Boyfriend ananitegemea

Boyfriend ananitegemea

Hali zenu wana Jamii forum naombeni ushauri wenu,

Mimi ni msichana wa miaka 28 nina degree Bcom,boyfriend wangu ana miaka 34 ni mwalimu serikalini.tulipoanza uhusiano nilikua mpweke tukaingia kwenye mahusiano,yeye kutokana na umri kwenda anatafuta mtu wa kuoa.

Huwa anagusia kuhusu ndoa mi namwambia kwanza ajiandae kimaisha either asome afikishe level ya degree au kama ana njia mbadala ya maisha, cause kama mimi sina kazi ni ngumu kuishi kwa kutegemea mshahara wake nikajipa mahope mayb nitulie nae ipo tu siku atawini maisha kila siku namkazania asome au abadili kazi navyomuona mwenzangu hana haraka ya kukazana kimaisha.

Kinachoniboa hua ananiomba hela ya matumizi wakati mwengine hadi nauli anaomba,sim yake katupa anatumia yangu na aliniambia sometimes anapandaga daladala bila nauli,jamani mtu gani wa kuanza nae maisha huyu? Natamani nimuache ila ntaanzia wapi,kumpenda nampenda ila maisha yanamshinda hua anamuombaga hadi mama yake ela, msinitukane mnishauri.alafu ana wivu mpaka nakosa amani akipiga simu nisipopokea kanuna
.

Ningefurahi kama ulivyoviandika humu,ungemwambia boyfriend exactly kama vilivyo,uso mikavuu na mchana kweupe!
See,nahisi tayari umeshafanya maamuzi unatafuta wa kukwambia tu kwamba upo right.Binafsi, napenda sana mwanamke anayeniambia laivu bila chenga,japo truth hurts kama unampenda msaidie kwa kumueleza ukweli wazi wazi.Mabadiliko hayaji kwa kusaidiana hela,lakini pia kuna level ya mabadiliko ambayo inabidi ujipange kuyafikia,otherwise utarudi nyuma zaidi.

Kuna wanaume wachache sana wana-enjoy kuomba hela kwa wapenzi wao hasa in 30's,tena kwa wapenzi waliosoma vizuri tu.Angalia yupo kundi gani baada ya hayo,fanya maamuzi.
 
Back
Top Bottom