Watu zaidi ya 150 hawajulikani walipo baada ya boti waliyokuwa wakisafiria kuzama katika Ziwa Kivu, katika mkoa wa Kivu kusini mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo. BREAKING: Boti Yazama, Watu 150 Hawajulikani Walipo! Kwa mujibu wa chanzo cha polisi katika eneo la Kalehe miili mitatu iliopolewa na watu 33 wameokolewa wakiwa hai huku abiria wengine 150 hawajulikani walipo. Mamlaka inayosimamia safari za majini katika ziwa Kivu inasema kuwa idadi ya watu waliokuwa kwenye chombo hicho haijulikani na wanahofu kuwa idadi ya watu 150 waliotoweka inaweza kuongezeka zaidi. Akiwa ziarani mashariki mwa nchi hiyo, rais wa DRC Felix Tshisekedi Tshilombo kupitia mtandao wa Twitter amesema, anafuatilia kwa karibu hali hiyo ili kuwatambua na kuwachukulia hatua kali waliohusika na ajali hiyo. Ajali kama hizo zimekuwa zikitokea mara kwa mara nchini DRC ambapo mwaka 2015, watu zaidi ya 100 walitoweka baada ya maboti mawili kugongana katika Mto Congo nchini DRC.