breaking news: mwanza | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

breaking news: mwanza

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by Ze burner, Oct 18, 2011.

 1. Ze burner

  Ze burner JF-Expert Member

  #1
  Oct 18, 2011
  Joined: Jan 5, 2011
  Messages: 460
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 33
  hapa ninapoandia habari hii machozi na kamasi nyembamba zinatiririka kutokana na mabomu ya machozi. ni majira ya saa kama kumi na mbili hivi wakati narejea kutoka mizungukoni nakuta watu wengi wakitembea njiani. nilidhani ni hali ya kawaida ya tabu ya usafiri ambayo imeibuka katika hizi siku za karibuni. wakati naelekea katika mitaa tunayoishi jamaa wakanisimamisha na kunieleza kuwa nisende na gari upande ule hivyo nilibadili njia na kupita njia nyengine.
  Baadae niliwauliza wadau ambao walikuwepo barabarani wakiteta kulikoni? walinieleza kwamba leo kuna vijana katika mitaa ya hapa Mwanza kuanzia mitaa ya Voil, shede, mitatu, chakechake, shule, mswahili na mkuyuni wameamua kufanya uharifu kwa gari yoyote ya abiria "daladala" ina yopita katika njia hiyo kutokana na kuchoshwa na vitendo vya magari hayo kuuwa ndugu na watoto wao katika maeneo hayo.
  Habari za kina zinasema kwamba ni kama mwezi mmoja tu mtoto ameuawa na juzi ameuawa mwengine.

  Hapa nadhani serikali ilishapata taarifa juu ya heka heka hizi kwa sababu ni jana tu wakati napita eneo la mswahili hapa mwanza nilikuta wanachora zebra nikashangaa sana maana hata hiyo zebra yenyewe imechorwa katika corner kali. na leo hii ndo yametokea hayo.

  hali bado si suari mana mara baada ya kufika home na kutoka kidogo kutafuta vyocha. zilipigwa risasi sijui ndo za aina gani nadhani ni baruti tu niliona kama imepita upande mmoja wa sikio langu na kutokea upande wa pili huku nikiona cheche na moshi mkali. Nilipoamua niondoke bado walikuwa wanaendelea kupiga mabomu hayo mara nikahisi macho yanawasha. watu wanakimbia milimani na mimi nikaunga tela sijui niendako tukapata maji ikawa nafuu kidogo.

  bado watu hawajalalal wanasikilizia mshindo hivyo na askari patrol mabomu kama iraki kama una jamaa yako dereva wa daladala muulize zaidi asije akawemo katika waathiriika wa makasa huo.

  nawatakia jioni njema.
   
 2. DASA

  DASA JF-Expert Member

  #2
  Oct 18, 2011
  Joined: Jan 6, 2011
  Messages: 1,031
  Likes Received: 11
  Trophy Points: 135
  Poleni sana mwanza. shukurani kwa taarifa mjomba.
   
 3. M

  Mafuluto JF-Expert Member

  #3
  Oct 18, 2011
  Joined: Aug 25, 2009
  Messages: 1,602
  Likes Received: 234
  Trophy Points: 160
  ....Nji hii bana, yaani ni balaa tu. Viongozi wakuu badala ya kushughulikia matatizo ya msingi wapo wanazunguka kila mahala kuuza inji kwa visingizio vya uwekezaji. Ona upupu anaoongea huyu anayejiita ntoto wa nkulima.....!! Ipo siku zitapigwa na hawa ole wao tutawatafuta hata wakimbilie sijui brasil au iowa !!!
   
 4. ram

  ram JF-Expert Member

  #4
  Oct 19, 2011
  Joined: Oct 5, 2007
  Messages: 6,225
  Likes Received: 920
  Trophy Points: 280
  Asante kwa taarifa na poleni pia
   
 5. Jeji

  Jeji JF-Expert Member

  #5
  Oct 19, 2011
  Joined: Jun 28, 2011
  Messages: 1,981
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 135
  duh!! poleni wana Mwanza.
   
 6. Mzee wa Rula

  Mzee wa Rula JF-Expert Member

  #6
  Oct 19, 2011
  Joined: Oct 6, 2010
  Messages: 8,177
  Likes Received: 89
  Trophy Points: 145
  Hao wananchi wamekosa busara kidogo, kufanya vurugu siyo njia muafaka sana ya kushinikiza kuwekewa matuta. Purukushani zote hizo mwisho wake ni kuwekewa matuta jambo ambalo linawezekana.
   
 7. prakatatumba

  prakatatumba JF-Expert Member

  #7
  Oct 19, 2011
  Joined: Oct 17, 2011
  Messages: 1,337
  Likes Received: 11
  Trophy Points: 135
  Abaha abaha
   
 8. M

  Mkwe21 JF-Expert Member

  #8
  Oct 19, 2011
  Joined: Apr 11, 2011
  Messages: 1,857
  Likes Received: 499
  Trophy Points: 180
  Poor Planning of Our Towns will always cause Problems!! Na Hii Haitakwisha Hata Tuweke Matuta Hadi Milangoni mwa Nyumba Zetu!! Anyway ndio Tunayojivunia kwa Miaka yetu 50 Ya Uhuru!!
  Pendekezo!!
  Tunatakiwa Kila Tunapoweka Barabara ya Lami Mahali Popote Tufikirie Pia Pedestrians Way!! Njia za Waenda Kwa Miguu!! This is What we Call sustainable Planning!! Matuta sio Suluhisho!!!
   
 9. Ze burner

  Ze burner JF-Expert Member

  #9
  Oct 19, 2011
  Joined: Jan 5, 2011
  Messages: 460
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 33
  kwa kweli serikali sijui ni nini wameshachora zebra wamemaliza na hapo zebra ilipochorwa naona kama hizo ajali zitaongezeka. nao jeshi la polisi ni kama vibaraka wanasubiri vurugu waongeze vurugu. hawana muda wa kukaa pamoja na vyombo husika kama vile jiji kuona watafanyaje kutatua matatizo hayo. nasubiri tuone
   
 10. Vinci

  Vinci JF-Expert Member

  #10
  Oct 19, 2011
  Joined: Jul 6, 2009
  Messages: 2,641
  Likes Received: 120
  Trophy Points: 160
  kuliko kuharibu hayo magari ni vyema wangeifunga hiyo barabara kuzuia magari yasipite....hii ni kuepusha vurugu na uharibifu wa mali na kusababishiana majeraha kwa wasio husika kabisa kama abiria na watembea kwa miguu.
   
 11. Nkwesa Makambo

  Nkwesa Makambo JF-Expert Member

  #11
  Oct 19, 2011
  Joined: Aug 26, 2011
  Messages: 4,765
  Likes Received: 24
  Trophy Points: 0

  Kwanini Busara iwe kwa wananchi peke yao ? Jeshi la polisi (Trafific)Busara iko wapi ? Mahakama na mahakimu na majaji Busara iko wapi ? hata wewe mwenyewe busara iko wapi kuamini kwamba ajali zitaondolewa na ujenzi wa matuta barabarani ?,Hata zebra zikicholwa haimaanishi kuwa wavunja sheria za usalama barabarani watasita kuwagonga watoto na raia wema,watawagonga kwa kuwa wanauhakika na kwamba hawawezi kufanywa kitu ambacho ni fundisho kwao au kwa madereva wengine,wataua,watajeruhi,lakini watatakiwa kujazqa fomu za bima na kuonyesha leseni,kuandaa rushwa na faini ya 50000/=. Sheria zipo,usimamizi hakuna,unataka wananchi wenye uchungu na maisha ya ndugu zao wafanye nini,Dereva akigonga mtu/mtoto hata pembeni ya barabara akamua,bado trafic wanasema ni ROAD ACCIDENT/CARELESS DRIVING,kumbuka kuna mistari imechorwa barabarani ambayo mingine ni makatazo,lakini kwa kuwa rushwa imetamalaki hamna anayewaza kuokoa maisha ya waenda kwa miguu kwa kusimamia japo sheria hizi dhaifu zilizopo.
  Kwanini isiwe kuwa dereva anayegonga mtu sehemu ya kivuko cha wenda kwa miguu ashitakiwe kwa kuua au kujeruhi kwa makusudi,au yule anayeua au kujeruhi kwa kugonga waendao kwa miguu ili hali akitanua asishtakiwe kwa kujaribu kuua au kujeruhi kwa makusudi,naamini kama sheria ya uslama barabarani ingetambua uwepo wa kadhia hizi za madereva na kuweka adhabu stahili barabara zetu zisingekuwa na matuta wala wananchi wasingepandisha hasira.
  Kwa kuwa wenye mamlaka hawataki kuwalinda wananchi ili madereva wawaheshimu ni wajibu wa wananchi husika kubuni mbinu za kuwalazimisha madereva wawaheshimu barabarani.
   
 12. marejesho

  marejesho JF-Expert Member

  #12
  Oct 19, 2011
  Joined: Jan 6, 2011
  Messages: 6,539
  Likes Received: 830
  Trophy Points: 280
  Poleni sana
   
 13. Ze burner

  Ze burner JF-Expert Member

  #13
  Oct 19, 2011
  Joined: Jan 5, 2011
  Messages: 460
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 33
  mzee maelezo matamu kama asali, sasa tupe kidogo tufanyeje kwa mawazo yako. au hiyo unayoiita busara ya raia waliyoichukua ndiyo sahihi?
   
 14. katabu

  katabu JF-Expert Member

  #14
  Oct 19, 2011
  Joined: Apr 19, 2011
  Messages: 307
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 35
  Kama ingekuwa kwetu tusinge fanya vurugu. Tungejikusanya na kuweka matuta halafu tuweke dolia ya kusubiri ni nani atakaye sogeza kichwa chake kuondoa.
   
Loading...