EMANUEL LUKWARO
Member
- Aug 20, 2015
- 24
- 30
Mchakato wa kumn'goa raisi Dilma Ruseff madarakani ulioanza tar 17 mwezi uliopita jana ulichukua sura mpya baada ya kaimu spika wa bunge la wawakilishi kubatilisha kura iliyopigwa na bunge hilo ambapo wabunge wengi walipiga kura ya kumuondoa raisi Dilma.
Katika taarifa yake kwa vyombo vya habari kaimu spika Warlid Maranhao, amesema kuwa sababu za kubatilisha kura ya awali na kuanzisha mchakato upya kunatokana na kukiukwa na/au kutofuatwa kwa baadhi ya taratibu wakati wa upigaji kura, na moja ya ukiukwaji wa taratibu alioutaja ni Viongozi wa vyama vya siasa kuruhusiwa kupiga kampeni wazi wazi kwa wabunge.
Waldir Maranhao, alichukua nafasi hiyo ya uspika wiki iliyopita baada ya Eduardo Gunha aliyesimamia kura hiyo kuondolewa katika nafasi ya uspika kutokana na tuhuma za rushwa, uvunjaji wa haki na matumizi mabaya ya ofisi.
Hata hivyo spika wa bunge la Seneti Renan Calheiros, ambalo linatarajiwa kupiga kura kesho jumatano kuunga mkono au kupinga raisi dilma kuondolewa madarakani, Alitoa tamko jana hiyohiyo akipinga uamuzi wa spika mwenzake wa bunge la wawakilishi.
Renan Calheiros alisisitiza kuwa maandalizi ya kura ya jumatano yamekamilika na kura itapigwa kama ilivyopangwa. Tayari kamati ya bunge la seneti iliyoketi ijumaa iliyopita imemkuta rais Ruseff na hatia ya makosa ya kuvunja sheria ya budget.
Hata hivyo jambo la kushangaza tena ni kwamba leo jumanne spika wa bunge la wawakilishi bwana Warldir Maranhao amebatilisha tena tangazo lake la jana na kuubatiza mchakato aliouita wenye dosari.
Bwana Warlid Marnhao anasemakana kuwa ni mshirika mkubwa wa Gavana Flavio Dino ambaye ni mfuasi mkubwa wa raisi Russeff, hivyo yawezekana jaribio la kubatilisha kura ya bunge la wawakilishi ilikuwa ni sehemu ya mkakati wa raisi Dilma Ruseff kukwamisha mchakato wa kumuondoa madarakani,ili aweze kufunguliwa mastaka ya kuvunja sheria za fedha.
Endapo bunge la seneti litapiga kura ya kuunga mkono raisi Dilma kuondolewa madarakani, basi nchi itaongozwa na makamu wa raisi, na itatoa mwanya kwa raisi Dilma kufunguliwa mashtaka kuhusiana na tuhuma zinazomkabili. Na huenda ikawa hitimisho la maandamano ya miezi kadhaa yaliyokuwa yakiongozwa na upinzani kushinikiza raisi kuondoka madarakani.
Kwa upande wake Rais Ruseff amekuwa akisisitiza kila wakati kuwa hakuna sheria yoyote aliyovunja na ametafsiri kile kinachoendelea kama mpango wa mapinduzi ya serikali yake. Ameapa kuendelea kupambana kulinda haki yake binafsi na demokrasia mpaka dakika ya mwisho.
Kwa upande wao wachambuzi wa mambo wanaona kama vile kile kinachoendelea Brazil kimebebwa kiushabiki zaidi kuliko uhalisia, mitandao ya kijamii inaonekana kuchangia kwa kiwango kikubwa, na vyombo vya habari vya ndani vinatuhumiwa kumtenga raisi Ruseff na serikali yake kwa manufaa ya maadui zake.
Zipo taarifa ambazo sio rasmi kuwa serikali ya Ruseff ilikuwa na mpango wa kuwashughulikia mafisadi wakubwa wa nchi hiyo. Lakini kabla ya utekelezaji wa azma hiyo mafisadi wakamuwahi.