Kama nawaona dada zetu kina Mboni Masimba na Mange waki strategise namna ya kumkamata Kaka na Robinho kimahaba!!
Kaeni mbali na Kaka jamani coz jamaa ni mlokole wa ukweli!!
Ni bora niende kuangalia mazoezi ya abajalo ktk uwanja mashujaa sinza kuliko kwenda kuwaangalia brazil pasipo saint gaucho ambaye anaaminika kuwa ndiye balozi wa soka la mbinguni hapa duniani.
Timu ya taifa ya Brasil (Samba Boys) inatarajiwa kucheza na Taifa Stars katika mchezo wa kirafiki utakaofanyika tarehe 7 June 2010. Mechi hiyo itakayokuwa ya mwisho kwa Brasil kabla ya kuanza kwa Kombe la Dunia, inatarajiwa kufanyika katika uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam.
Hayo yamesemwa na balozi wa Brasil nchini Tanzania alipokuwa akizungumza na gazeti la The Citizen, ambapo alisema taarifa kamili na mipango mingine kuhusiana na hiyo mechi itatolewa na Rais wa TFF ndugu Tenga.
Source: The Citizen of 25 June, 2010
Mboni Masimba MALAYA CLASS A Tender hiyoooooooooooo kama nakuona ukiopoa Kaka duh noma Kaka mlokole itabidi tu uruke na Lucio maana lazima Etoo atamtonya
:rolleyez:MjasiliaMali huyu! Kazi kwenu dada zetu, Ruge kama kawaida walengeshe
Mimi si support hii issue - Its too political, lakini ki ukweli kucheza na Brazil haitasaidia chochote timu yetu - Sisi tuhangaikie na hapa Africa Mashariki kwanza Rwanda, Kenya Uganda wanatuacha. sisi tunapenda kuongea ongea sana na kujikwaza. Juzi juzi eti tukaomba game na Misri kujipima nguvu tukapigwa 5-0 nini kimefanyika baada ya kipigo?
Haya timu zetu zote zimetolewa katika mashindano ya kimataifa, tunaambiwa ligi yetu legelege tumelifanyia kazi hilo? zingatia ligi hii ndiyo inatoa wachezaji wa taifa tegemea nini mazao yake?
Kwa hiyo kuwaleta Brazil ndiyo itakuwa perfomance ya kina tenga au? kama wameamua kuja kupitia kwetu thats fine - lakini si eti tujipme nguvu na wao - we're too far behind.