BRELA badilikeni

Oppomall

JF-Expert Member
Feb 8, 2017
3,496
3,595
Poleni na Majukumu ya ujenzi wa Taifa wakuu. Nianze kutoa masikitiko yangu kwa hawa jamaa wanaojiita brela.
Hawa jamaa wanajiona Miungu watu.

Hawana Customer care, wanadharau kama si kuwapuuza wateja ilihali hawajui kuwa watoto wao wanakwenda msalani kupitia kodi za hao Wananchi.

Serikali ilianzisha mfumo wa usajili wa makampuni, majina ya biashara, alama za biashara nk kwa njia za mtandao kwa nia nzuri kabisa. Ulikua ni mfumo wa kupunguza urasimu na kuharakisha maendeleo ya nvhi yetu.

Cha ajabu yanayofanyika leo na Brela, wanarudisha maombi ya watu hovyo hovyo bila maelekezo ya kutosha.
Hivi mnadhani kila mtu anaesajili kampuni/biashara yake anafahamu mnachokifahamu ama anashughulika na jambo hilo hilo kila siku?

Mkipigiwa simu kutoa maelekezo mnatoa majibu ya hovyo, kwa mkato na kukata simu za wateja bila kujali kwamba mmepigiwa ili mlete utatuzi wala si kuleta nyodo kwa wanaolipeni.

Pili mteja anaamua awafuate Ofisini mnazuia mteja asiingie kwenu eti nenda kamalizane na mtandao??
Mko serious kweli?

Hebu oneni aibu na mbadilike, mpo Ofisini kutatua, kusaidia, kuelimisha na kuondoa changamoto za walaji wenu na si mahali pa kwenda kusaini na kuondoka.

Jioneni wenye hatia unaingia Ofisini na kutoka hakuna mteja alieridhika na huduma yako.
Nawasilisha.
@brela
 
Ni mwendelezo wa roho mbaya za baadhi ya Watanzania waliopewa nafasi fulani kuhudumia jamii. Watu hawajali wenzao kabisa.
Saa nyingine mtu kaamua afungue biashara/ kampuni yake kutokana na kukosa ajira Ila unakuta anakwamishwa na mijitu iliyokosa utu. Hii ipo kwa Brella,TRA, Halmashauri na baadhi ya taasisi za Serikali.
Hebu waoneeni huruma wenzenu wanaoamua kujiajiri. Pia wanavyofungua kampuni/ biashara wanatengeneza ajira kwa vijana mtaani.
I will miss JPM.
 
Nchi hii ingekuwa na kitengo cha Usalama wa Taifa kinachofanya "intelijensia" ya uchumi, hao wahuni wa Brela wala wasingekuwepo ofisini kufanya hujuma kwa taifa! Ucheleweshaji na ukiritimba wanaofanya watumishi wa Brela ni "UHUJUMU WA UCHUMI" Maana wanaikosesha Serikali mapato halali ya kodi kutoka kwa wafanyabishara! USALAMA WA TAIFA tusaidieni. Brela wanahujumu uchumi kwa maksudi!
 
Nchi hii ingekuwa na kitengo cha Usalama wa Taifa kinachofanya "intelijensia" ya uchumi, hao wahuni wa Brela wala wasingekuwepo ofisini kufanya hujuma kwa taifa! Ucheleweshaji na ukiritimba wanaofanya watumishi wa Brela ni "UHUJUMU WA UCHUMI" Maana wanaikosesha Serikali mapato halali ya kodi kutoka kwa wafanyabishara! USALAMA WA TAIFA tusaidieni. Brela wanahujumu uchumi kwa maksudi!
Nawazaga sana kuhusu hiki kitengo, unakuta kuna mtu anakwamisha mambo au uhujumu unaendelea somewhere, mpaka watu wabebe mabango,
 
Hao jamaa ni wa hovyo sana, washawahi kunisumbua zaidi ya wiki kila nikifanya marekebisho yanarudi yale yale. Ofisi za Kanda ya ziwa yule jamaa anaitwa AG ndio hovyo kabisa kafanya ile ofisi yake binafsi anaingia na kutoka muda atakao, ukipiga simu hapokei akiona usumbufu anazima kabisa.
 
Back
Top Bottom