BRAVO Deus Kibamba, lakini! ...............

MchunguZI

JF-Expert Member
Jun 14, 2008
4,006
2,166
Deus Kibamba ni kijana ambaye amesaidia sana kuelewesha umma juu ya mambo mbali mbali na hasa ya kisiasa, kupitia vyombo vya habari. Hivi karibuni ndiye aliyeshika uenyekiti ktk mjadala wa katiba siku moja kabla ya muswada kuwasilishwa na kusomwa kwa mara ya pili (kama Bunge la CCM lilivyoamuwa).

Baada ya hapo kijana huyu amesikika ktk vyombo mbali mbali vya habari na binafsi nilimsikia mara ya mwisho BBC ya Kiswahili, akihojiwa na mwana dada mmoja juu ya hilo la mchakato wa katiba.

Tatizo nionalo siyo yale anayoyaeleza. Yote ni sahihi na nadhani yanastahili kusemwa. Namuomba sasa na yeye aamini kwamba suala hilo siyo lake peke yake. Kidogo naona kama anaingiza ukorofi wa kitaaluma (academic arrogance). Yaani ule wa kuamini kwamba hakuna mwingine zaidi yake. Itakuwa vizuri kabisa kama jukwaa la katiba analoliongoza litatoa watu wengine katika mapambano hayo ili kuondoa umiliki wake wa hoja hiyo.

Alipohojiwa na BBC alifikia hatua ya kujinadi kwamba yeye ni mtaalamu na kwa utaalamu wake ndo maana anaona yale ambayo wengine ni vigumu kuyaona. Hapo nikaona sasa kijana kasahau kwamba hiyo shule aliyoisoma kuna wengine pia waliwahi kusoma hapo na hata yeye alisoma na wengine wakijiita darasa na wote walihitimu. Naamini siyo yeye peke yake aliyehitimu, ni wengi.

Nimeaminishwa kwamba Kijana Kibamba ni mwana JF. Naomba unisikie. Hata Che Guevara aliwatumia wengine.
 
Unampongeza au unamkandya?

QUOTE=MchunguZI;2852797]Deus Kibamba ni kijana ambaye amesaidia sana kuelewesha umma juu ya mambo mbali mbali na hasa ya kisiasa, kupitia vyombo vya habari. Hivi karibuni ndiye aliyeshika uenyekiti ktk mjadala wa katiba siku moja kabla ya muswada kuwasilishwa na kusomwa kwa mara ya pili (kama Bunge la CCM lilivyoamuwa).

Baada ya hapo kijana huyu amesikika ktk vyombo mbali mbali vya habari na binafsi nilimsikia mara ya mwisho BBC ya Kiswahili, akihojiwa na mwana dada mmoja juu ya hilo la mchakato wa katiba.

Tatizo nionalo siyo yale anayoyaeleza. Yote ni sahihi na nadhani yanastahili kusemwa. Namuomba sasa na yeye aamini kwamba suala hilo siyo lake peke yake. Kidogo naona kama anaingiza ukorofi wa kitaaluma (academic arrogance). Yaani ule wa kuamini kwamba hakuna mwingine zaidi yake. Itakuwa vizuri kabisa kama jukwaa la katiba analoliongoza litatoa watu wengine katika mapambano hayo ili kuondoa umiliki wake wa hoja hiyo.

Alipohojiwa na BBC alifikia hatua ya kujinadi kwamba yeye ni mtaalamu na kwa utaalamu wake ndo maana anaona yale ambayo wengine ni vigumu kuyaona. Hapo nikaona sasa kijana kasahau kwamba hiyo shule aliyoisoma kuna wengine pia waliwahi kusoma hapo na hata yeye alisoma na wengine wakijiita darasa na wote walihitimu. Naamini siyo yeye peke yake aliyehitimu, ni wengi.

Nimeaminishwa kwamba Kijana Kibamba ni mwana JF. Naomba unisikie. Hata Che Guevara aliwatumia wengine.[/QUOTE]
 
mimi nafikri umemnukuu vibaya ,hakumaanisha kua yeye ndie pekee anaejua kinacho endelea ,kumbuka huo ni mtazamo wake na maono yake wala hakusema anapingana na maoni ya watu wengine au kua yeye ndio anaejua sana.yupo wazi sana jamaa unatakiwa umpe suport na sio kumchukulia kihivyo kwamba kangangania issue kua yeye ndio kilakitu.yumpe suport jamani.welldone KIBAMBA .
 
Hujaeleweka sana mkuu,but all in all, jamaa mchango wake umekuwa mkubwa ikiwa kuna mapungufu yaliyojitokeza(kama unavojaribu kuainisha) basi nadhani ni katika hulka ya ubinadaamu tu!
 
Huyu ni yule anayehubiri demokrasia na kuvumiliana wakati yeye mwenyewe hana sifa ya uvumilivu na demokrasia? Nakumbuka alivyomdhalilisha Mzee Chipaka kwa sababu tu alikuwa na maoni tofauti. Hopeless kabisa.
 
Back
Top Bottom