Kuna nchi Afrika zimeshtuka kimawazo,na kuna nchi zimelala kimawazo,moja katika nchi zilizoamka ni pamoja na nchi ya Botswana,na katika nchi zilizolala kimawazo ni nchi kama majirani zetu Kenya na Rwanda
Sio siku nyingi zilizopita raisi wa marekani alitanganza kuwa Jerusalem ni mji mkuu wa Israel,nchi nyingi zilipinga hatua hiyo,lakini
Kenya na Rwanda zilikubaliana na Trump...
Tukumbuke Kenya vile vile ilikuwa inaunga mkono utawala wa ubaguzi wa rangi(Apatheid) Afrika Kusini....
Trump katika siasa zake zinaohusu uhamiaji,kauliza kwanini nchi zenye watu
wachafu kama makalio, kakusudi watu wa Afrika ikiwemo Kenya,Rwanda na Haiti kwanini wanakuja kuishi marekani..?
Botswana imechukuwa hatua ya kumrejesha balozi wake nyumbani,ni hatua nzuri sana kwa watu wanojijua,
kama nchi za Afrika zitaiga mfano wa Botswana basi dunia itaziheshimu nchi za Afrika
Je Tanzania tutasubutu kama walivyofanya Botswana....?
Habari kutoka BBC
Serikali ya Botswana imemshutumu Rais wa Marekani kwa kusema mataifa ya Afrika ni "machafu" na kusema tamko lake rais huyo ni la kukosa kuwajibika, la kukera na "ubaguzi wa rangi".
Bw Trump alisema hayo alipokuwa akizungumzia sera ya uhamiaji ya Marekani, ambapo alisema anafikiti watu kutoka Haiti, El Salvador na nchi za Afrika hawafai kuruhusiwa kuingia kama wahamiaji Marekani.
Botswana imesema kupitia taarifa kwamba imemwita balozi wa Marekani nchini humo kufafanua iwapo Marekani inachukulia taifa hilo la kusini mwa Afrika kama "taifa chafu" na taifa la mabwege.
Taarifa hiyo ya Botswana imesema tamko la Trump ni la kukosea heshima taifa ambalo lina urafiki wa kufana na uhusiano wa kibalozi.
Botswana imeitaka jumuiya ya kiuchumi ya nchi za kusini mwa Afrika Sadc pamoja na Umoja wa Afrika kushutumu tamko hilo la Trump.
Bw Trump kwenye Twitter hata hivyo amejitetea na kusema hakutumia maneno hayo, lakini akasema aliyoyasema yalikuwa na "lugha kali".
Msemaji wa Umoja wa Mataifa amesema tamko hilo la Trump ni la kushangaza, la aibu na la ubaguzi wa rangi.
Rupert Colville amesema: "Iwapo yatathibitishwa, matamshi haya ni ya kushangaza na ya aibu sana kutoka kwa rais wa Marekani, nasikitika kwamba hakuna maneno mengine ya kueleza hili ila kusema kwamba ni ubaguzi wa rangi.