Breathtaking Kinetic Typography Video

1. Wewe unajifunza wakati wenzio tunatafuta kazi!!!?? angalia usizeekee kwenye kujifunza.
2. Kuwa trendy. Typography za kisasa zinahusiha still graphics na timelapses
3. Hongera for making it from scratch
 
1. Wewe unajifunza wakati wenzio tunatafuta kazi!!!?? angalia usizeekee kwenye kujifunza.
2. Kuwa trendy. Typography za kisasa zinahusiha still graphics na timelapses
3. Hongera for making it from scratch

mkuu kumbuka hii ni forum ambayo imekusanya watu wa kada mbalimbali,hivyo sioni kama ni jambo jema ninyanyue mabega juu ili tu nionekane nimefuzu au napata sana kazi.mda mwingine ni bora kuacha jamii iku-judge yenyewe kwa kile kidogo unachofanya.allah alhamdulillah sifi njaa lakini pia siishi kwa kutegemea kinetic typography.thanks for your advice though.
karibu sana.

samahani kidogo,naomba unifundishe japo kwa maneno machache kuhusu hiyo time-lapse.ni nini hiyo mkuu?.

CC Lukansola
 


Kwanza nikupongeze kwa kujitahidi kutoa jibu la kiungwana kwa huyu @John Ezekiel.

Jamaa anafurahisha sana, yani kawa hiyo kama yeye anatafuta kazi sisi tusijifunze! kwani yeye hakujifunza?... ajabu sana, au kwake elimu ina mwisho kama Profesa Muhongo aliyesoma mpaka mwisho, wazungu wangekuwa na mawazo kama yako @John Ezekiel leo tusingekuwa na smartphones tungeishia kwenye Phillips Savvy hahaha...






Unanikumbusha jamaa mmoja wakati natamani kufanya graphics aliniambia haitanisaidia eti kwa kuwa siku hizi kuna software zinafanya design hivyo watu wanafanya kazi zao wenyewe, wakati huo ilikuwa 2002, nashukuru Mungu nilimpuuza huyu jamaa, maana leo nisingekuwa hapa nilipo japo sijaridhika lakini alhamdulillah na sasa najifunza motion graphics, sijifunzi kupata kazi najifunza kujua, unanukimbusha pia wale wahitimu wanakujaga hapa kusema nimemaliza chuo natafuta kazi badala ya kutengeza kazi. THINK
 

ndiyo mambo ya mitandaoni mkuu.mda mwingine inabidi uuvae ustaarabu unapo jibu post za watu kama hawa.

ulicho zungumza hapo juu ni sahihi kabisa.kwanza kabisa,ktk creative industry siyo lazima uzunguke na vyeti mtaani kutafuta kazi.kile unacho kifanya,ambacho wadau wanakiona na kuvutiwa nacho ni product/qualification kubwa ya kukuuza sokoni.huna haja ya kukimbizana huku na kule kutafuta kazi,deal zenyewe zina-flow ktk simu yako.unachotakiwa kufanya ni kutengeneza tu mtandao mzuri wa customers.

uzoefu wangu unaniambia,mara nyingi watu wenye statement za kujisifu kama huyo mdau hapo juu,ni amateurs wasio na CV ya project yoyote kubwa walizo wahi fanya ktk field yetu hii.

nimekaa mda wote nasubiri aje atufundishe/kutoa maelezo mafupi/marefu kuhusu "time-lapse".maana ni kitu kigeni kwangu/kwetu,sijawahi kukisikia.
 


Asante sana, na mimi nasubiri atuambie hiyo time lapse ni nini, napenda kujifunza
 
nimekaa hama mda wote nasubiri aje atufundishe/kutoa maelezo mafupi/marefu kuhusu "time-lapse".maana ni kitu kigeni kwangu/kwetu,sijawahi kukisikia.

Baada ya kuona harudi nime consult dictionary yangu:

[h=1]time-lapse[/h]
Also found in: Encyclopedia, Wikipedia.[h=2]time-lapse[/h] (tīm′lăps&#8242😉adj.Of, using, or being a technique that photographs a naturally slow process, such as plant growth, on movie film at intervals,so that continuous projection of the frames gives an accelerated view of the process.

Sioni uhusiano wa hii kitu na mada yako...








 
timelapse mi nafanya sana kwenye simu yangu ni kitu kinachofanywa na camera au video editor kuifanya video ndefu sana (pengine hata siku hadi miaka) kuja kivideo kifupi. mfano unatega camera feri kwa siku nzima then ile video unaifanyia time lapse halafu inakuwa maybe dakika tatu. cheki hii timelapse ya nokia 808

https://www.youtube.com/watch?v=5YdhR8Px_dY

na kuhusu huyo jamaa anaesema yeye anatafuta kazi tayari inaonesha sio creative designer, huwa watu wa field hii wanajiajiri sababu ukiajiriwa unapokonywa uhuru wako na field hii haina mwisho na mtu anaetumia kalamu na karatasi anaweza mshinda mwenye masoftware zaidi ya 100 na pc yenye nguvu kushinda zote duniani. inahitaji talent zaidi kuliko vyeti.
 

luka hapo kwenye red ndio hasa nilikuwa nimetegea aje aeleze,halafu atuambie how time-lapse relates with kinetic typography?.ndio maana nika mshauri,ktk hizi social media ni bora ku-keep low profile kuliko kujifanya mjuaji mwingi.kuna madhara yake.ila asiogope,aje tu aongeze nyama kuhusu hiyo kitu kwa faida ya wale "wanaojifunza kama mimi".
 

Chief habari za masiku mkuu,
nimefurahi kuona comment yako hapa.kuhusu time lapse,kama ulivyo sema,ni muunganiko wa picha mnato zilizochukuliwa ktk location moja na kupangwa ktk sequence ili kuleta ile smooth transition ktk video.haina mambo mengi,unachotakiwa kufanya ni kutega tu camera yako na kui-automate ichukuue picha mfululizo ktk eneo ambalo subject zina-move toka point A-B au toka chini kwenda juu and vise versa.yaweza kuwa jua,mwezi,watu,wanyama,mimea,magari,nk.


technically,hakuna uhusiano wa moja kwa moja wa time lapse na kinetic typography,kwanini?kwasababu time lapse inahusisha zaidi picha wakati kinetic typography inahusisha zaidi animated fonts/words being synchronized with audio.isipokuwa tu unaweza ukachukua ki-clip cha time lapse na kuki-insert ktk KT video.pia unaweza chukua image ukai-sync sambamba na audio ktk KT.sina hakika sana na maelezo yangu,kama yupo anaeweza kuongeza nyama anakaribishwa.

niliwahi kufanya moja siku za nyuma,ipo siku nitaiweka hapa JF.
asante.
 

Mkuu, naona ww na mwenzako mmekuwa offended. pengine chakula nilichotema ni kigumu kumeza, nahisi ni kwasababu ya levels, mie nimezungumza kwa mentality ya level yangu, na nyie wanetu imewalemea. Anyway, kuhusu usemi wa kwamba "angalia usizeeke kwenye kujifunza" maana yangu ilikuwa hii field haina mwisho wa kujifunza, hivyo kanuni ni kupiga kazi huku unajifunza kwasababu kila siku teknolojia zinavumbuliwa kuacclerate hii shughuli yetu. Mfano, InDesign ndio ilikuwa unbeatable upande wa layout designing, lakini hivi karibuni zimeibuka flagship matata kuliko hii product ya Adobe.

Kuhusu aliyesema mimi ni ameteur, nadhani kila siku kazi zangu mnaziona EATV na K24 ya Kenya, hivyo muelewe mimi ni kaka yenu tu. Na nilipozungumzia "kutafuta kazi" nilimaanisha those corporate positions, sio freelace gigs ambazo hukati hulipi hata VAT tra. Najua wengi wenu ni self-taught hasa kupitia Youtube, Google na Torrents..tabia za self learners ni kuresist formality, hasa wanapokosolewa...so guys watch out. Mbali ya mm pia kuvitumia vyanzo hivyo kwa wingi mimi ni college graduate from a reputable instute of outside Tanzania.


jambo la mwisho na ushauri wangu kwenu wote wenye nia na hii field ya Interactive Multimeda & Design (Animation, Graphic, Web, Video etc) ni kwamba: We are learning a knowledge ahead of our time. Utandawazi umesaidia kujua kinachoendelea kwa wenzetu lakini sio kila kitu tunaweza himili. Ukijifunza Autodesk Maya au Nuke leo, Tanzania hii hutathaminiwa, kwasababu bado hatujafikia pace ya kuiaccomodate Autodesk Maya...coz faida ya huyu guy(this software) nikuproduce hollywood-like projects, ila kama unamtumia kuproduce 5 mins long projects, why not learn Cinema 4D? why not invest that time in learning After Effects? Kwahiyo mnapoendelea kujifunza msipeperushwe na upepo wa magharibi, the nature rule you...uchumi wetu bado sana ili kuinvest kwenye studio kwaajili ya kuproduce Sci-Fi movies, ass kicking projects n.k. What's my point? IT'S NOT ABOUT SKILLS...IT'S ABOUT HARDWARE AND FINANCES. Sijui kama mmenipata wazee.
 

nina hamu nione hizo project zako unaweza kuzitaja? maana sizifahamu.

its about skills kaka na sio mtaji, ukiwa na hela unaweza kuwa na maelfu ya software na computer unaweza jifunza setting zote ila huwezi kujifunza kipaji, kipaji unazaliwa nacho. nitakupa mfano wa mwanadada kseniya simanova yeye anakaa na meza na mchanga then anawapigia watu story kupitia mchanga. ameshinda tuzo za talents, projects kibao kubwa anafanya yeye hatafuti kazi na anatumia mchanga tu. mamilioni wanaangalia video zake youtube nenda ka upload wewe video zako youtube kama utapata viewers wengi.

cheki video yake
https://www.youtube.com/watch?v=BIVTBL5r1Hg&spfreload=10&hd=1

kuna watu wanachora kwenye paint vizuri kushinda hata wanaotumia photoshop, kuna wanaotengeneza motion graphics nzuri kwa powerpoint kushinda anaetumia after effects, kwanini wanaweza? ni talent kaka hata ujifunze setting vp kama hauna talent ukikutana na mwenye talent lazima utatulia.
 
Mkuu, naona ww na mwenzako mmekuwa offended. pengine chakula nilichotema ni kigumu kumeza, nahisi ni kwasababu ya levels, mie nimezungumza kwa mentality ya level yangu, na nyie wanetu imewalemea.
ni bahati mbaya sana sikupenda "siasa za majigambo" ziingie ktk topic hii,hususani kwa jukwaa makini la Tech, Gadgets & Science.lakini kwakuwa thread unaipeleka huko,i will try to dance with your tune.

point.sina cha kuongeza

Kuhusu aliyesema mimi ni ameteur, nadhani kila siku kazi zangu mnaziona EATV na K24 ya Kenya, hivyo muelewe mimi ni kaka yenu tu
.

uzuri ni kwamba mimi ni mtazamaji mzuri wa EATV,na nimebahatika kuwa na urafiki wa karibu na baadhi ya staff wa pale hasa ma-cameraman,editors na watu wa transmission.nilibahatika kusoma nao college moja.la kusikitisha tu ni kwamba hatukupata bahati ya kusoma kwenye "reputable institute outside Tanzania".baadhi yao wapo hapa JF,nimewaalika tu kiroho safi waje wachangie japo mawili matatu.itakuwa bora ukituwekea moja ya motiongraphics video ulizo wahi fanya EATV.hakuna shaka huwezi kosa data hata kama sera za kampuni haziruhusu (mtizamo wangu tu).


Na nilipozungumzia "kutafuta kazi" nilimaanisha those corporate positions, sio freelace gigs ambazo hukati hulipi hata VAT tra.
nina idea kidogo na marketing japo sikusomea,ninavyo fahamu ni kwamba big budget cooperate project zinaenda kwa kampuni ambazo ni registered and well established.isipokuwa tu a freelancer can be hired as an expert kwa hiyo kampuni ambayo imepewa kazi na corporate company.tunarudi pale pale,freelancer ktk creative industry bado ana nafasi kubwa ya kuwa hired kutokana na efficiency yake ktk kazi.hana haja ya kugonga milango ya ofisi za watu kutafuta kazi.anachoweza fanya ni kujitangaza tu kupitia vyanzo mbalimbali.mfano social media,blogs,website,forums, etc.

jambo lingine ni kwamba,kama umefata taratibu zote za kusajili kampuni brela na ina TIN number,ili tu u-target project za mashirika,kwanini tena wewe mtu wa production uingie mtaani kutafuta kazi?.kwanini usiajili mtu wa marketing akufanyie kazi ya kukutafutia soko.au ni kampuni ya mfukoni!!?,kila idara una cover mwenyewe!!?.just curious you know.:madgrin:


Najua wengi wenu ni self-taught hasa kupitia Youtube, Google na Torrents..tabia za self learners ni kuresist formality
laiti kama ungejua most of online tutors ambao hata wewe huwasoma ni self taught,usinge dharau swala la watu kutafuta maarifa mtandaoni.
nikupe mfano,leo hii mmiliki wa video copilot endrew kramer anaheshimika duniani kwa uwezo wake wa kuifundisha AE na kuunda motion graphics plug-ins mbalimbali.je unajua kwamba jamaa alijifunza AE yeye mwenyewe tangu angali kijana?.msome HAPA.

mimi ni college graduate from a reputable instute of outside Tanzania.
duh!!.hongera sana mkuu.

point nzuri.sina tatizo nayo.
 
Mkuu Adobe After Effects, ni kama ulikuwa mawazoni mwangu, umefafanua vizuri sana... kwa namna ya kujieleza aliyonayo huyu bwana nina shaka kama hata huko 'ulaya' alisoma kweli, nimesoma moja ya post zake za zamani alileta post yake kuhusu video yake akidai yeye ndo ya wa kwanza kuitengeneza na kuisifia yeye mwenyewe.

Mawasilaoni ni moja ya nyenzo muhimu kabisa katika biashara, au maisha kwa ujumla, sasa wewe umesoma mass communication lakini hujui useme nini wapi.

Huu uzi mimi binafsi umenisaidia sana tayari pamoja na kuwa hauna muda mrefu sana, kwa hiyo ningependa utumiwe na wale tu wanaopenda kujifunza, kama wewe unaona unajua tayari huna sababu ya kushiriki uzi huu, hata mwanzo mleta mada amesema kabisa kuwa lengo ni kupeana ujuzi.
 
Last edited by a moderator:

mkuu tutafika tu taratibu kadili mood ya thread itakavyo enda.wehenga wa kiswahili husema ''njia ya muongo ni fupi",na wale wakizungu nao wakaja na msemo wao unasema "one ought to have a good memory when he has told a lie".nasisitiza tena "tutafika tu",tuvute subira.

well,
hukusu maudhui ya uzi huu,lengo hasa ni kushirikishana technicalities za maswala ya motion graphics/animation.na sio kuonyeshana ujuaji/mbwembwe kama mdau mmoja anavyotaka iwe,ndio mana pale juu nimetoa angalizo la kukaribisha maswali,maoni na ushauri toka kwa wadau mbalimbali.

ni utamaduni wangu kufanya hivyo,sio kwa thread hii tu,hata HII nimetoa angalizo kwamba mimi siyo "alfa and omega" wa adobe AE hapa JF kiasi cha kila mtu aamini kila post yangu,yeyote yule anaweza nisahihisha/kuongeza maelezo pale ambapo nimefafanua ndivyo sivyo.

asante sana mkuu.
 

Sitaki kuongea sana maana nilshaongea na kukuasa mawili matatu. Mkuu, wewe bado upo kwenye level "proving yourself", ndio maana unasisitiza kuona kazi ama kuwa na viewers nk. Mi nimeshavuka hapo, nafanya kazi na corporate clients kama hao wachache niliokuorodheshea, huku hakuna kuweka kazi ya mteja Youtube na ujinadi ati hii ni yangu, tunafanya kazi kwa copy rights na kibali cha mteja pale unapolazimika kutumia kazi ulizomfanyia kama portfolio ukiwa unatafuta kazi kwa mteja mwingine, and you're not the client, why should i upload my works for you???

P.S. Niliposema "HARDWARE & FINANCES/CAPITAL" are what matters nilimaanisha "SKILLS" everybody can afford it. Okay??
 

Sitaki kuongea sana maana nilshaongea na kukuasa mawili matatu. Mkuu, wewe bado upo kwenye level "proving yourself", ndio maana unasisitiza kuona kazi ama kuwa na viewers nk. Mi nimeshavuka hapo, nafanya kazi na corporate clients kama hao wachache niliokuorodheshea, (im an employee in kenya but i freelance too, I meet clients wakubwa kwasababu nipo kwny kampuni kubwa ya media hapa kenya, tunaweza ilinganisha na IPP hapo bongo) huku hakuna kuweka kazi ya mteja Youtube na ujinadi ati hii ni yangu, tunafanya kazi kwa copy rights na kibali cha mteja pale unapolazimika kutumia kazi ulizomfanyia kama portfolio ukiwa unatafuta kazi kwa mteja mwingine, and you're not the client, why should i upload my works for you??? Kuhusu kujuana na watu wa EATV, mimi sidili na cameramens or editors. Kwenye mastesheni kama hayo nadili na Head Of Programmes then Accountant.

P.S. mimi ni mteja mzuri wa Andrew kramer. Departmennt yangu imenunua Plugins/Packs zake zote. Wewe si unadownload za crack???!!! ungekuwa unampenda/kumfatilia na kuthamini mchango wake ungenunua au hata kumtumia donation/thank you letter
 

wapi umeona kazi yangu? profession yangu hata haihusiani na computer kabisa. ila nafahamu computer na design usipoonyesha kazi yako tutajuaje kuwa wewe ndio unaclaim unayosema?

je mimi nikifungua id nikaclaim naitwa kanye west na kim kardashian ndio mke wangu utaamini hivi hivi? hili ni jukwaa la tech ambalo tulitegemea kila kitu kiwe wazi. anyway kama unataka kutambiana na hutaki kuonyesha hicho unachotambia then kwaheri.
 


Kwa kifupi unaongea pumba tupu, hukawii kutuambia hata Andrew Cramer mnafahamiana, wewe ni wa kupuuza tu. huna msaada hapa zaidi ya majigambo tu.
 

bila shaka, huwezi kuongea sana sababu unajua ni uongo,utudanganya tu hapa.the truth is you are not on a class you claim to be.it appears that your words are an illusion of what you wanted to be in your life(from my psychological perspectives),ulikuwa na expections kubwa ktk fani uliyo ipenda,ni bahati mbaya sana haikuwa kama ulivyotaka iwe kwako.matokeo yake umekuwa depressed na ndoto zako zilizo feli kiasi cha kuamua kudanganya watu kwa kujikweza kwamba wewe ni hivi wewe ni vile, kumbe sio kweli.nina uzoefu na watu wa aina yako.tafakari sana maneno yangu mdogo wangu.au kama hutojali ni PM,kuna jambo la kikazi naweza nikakushirikisha.jishushe tu usione haya.

BWT hivi unajua ni majukumu gani yapo chini ya head of programs wa TV station?.hivi unajua section ya maswala ya graphics design ipo chini ya department gani pale EATV?.hivi unajua graphics designer wa tv station hushirikiana na watu wa kitengo gani ili kukamilisha majukumu yake vizuri?.unamfahamu chief graphics designer wa EATV anaitwa nani?.

ni kwa namna gani accountant wa TV station anakuwa affiliated na HOP(head of programs)?.hiyo ni management ya nchi gani ktk biashara ya TV station?.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…