Breaking news: Chuo kikuu cha mkwawa kimenuka tena mgomo waendelea

BASHADA

JF-Expert Member
Jul 13, 2011
513
148
Wanafunzi wa Chuo kikuu kishiriki cha Mkwawa (MUCE) leo wameendelea na mgomo wao wa kushinikiza uongozi ili walipwe hela zao za kujikimu ambazo zimecheleweshwa kwa zaidi ya wiki sasa. Shughuli za masomo zimesimama na wamezingira ofisi ya Mkuu wa chuo.

My take: Je kuna uhusiano wowote kati ya huu mgomo na kashfa zilizokuwa zikiwaandama viongozi waandamizi wa chuo? Ni hisia zangu tuu, huku kukiwa na tetesi kutoka vyanzo vyenye uhakika kuwa serikali inafanya reshuffling ya vingozi, na hivyo tutegemee viongozi waliopo kupigwa chini na wengine wapya kuletwa.
Karibuni kwa mjadala
 
Vipi CDM hawajahusishwa tena?maana kila kitu utasikia cdm ndiyo wamechochea.
 
Nasikia mkuu wa chuo baada ya kuanikwa Bungeni kaamua kuyaweka mafichoni magar yake sasa anatembelea HIACE.
Tz ni zaidi ya uijuavyo.
Imagine MUSHI + KIMEI/CRDB jibu utajaza mwenyewe watu wanapiga ela kwenye Fixed Account uku vijana wanaumia.
Pesa ya laana haita kaa unufaike nayo ukiachia ngazi tuu nayo inapukutika
 
kudadadeki SAUT- mwanza! mbona wamejaa mazuzu jamani? Hata hayastuki kudai hela zao, yapoyapo tu. Aagkh!!
 
Mkuu, sasa hivi amekuwa mpole sana maana anajua hana lake, hivi sijui kama anajua kuwa ameshapigwa chini na anasubiri kupewa barua ya kuachia ofisi. Wanafunzi wamechoka mbaya ukiwaona utawahurumia, akina dada mpaka wanatia huruma kila kona wanalalamika njaa, wengine wameamua kushindia mjini kwa wafanyabiashara,
Inauma sana, wenye dada zao huku wahurumieni,
 
Sasa hivi imekuwa desturi pale getini mida ya jioni wanachuo wanashindia mahindi ya kuchoma kwa sh. 300/-
 
Sasa hivi imekuwa desturi pale getini mida ya jioni wanachuo wanashindia mahindi ya kuchoma kwa sh. 300/-

pole zao hasa hao dada zetu...Hivi pale makanyagio kwa Chuwa na Nelkon hakuna tena wali wa mia mia? Zamani kidogo pale mtu ulikuwa unapimiwa kadiri ya kiasi ulichonacho......yaani mpaka wali wa shs 10 ulikuwa unapata!!!!hapa naongelea miaka ya 2000 sio zamani sana kihivyo! Pia kulikuwa na mabans ya shs 10 tu,makubwa ukila mawili unalala...sijuhi km bado wana hiyo opportunity!
 
kudadadeki SAUT- mwanza! mbona wamejaa mazuzu jamani? Hata hayastuki kudai hela zao, yapoyapo tu. Aagkh!!

Hapo ndio utaona tofauti ya private na serikali.....SAUT wanafunzi ni wateja wakati kwenye govt universities wanafunzi ni waajiri....that's why wanaweza kudai haki yao na serikali ikawajibika but in private thubutu uone chuo wanavyokupotezea uende kuifanyia serikali yako...kwa hiyo wateja wachache hawawezi kuharibu image ya chuo kizima...na by laws zao ni tofauti...na ndio maana wana somo la maadili pia!
 
Unajua MUCE ni branch ya UDSM...kama udsm hawaruhusu wanafunzi kujihusisha na biashara....hivi wanategemea nini pale wanapochelewesha pesa kwa wanafunzi kwa takribani wiki tatu sasa....?
Serikali ijifunze kutoa hela kwa wakati..yaani walishajiendekeza kwa mfumo wa malimbikizo!
 
Jana niileta thread ya mgomo wa wanachuo wa Mkwawa, na leo hali imeendelea kuwa mbaya kwani waliahidiwa kuwa hela yao ingeingizwa jana. Mpaka sasa hawajalipwa na mgomo umeendelea. Wanachuo wamefunga mageti yote na ndipo lilipokuja gari lililokuwa linakuja kubadilisha askari wanaolinda benki ya CRDB. walipofika getini wanachuo hao wakalizuia gari na kuanza kulipiga mawe ambapo askari mmoja alijeruhiwa. Gari hilo likaondoka kwa hasira na sasa hivi yamekuja magari matatu ya FFU wakiwa tayari kwa lolote.

Nitawajuza updates, niko eneo la tukio.
 
Wanachuo wa Mkwawa wamefunga barabara na kushambulia gari la Polisi lililokuwa likipeleka askari wa zamu kazini. Ntarudi for more updates.
 
Jana niileta thread ya mgomo wa wanachuo wa Mkwawa, na leo hali imeendelea kuwa mbaya kwani waliahidiwa kuwa hela yao ingeingizwa jana. Mpaka sasa hawajalipwa na mgomo umeendelea. Wanachuo wamefunga mageti yote na ndipo lilipokuja gari lililokuwa linakuja kubadilisha askari wanaolinda benki ya CRDB. walipofika getini wanachuo hao wakalizuia gari na kuanza kulipiga mawe ambapo askari mmoja alijeruhiwa. Gari hilo likaondoka kwa hasira na sasa hivi yamekuja magari matatu ya FFU wakiwa tayari kwa lolote.

Nitawajuza updates, niko eneo la tukio.

Hawajalipwa nini mshahara au pesa za kujikimu?
 
Sasa nao wapunguze hasira CRDB na mgomo wao wapi na wapi si wakomae na MUSHI anajua ela zilipo!
 
Wanafunzi waanaangaika kuwa hawana pesa Mawaziri wanachezea pesa kama mchanga na walipogundulika wanatafutwa wengine kwaajili ya kuendlea kula keki ya Taifa
 
Back
Top Bottom