Brands maarufu za zamani Tanzania 90z kurudi nyuma

1. Kimbo

2. Mshindi ~ sabuni ya mche

3. Jambo~ lotion

4. Ayu~sabuni ya kuogea

5. DH~raba mtoni maarufu sana kuvaliwa shule

6. Sport ~ brand ya mfuko wa madaftari la kwanza hadi la tano la sita na la saba tulibeba begi za Montana au mifuko ya visalufeti

7. BenQ ~ 'ndopa' kiatu cha kijanja kina boonge la ulimi na kamba ndefu za rangi rangi

8. Lasonic~redio kaseti maarufu sana kupiga sebene na soukous za kikongo vilabuni enzi hizo migoma kama 'zangulo' 'yondo sista mwanamama iyee maua' nk

9. Sanyo~hii brand ya redio kaseti ya kishua utazikuta kwa matajiri tu wa enzi hizo kama akina Kasokela na Pataya au Bob G European brand hiyo ya mbao lakini.

10. National Panasonic ~ brand ya watumishi wa umma na mashirika ya umma au utaikuta kwa mwenyekiti wa chama cha ushirika 90z mwanzoni TV ndo zinaanza kuzoeleka huku bara

11. Adidas ~ ukivaa hiyo raba basi una ndugu anaishi ng'ambo

12. FILA ~ Brand ya Masela nondo

13. Reebok ~ ulishakuwa unaenda sana sinema kwa hiyo umeiga tu hilo sweta lenye kikofia maselanondo unawasimulia hii hata Vandame anavaaga

14. Nike~raba ya mabitozi wa wakati huo

15. Umoja~ brand maarufu ya malapa walivaa wa daslamu wakija likizo kijijini sisi tulivaa brand ya OK

16. Nikon~brand maarufu ya kamera

17. Pentax~brand ngumu na ya bei juu ya kamera mkikutana na wenzio kwa muhindi kusafisha picha unawaambia hiyo uliagiza Ng'ambo Japan iliogopewa sana hii brand na ilitoa picha kali sana icheki kule chini nimeiweka picha yake

18. Magauni ya red made/ready made~ Wanama waliyavaa sana haya Ila baadae ikaonekana ni ushamba ukivaa haya kule juu kusini walivaa sana wamama kutoka Makete na kaskazini wamama wakichaga waliyapenda sana...wengine waliyaita 'magauni mtunguo'

19.Mafuta ya kupakaa ya Rays/Reiz~haya yalikuwa kwenye kakopo kadogo maalum kwa wanafunzi, tulikuwa tunajisiliba kakopo kanaisha fasta sababu wakati mwingine mnajipakaa mafuta bila kuoga hasa tuliosoma shule za mikoa ya baridi kali

20. Viatu 'BORA' na BATA zilikuwa brands maarufu zikitengenezwa hapa 'i'nchini

21. Katambuga ~viatu vitokanavyo na matairi

22. Peugeot 504 ~ Gari maarufu walilotumia wenye nazo ni kama VX za enzi hizo ukimiliki hii unaogopewa na zilikuwa za kuhesabu

23. RTD~Redio Tanzania Dar es salaam ndilo jina maarufu la redio pekee Tanzania bara wakati huo hadi 1994 mbadala ilikuwa KBC ya Kenya BBC London, DW, Channel Afrika,VOA swahili,Redio China Kimataifa FEBA redio,na Ile ya Manzini Swaziland unazipata kwenye SW hatukuwa na FM hadi 1994...ukisachi chaneli inalia 'ko','ko''ko'...

24. Mkulima~ni brand maarufu sana ya redio ambayo aghlabu kaya nyingi Tanzania walikuwa nayo ilikuwa simple ina kasha la mbao saketi ndogo yenye genge ndani ilisifika kwa kunasa vizuri mawimbi hata ukiwa kondeni

25. Swala,Avon,Phonex ~ brands maarufu za baiskeli wakati huo,ukiona baiskeli ya gia basi fahamu ni ya paroko muumini kaazima akachukulie maziwa apeleke mission

26. Majira ndilo gazeti binafsi lililokuwa maarufu sana wakati huo 90z mengine ni Mzalendo, Uhuru, Daily News nk

27. Katitu ~ni brand pekee ya music wa Kenya iliyokubalika Tanzania lakini zaidi wakenya waliukubali sana muziki wa Tanzania hadi leo iko hivyo

28. Elias Magembe,Tommy Atandi,Aika Elinewinga,Mwamoyo Hamza,Tido Muhando,Emmanuel Muganda,Waihenya Kabiru,Abdul Shakur Aboud,Joseph Warungu na wengineo...hizo ni Brands maarufu za watangazaji waliovuma kwenye Idhaa za Kiswahili za BBC London na Sauti ya Amerika VOA

29. Edda Sanga~Mtangazaji mwanamke wa kwanza kusoma TAARIFA YA HABARI hapa Tanzania alifanya pia kipindi maarufu cha watoto Mama na Mwana...hii ni brand kongwe hongera mama kwa Sasa yupo na taasisi moja ya waandishi sijui inaitwaje nshaisahau

30. RETCO ~ brand maarufu ya makampuni ya serikali ya usafirishaji yalikuwepo kila mkoa eg RUKWA~RETCO, MBEYA~RETCO nk nk

31. NOREMCO, KAJIMA, SOGEA nk ~ brands maarufu kwa ujenzi hasa wa mabarabara miaka ya 80 hadi 90z kati ya haya naliona NOREMCO tu hapa Mwenge Daslam karibu na kwa Mwingira.....na yalijenga mabarabara kwa viwango sana...miongoni mwa barabara BORA KABISA Tanzania ile ya Tukuyu walijenga SOGEA

32. Leyland na Benz ~ brands maarufu za malori hao benzi walivuma hata kwa gari ndogo sedans hizo waliendesha vigogo kv Mkuu wa Ushirika wa mkoa au matajiri wakubwa. Yacheki pichani

33. Ndobolo ~ kibwagizo muhimu ktk sebene za DRC mwenye nacho angekikatia copyright kabisa maana wenzie wote walikidesa hiki, nacho ni song brand

34. Njumu za Romalio zilivuma sana early 90s hadi mid wanafunzi primary walivaa hizi kama kiatu cha shule kabisa

35. Jonas Savimbi ~ mbabe wa vita huko Angola alietikisa sana angalau kila mwananchi alifahamu habari muhimu za kitaifa na kimataifa maana uzalendo ulikuwepo na tulifuatilia habari muhimu unlike kizazi hiki cha udaku (mnisamehe wadogo zangu ila ndio ukweli nikiwauliza hapa Jamal Kashoghi ni nani hamtasema ila nikiuliza Wema Sepede ni nani mtajibu fasta).....Thomas Sankala pia ni mbabe wa vita alievuma sana.

36. General Tyre~ brand muhimu na maarufu ya tairi ilitumika kote nchini na ilimudu mazingira ya mabarabara yetu huko vijijini

37. Buluga, sukarigulu ~ sukari mbadala kwa familia nzima , wengine waliita asante Nyerere

38. Sogesa/Sogeza ~ kampeni iliyofanikisha vijiji vipya na kuachana na nyumba za peke peke zilizobaki kuwa mahame,hilo jina ni kama hizi operesheni za siku hizi operesheni sangara, kuunga juhudi,nk

39. ASAHI ~ brand muhimu kabisa ya saa ya mkononi tuliipenda sana pia ilikuwepo DISCO saa yenye calculator asikwambie mtu hizi zama tamu sana, and we were proud of whatever we had and enjoyed.

40. Ajanta ~ brand ya saa ya ukutani
Namba 29 kipindi cha Mama na Mwana sio alikuwa Debora Mwenda yule hebu wahenga angalieni vizuri kumbu kumbu vizuri
 
Umesahau VIP

Umesahau VIP = chupi hizi bwana zilikiwa noma sana upo uwanjani unacheza mpira gafla inakatika unashangaa imepanda kifuani watu kelele wewe.

Ukiwa mchafu sasa chawa za kufikia tu
 
Utumie Kibuku eeh ni pombe bora, tumia kibuku ni pombe boraaaa.

Hapo tunajiandaa kusikiliza kipindi cha kina Jangara siku ya Jumatano saa tatu na nusu baada ya majira.

Kibuku waliwahi kuwa wadhamini wakuu wa hiko kipindi.
Very true.... Jangala na mwanae Mshamu
 
Nakumbuka tamthiliya ya Tausi mwishoni mwa miaka ya '90
Hiyo tamthilia na TV zilishaanza kununuliwa, michezo ya redio ndio ilikuwa kama TV, jumamosi usiku baada ya kipindi cha majira kama kwenu kuna redio nyumba za jirani wote wanakuja kujazana kuwasikiliza kina mzee jongo, havijawa ba wengine wengi. Jumapili tunasikiliza mahoka kabla ya club raha leo show..... RIP Halima Mchuka
 
Mafuta- SHANTI
Sabuni ya kukogea -GARDENIA
Sabuni ya UNGA - FOMA
Usafrishaji- - KAUDO,KAUMA,KAUTA,KAUMU,KAMATA
Magazeti - MFANYAKAZI,UHURU,MZALENDO,DAILY NEWS,SUNDAY NEWS,SANI
Viatu - UTANIKOMA SAA8, CHACHACHA,
Hahahahahahahaaa unanikumbusha enzi za kasheshe komesha. Na tingisha
Hahahahahahaa ukilikosa kasheshe jimalize
 
Kibaba...
Sumni tulinunua pipi za rangi
Togwa na vibata
Shuleni kulikiwa na somo la sanaa na tulilima sana pamba
Soda ya Fahari na Vimto
Asubuhi tulienda shule na mahindi ya kuchemsha mamung'unya na maboga
Kibisa
Power ilanda
Mazingaombwe
Mumiani
Ngoma za mashetani
Bwimbwi
Pepeta
Nguo za mchelemchele
Moka
Kula daku
Enzi za pawa mabula
 
Back
Top Bottom