Breaking news.....serikali ludewa yasababisha shule kuanguka | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Breaking news.....serikali ludewa yasababisha shule kuanguka

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by Saint Ivuga, Jul 12, 2011.

 1. Saint Ivuga

  Saint Ivuga JF-Expert Member

  #1
  Jul 12, 2011
  Joined: Aug 21, 2008
  Messages: 39,471
  Likes Received: 19,862
  Trophy Points: 280
  [h=3]BREAKING NEWS.....SERIKALI LUDEWA YASABABISHA SHULE KUANGUKA[/h]
  [​IMG]

  SHULE mpya ya msingi katika kitongoji cha Mbugani kata ya Mavanga wilaya ya Ludewa mkoani Iringa iliyojengwa kwa nguvu za wananchi imebomoka baada ya serikali kushindwa kupeleka bati za kuezeka shule hiyo kwa wakati.
  Uongozi wa shule hiyo umesema kuwa kuanguka kwa kuta zote za shule hiyo kumetokana na serikali ya Halmashauri ya wilaya Ludewa kuchelewa kuunga mkono jitihada za wananchi wa kijiji cha Mavanga ambao walilazimika kujitolea kujenga shule hiyo ili kuepusha msongamano wa wanafunzi katika shule moja iliyopo kijijini hapo.
  Akizungumza kwa niaba ya mkuu wa shule hiyo kaimu mkuu wa shule hiyo Alemaatema Ngalalikwa alisema kuwa hivi sasa shule hiyo imeshindwa kuanza kutokana na jingo moja lenye vyumba viwili vya madarasa kubomoka kwa kukosa bati na saruji na kupelekea shule hiyo kuendelea kusimama bila kupokea wanafunzi.
  Hata hivyo alisema kuwa wazo la kujenga mkondo huo mpya wa shule ya Mbugani kulitokana na kikao kilichoketi mwaka 2008 kutathimini tatizo la utoro wa wanafunzi na msongamano wa wanafunzi hao madarasani na kuazimia kujenga majengo hayo.
  Alisema kuwa ujenzi huo ulianza toka mwaka 2009 baada ya wananchi kujitolea kufyatua tofali na kusongeza mawe na kuwa mwaka huo huo ujenzi ulikamilika na jumla ya shilingi zaidi ya milioni 5 ndizo zilitumika kujenga majengo hayo ambayo baadhi tayari yamebomoka .
  Mbali ya kubomoka kwa majengo hayo pia alisema hata vyumba viwili vya madarasa vilivyosalia katika eneo hilo vipo hatarini kubomoka kutokana na kutosakafiwa kwa saruji na kuwa iwapo serikali itachelewa kusaidia kutoa fedha za kukamilisha ujenzi huo upo uwezekano wa nguvu za wananchi na fedha hizo zaidi ya milioni 5 zilizotumika katika ujenzi huo kupotea.
  Pia alisema tatizo la madawati ni kubwa katika shule hiyo mpya ambayo ilitarajiwa kuombewa kibali kwa ajili ya kupunguza wanafunzi kutoka mkondo mama na kuanzishwa kwa shule hiyo na kuwa hadi sasa hakuna dawati hata moja katika vyumba hivyo vya madarasa.
  Maria Ngatunga ni afisa mtendaji kata ya Mavanga ambaye alithibitisha kuwepo kwa tatizo la kubomoka kwa madarasa hayo kutokana nna kukosa mchango wa serikali katika kukamilisha ujenzi huo na kuwa kwa sasa tayari Halmashauri iimeazimia kuchangia fedha za kukamilisha ujenzi huo baada ya kutokea kwa maafa hayo ya majengo kubomoka.
  Kwa upande wake mbunge wa jimbo la Ludewa Deo Filikunjombe wa kwanza kushoto pichani akitembelea shule hiyo kabla ya kuwahutubia wananchi wa kijiji cha mavanga mbali ya kuwapongeza kwa ujenzi wa shule hiyo mpya ambayo kwa sasa majengo yake yameanza kubomoka bado aliahidi kujitolea kuchangia bati 104 ili kuenzeka majengo hayo mara yatakapojengwa upya pamoja na kjmwomba ofisa elimu kuchangia saruji.

  source :fransic godwin blogspot
   
 2. Yericko Nyerere

  Yericko Nyerere Verified User

  #2
  Jul 12, 2011
  Joined: Dec 22, 2010
  Messages: 16,246
  Likes Received: 3,836
  Trophy Points: 280
  Hiyo silikali ya sisiemu!
   
 3. Chimunguru

  Chimunguru JF-Expert Member

  #3
  Jul 12, 2011
  Joined: May 3, 2009
  Messages: 9,843
  Likes Received: 270
  Trophy Points: 180
  wamejaa wezi tu huko serikalini
   
 4. K

  Kifulambute JF-Expert Member

  #4
  Jul 12, 2011
  Joined: May 8, 2011
  Messages: 2,509
  Likes Received: 19
  Trophy Points: 135
  Wanadai posho tu kila siku, ingekuwa ni posho ingeungwa mkono siku hiyo hiyo lakini kwa vile ni mabati ya kujengea shule ya kata tena ambayo mtoto wa mbunge haendi kusoma bora ianguke ila yeye apate posho. naamini hiyo shule mabati yote yasinge chukua hata 10M ambayo mbunge wake anaipata kwa mwezi mmoja.

  wananikera na sera yao eti...tumethubutu, tumeweza na tunaendelea......kweli wanjaendelea kuiba na watatuiba hadi wananchi
   
Loading...