Sasa hivi imekuwa desturi pale getini mida ya jioni wanachuo wanashindia mahindi ya kuchoma kwa sh. 300/-
kudadadeki SAUT- mwanza! mbona wamejaa mazuzu jamani? Hata hayastuki kudai hela zao, yapoyapo tu. Aagkh!!
Jana niileta thread ya mgomo wa wanachuo wa Mkwawa, na leo hali imeendelea kuwa mbaya kwani waliahidiwa kuwa hela yao ingeingizwa jana. Mpaka sasa hawajalipwa na mgomo umeendelea. Wanachuo wamefunga mageti yote na ndipo lilipokuja gari lililokuwa linakuja kubadilisha askari wanaolinda benki ya CRDB. walipofika getini wanachuo hao wakalizuia gari na kuanza kulipiga mawe ambapo askari mmoja alijeruhiwa. Gari hilo likaondoka kwa hasira na sasa hivi yamekuja magari matatu ya FFU wakiwa tayari kwa lolote.
Nitawajuza updates, niko eneo la tukio.
........................Gari hilo likaondoka kwa hasira.....................
Hawajalipwa nini mshahara au pesa za kujikimu?