Brazil to play Tanzania in a friendly

WanaJF naombeni mawazo yanu,

Siasa ya Tanzania mbaya sana watu wanakufa kwa umasikini, maisha yao yanaendelea kuwa duni chini ya serikali ya CCM. Watu wamaichoka serikali hii watu hawtaki kuisikia hata kidogo. CCM imeona kwamba imepoteza muelekea kisiasa na kimaadili kwa viongozi wake.

CCM imetafuta ni kitu gani ambacho ikikifanya kinaweza kuondoa hata kupunguza machungu ya wananchi kwa serikali ya sisimu ni kuileta Brazil TAnzania. WaTanzania wenye akili changa wataona serikali inafanya kitu cha maana kumbe ndo inazidisha umasikini.

Hili ni chenga la macho kuwapumbaza wananchi wasiendelee kuisakama serikali ya CCM kwa kutofanikisha malengo yao.

WanaJF mnasemaje??
 
yani hiyo pesa ya kuwaleta brazil ingetuongezea hata ka elfu hamsini kwenye mshahara
 
Haya ni maisha, hii opportunity inaweza isitokee tena katika maisha yangu!!

Kwa hiyo kwa gharama yoyote ile lazima nikawaone wachezaji wa ukweli wanaocheza soka la peponi.

Labda TFF waninyime kuniuzia tiketi......si unajua bongo hizi tiketi zinaweza kununuliwa zote na mtu mmoja afu zikauzwa kwa bei ya kuruka mtaani. Usishangae hizo za Tsh. 30,000 zikauzwa kwa Tsh. 70,000!!

Kuhusu ghrarama ya kuwaleta Brazil hapa bongo mi naona sawa tu, tuongee ukweli jamani brazil kwa soka ni kitu kingine kabisa, no wonder they are very expensive!!
 
KWA MWENDO HUU WIZI NA UFISADI VITAISHA?
Consider this:
Kima cha chini cha mshahara ni 150,000/=
ticket ya mpira 200,000/=
Si ni kishawishi hiki?
ama kweli OPPORTUNITY ( AND TEMPTATION) MAKES THE THIEF!

Lets not be toooo -ve jamani. Hii comparison yako ya kiingilio cha juu na kima cha chini ina maanisha nini.??????

Ungefanya hivi unacompare kiingilio cha juu na kima cha juu au kiingilio cha chini na kiingilio cha chini ambacho ni 30,000. Elfu 30 ni sawa kabisa hata wa kima cha chini kama ni mpenzi wa mpira kweli na anavyo vijisenti atajibana.

Issue nyingine huwezi kufanya maamuzi ya kwa consideration ya factor 1ja tu ya kiingilio. Kuna factor nyinginine kama ya maximum capacity ya watazamaji, idadi ya wapenzi walio tayari kwenda kutazama mpira huo, gharama za mechi.

Ukiweka kiingilio elfu moja kufurahisha watu wote kesho utasikia watu wamekanyagana na kufa uwanjani itakuwa kesi nyingine.

Vile vile kichwa cha habari hii kiko biased sababu kimelenga kuonyesha kiingilio ni 200,000 wakati idadi ya ticket za laki mbili zitakuwa chache sana na hazitafika hata 1/4 ya zile zitakazouzwa elfu 30,000.

Viwango vya kiingilio walivyoweka ni sawa kabisa .
 
Sasa Brasil kuka ni mradi? Ni kwa nini kiingilio kikubwa namna hiyo? maana hata kimepita viingilio vya world cup yenyewe!!!!!:angry:
 
Nauliza hivi!............
Huu mpira kwenye Local TV utaoneshwa au hauneshwi??
 
Na nyie mnaopanga kwenda ni sehemu ya tatizo. Ukienda kwene hiyo mechi na kulipa kiingilio chochote kile you are a part of conspiring govt na kuwasaliti waTz wenzako. Pesa inayotumika kwene hizi extravagant activities haziko-justified kwa namna iwayo yote. Haya endeleeni kupanda chelewa, mtavuna madafu muda si mrefu.
 
OMG!!!!!
Bora mie sipendi mpira ila nasikitikia uharibifu wa pesa kiasi hiki wakati wadogo zangu na ndugu zangu kibao nimeshindwa kuwasomesha kwa ukosefu wa pesa.
 
so what?
waende wanaoweza lipia si wapo?
mayb unaweza pata ngekewa ya kupiga picha na KAKA

hahahahaa
 
MDHAMINI wa Yanga Yusuf Manji ameahidi kuwanunulia tiketi ya kushuhudia mechi ya kirafiki kati ya timu ya soka ya Taifa Taifa Stars na Brazil inayotarajiwa kuchezwa Juni 7 kwenye Uwanja wa Taifa Dar es Salaam.

Manji aliahidi hayo jana kwenye barua yake kwenda kwa Katibu wa Yanga Lawrence Mwalusako kuhusu kusaidia mkutano mkuu wa wanachama unaotarajiwa kufanyika Juni 6 kwenye ukumbi wa Bwalo la Polisi Osyterbay.

Hata hivyo katika barua yake hiyo Manji alisema wanachama watakaopewa tiketi ni wale watakaohudhuria mkutano huo tu.

Manji alikuwa akijibu barua aliyoandikiwa na uongozi wa Yanga kumuomba kugharamia mkutano huo wa kupitisha rasimu ya Katiba.

Manji alisema kwa vile Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) limewaomba wananchi kusaidia gharama za kuileta Brazil nchini kwa njia ya viingilio, hana budi kama mdau kufanya hilo kwa kuwalipia wanachama wa Yanga.

“Rejea barua yako ya Mei 27 2010 yenye kumbukumbu namba YASC/165/LPM ikinikumbusha barua niliyopokea mapema mwaka huu kutoka kwa Mwenyekiti Iman Madega akiniomba kugharamia mkutano barua ilikuwa ya Machi 16, 2010 kumbukumbu namba YANGA/CM/10/010”.

“Sasa nimefahamishwa juu ya mkutano huo na nitagharamia yafuatayo, nitalipia ukumbi, nitagharamia usafiri wa wanachama kutoka klabu mpaka eneo la mkutano na kuwarudisha, kwa hiyo nitaandaa mabasi ambayo yatakuwa klabuni asubuhi kuchukua wanachama, nitalipa posho kwa maofisa wa serikali watakaokuwepo kwa ajili ya mkutano huo…

“Pia nitanunua tiketi kwa wanachama wote wa Yanga watakaohudhuria mkutano huo kushuhudia mechi ya kihistoria kati ya Taifa Stars na Brazil,” ilisema sehemu ya barua hiyo.

Brazil inatarajiwa kuwasili nchini Juni 6 usiku na baada ya mechi yake ya Jumatatu itaondoka kurejea Afrika Kusini inakojiandaa kushiriki michuano ya Kombe la Dunia inayotarajiwa kuanza Juni 11.

Brazil ipo Kundi G katika michuano ya Kombe la Dunia ikiwa na timu za Jamhuri ya Watu wa Korea, Ivory Coast na Ureno.

Itarusha kete yake ya kwanza Juni 15 dhidi ya Korea kwenye Uwanja wa Ellis Park Johannesburg.

Tanzania itakuwa imepata ugeni mzito kwa mara ya pili katika soka wa kwanza ulikuwa ni ule wa Ivory Coast iliyokuwa Januari ikielekea Angola kwenye fainali za Kombe la Mataifa Afrika.



Chanzo: Habari leo
 
Hii inadhihirisha wabongo tulivyo ishiwa na akili ya kufikiria mambo ya msingi na ya maendeleo. Huyu manji amefanya ufisadi pale NSSF na katuibia pesa kibao za matrekta ya kuzoa taka manispaa kinondoni kwa sababu anavaa tisheti ya kijani/njano. Leo anawalipia kiingilio ktk mechi, anatumia pesa alizokwiba kwetu anatununulia pipi na peremende....alafu hapo utakuta vizee vya dar es salaam meno 32 nje.......pambafu kabisa.
 
Simba mmeanza viroho vyenu huu ni wivu.
Na nyie si mnamatajiri waArabu wawalipie viingilio.
 
Hii inadhihirisha wabongo tulivyo ishiwa na akili ya kufikiria mambo ya msingi na ya maendeleo. Huyu manji amefanya ufisadi pale NSSF na katuibia pesa kibao za matrekta ya kuzoa taka manispaa kinondoni kwa sababu anavaa tisheti ya kijani/njano. Leo anawalipia kiingilio ktk mechi, anatumia pesa alizokwiba kwetu anatununulia pipi na peremende....alafu hapo utakuta vizee vya dar es salaam meno 32 nje.......pambafu kabisa.


Jamani hizi lawama nyingine hazina kichwa wala miguu. Manji kweli anaweza kuwa fisadi ,llakini yanga wao eamemuomba awasaidie amekubali na ameongeza zaidi kwa kuwalipia viingilio, sasa tatizo nini? ulitaka akatae?. hivi kuna mafisadi wangapi wazawa nchi hii hawajui kutoa hata senti angalau kwa watoto yatima? kama lawama basi walaumu yanga na si manji kwaswala la msaada, na mlaumu manji kama manji kwa ufisadi
 
OMG!!!!!
Bora mie sipendi mpira ila nasikitikia uharibifu wa pesa kiasi hiki wakati wadogo zangu na ndugu zangu kibao nimeshindwa kuwasomesha kwa ukosefu wa pesa.

hapo sasa mdogo wangu, hata ningekuwa na hobby nadhani hiyo pesa ina shughuli muhimu kuliko kuwaona hao kina robhino, wataenda wasio na pesa za mawazo.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom