara za kuregister biashara Brela kama partnership ama company. Ni vitu gani hasa inatakiwa kuviangalia (kodi? capital? aina ya biashara?)? Walioregister biashara zao kama partnership watupe uzoefu wao lakini wale walioregister kama kampuni nao pia watupe uzoefu wao.

Tafadhali
 
Mkuu hakikisha una uelewa mzur kuhusu maneno "patnership" , "company" ,"Sole", na "Limited" halafu ndo tuendelee

Mkuu sijakupata, neno kama neno la Kiingereza linaweza kuwa na maana tofauti likitumika kwenye fani/profession fulani. Ninachouliza ni faida na hasara za KIBIASHARA za kuregister shughuli yako kama partnership/firm ama Company.
 
Nimekwamia hapa, sielewi nichague kipengele kipi, saidia tafadhali

Screen Shot 2017-03-31 at 01.02.56.png
 
Asante mkuu, nimezipitia hizo threads ila bado sijapata maelezo fasaha ya utofauti wa Kibishiara kati ya Partnership na Company.
Tatizo lako hujaeleweka nadhani unamaanisha tofauti iliyopo kati ya:

1.Company Limited

2.Sole Proprietorship

3.Corporation

4.Cooperation

Mimi bado sijajua vizuri kama Compay Limited ndo pia inaandikwa Limited Liability Company nadhani wanaofahamu watu watatusaidia,

Pia kuna kampuni zinatumia eg Mkaruka Pvt Limited, kama ingetokea mtu akatusaidia ingekaa poa sana
 
Asante mkuu, nimezipitia hizo threads ila bado sijapata maelezo fasaha ya utofauti wa Kibishiara kati ya Partnership na Company.
Pole sana.Hata mie nilikwama lakini angalia upande wa kulia wa hiyo website na majina na nanmba za simu.Nilipiga na kumpata mmojawapo na akanielekeza vizuri.Wapigie.
 
  • Thanks
Reactions: SDG
kama un
Tatizo lako hujaeleweka nadhani unamaanisha tofauti iliyopo kati ya:

1.Company Limited

2.Sole Proprietorship

3.Corporation

4.Cooperation

Mimi bado sijajua vizuri kama Compay Limited ndo pia inaandikwa Limited Liability Company nadhani wanaofahamu watu watatusaidia,

Pia kuna kampuni zinatumia eg Mkaruka Pvt Limited, kama ingetokea mtu akatusaidia ingekaa poa sana

Mkuu mbona swali langu linaeleweka sana tu. Mimi nauliza tofauti (faida na hasara) ya kufanya biashara kama kampuni na kama partnership, hayo mengine mimi hata sihitaji kuyajua.
 
Pole sana.Hata mie nilikwama lakini angalia upande wa kulia wa hiyo website na majina na nanmba za simu.Nilipiga na kumpata mmojawapo na akanielekeza vizuri.Wapigie.
Asante mkuu, nilisita kuwapigia hao kwanza, nilitaka nipate uzoefu (first hand experience) kutoka kwa wenye partnership ama company. Lakini naona kuna umuhimu wa kuwapigia.
 
kama un

Mkuu mbona swali langu linaeleweka sana tu. Mimi nauliza tofauti (faida na hasara) ya kufanya biashara kama kampuni na kama partnership, hayo mengine mimi hata sihitaji kuyajua.
Kwahiyo Partnership haiwezi kuwa kampuni ? Ubishi mwingine wa kuzaliwa nao
 
Haya mambo naona yapo kisheria zaidi, unaposajili kampuni kwa haraka unakuwa na entity na faida za kuwa na entity ni kwamba liability inakuwa limited(kwa kifupi madeni ya kampuni ni ya kampuni na hayahusiani na mali binafsi za wanahisa), wakati mkiwa kwenye partnership mali binafsi za partners zinaweza kutaifishwa kufidia madeni ya partnership.

Faida nyingine ni kwamba kampuni itaendelea kuwepo hata ambapo shareholder atakapofariki lakini nadhani kwa partnership inakuwa dissolved.
 
Asante mkuu kwa elimu. Vipi lakini kuhusiana na mambo ya gharama za kuendesha kampuni na partnership? Vitu kama Kodi?
 
Partinership ni rahisi kama uko fast maana haihitaji memorandum halafu ni flexible...japo hiyo hiyo Partinership mkishakua fresh mnaigeuza company
 
Back
Top Bottom