Nyambala
JF-Expert Member
- Oct 10, 2007
- 4,465
- 1,170
Bravo Chadema! Let's move on....
Kama kuna kitu ambacho Chadema wamefanikiwa katika kipindi hiki basi ni kutimiza ile hamu ya watanzania tulio wengi kuhusu siasa. Chadema imetumbanulia haswaa kwamba pamoja na kwamba ni "official opposition" bungeni lakini pia hata mtaani. Ule utitiri wa vyama umeshakuwa kiasi fulani "obselete" na "irrelevant". It is now clear kwamba CHADEMA ndiyo chama cha upinzani na upinzani unaoishi. Hebu tuangalie yaliyojiri "in just some few months" kutoka uchaguzi uliopita.
1. Chadema imeionyesha CCM na wananchi kwa ujumla kwamba ni vyama vipi ni vya msimu kama alivyowahi kunukulia JK wakati wa kampeni kwamba "Vyama upinzani ni vya msimu" . Toka wakati huo hakuna hotuba iliyosemwa na JK bila walau kuitaja Chadema, directly or indirectly.
2. Chadema imeifanya CCM kusahau hata ilani yake ya uchaguzi na kujikuta iko bize kutekeleza yale yaliyokuwa kwenye ilani ya Chadema mfano katiba mpya. Hatujasikia tena ilani ile iliyokuwa ikinadiwa wakati wa uchaguzi ilipoishia.
3. Chadema imeilazimisha CCM, narudi "IMEILAZIMISHA" CCM kukubali kwamba ufisadi ni janga tena haswaa ndani ya CCM na serikali yake. CCM wamejikuta sasa nao eti wako bize kupambana na ufisadi.
4. Chadema imepelekea CCM kufika hatua ya kukubali kudhoofika na hatimaye kuamua eti kujivua gamba pia kufanyika upya kwa semina elekezi.
5. Ni Chadema inayoitikisa CCM kiasi kwamba inajikuta kila siku CCM inahangaika kujaribu aidha kutoa visingizio kwa tuhuma inazozikabili au kujaribu kulinganisha tuhuma hizo na za Chadema as if "two wrongs can make a right"
6. Ni Chadema tu inayozungumzwa na hii secretariat mpya ya CCM, nani amewahi kumsikia Nape au Mukama akizungumza kuhusu CUF au TLP.
7. Chadema imeonyesha kwamba ni alternative, inakubalika na inahitajika. Imepenetrate mpaka kule kusikotarajiwa, imesemwa kuhusu ukabila, udini, ukanda na alwayz imekuwa bigger than hizi tuhuma na propaganda zenye lengo moja tu ya kuidhoofisha Chadema.
8. Everywhere you go in Tz ni Chadema, Chadema........narudia tena Bravo! Chadema.
Kwa sasa Chadema inahitaji kwenda hatua mbele zaidi, hili limeshawahi kusemwa na kutolewa ushauri na watu mbalimbali. Hatua hiyo/ hizo ziada haimaanishi Chadema iache kuendelea ku-sensitize watanzania kuhusu haki zao na hatima yao kupitia maandamano na mikutano. Bali ni hatua za kufanya ili kuipambanua Chadema tofauti na chama chochote kile cha siasa.
a. Chadema waanze kubadili mfumo wa chama chao na ikiwezekana usifanane kabisa na ule wa CCM. Mfano namna ya kuchagua viongozi, kuongoza, kuachiana madaraka, kushirikisha wanawake (sio kwa upendeleo).
b. Ile sera ya Chadema kuhusu serikali za majimbo ambayo binafsi naamini ni mojawapo ya sera bora kabisa kuweza kutukwamua na umasikini ianze kufanyiwa kazi. Mfano mipaka ya majimbo, namna ya utawala wa hizo serikali za majimbo, Viongozi wa majimbo hayo namna watakavyopatikana, Uchumi katika majimbo - Vyanzo, uzalishaji umeme, viwanda. Kifupi ni picha halisi ya hayo majimbo iwe tayari na wananchi tupewe nafasi ya kuchangia mawazo.
c. Itikadi ya Chadema iwekwe wazi na itetewe na viongozi wa Chadema na wanachama wake. Itikadi hii iwe ndiyo msingi wa kwa nini mtu ajiunge Chadema. Tofauti na CCM ambayo kwa sasa haileweki ina itikadi gani. Wao kila mahali wanajidai kuwapo.
d. Chadema ifanye harambee ya kujenga vitu flani flani ambavyo serikali ya CCM inaonekana kushindwa au kutojali mfano maktaba kubwa kuliko zote Tanzania (Of course baada ya hapo unaweza kuwapa TLS waendeshe). Bustani kubwa (Park) katikati ya mji Dodoma, Printing unit ya kisasa kwa ajili ya machapisho ya halmashauri za miji. Na mengine mengi!!!
Ni wakati muafaka sasa Chadema kusonga mbele maana inaonekana CCM kazi wameshindwa ila wako tayari kwa malumbano. Nawakilisha.