BoT yazipa mbinu benki kupunguza riba

beth

JF-Expert Member
Aug 19, 2012
3,877
6,326
NAIBU Gavana wa Benki Kuu Tanzania (BoT), Dk Bernard Kibese ameagiza taasisi za fedha na benki zote nchini, kupunguza kwa kiasi kikubwa gharama za uendeshaji ili kumudu kupunguza riba kwa wateja wao.

Alisema hayo wakati wa uzinduzi wa huduma ya malipo, inayotumia mfumo wa kadi ya viza kutoka Benki ya Letshego Dar es Salaam jana.

Kibese alisema ni muhimu kuwezesha kupunguza gharama za riba katika mikopo na huduma nyinginezo, ili miaka mitano ijayo Tanzania ifikie katika hatua ya uchumi ya tarakimu moja.

“Benki zote hapa nchini zihakikishe zinapunguza kwa kiasi kikubwa mikopo isiyolipika, ziwe na mitaji mikubwa, ziwe tayari kuongeza na kuanzisha huduma zenye ghrama nafuu, lakini pia benki hizi ziwezeshe kupunguza gharama za riba katika mikopo yao na huduma zingine ili ndani ya miaka mitano tuweze kufikia hatua ya kiuchumi ya tarakimu moja,” alisema Dk Kibese.

Aliongeza kuwa riba kubwa, huathiri wananchi na uendeshaji wa shughuli za kiuchumi, hivyo taasisi za fedha ziwekeze katika tafiti ili kuweza kubuni miradi mipya ya uendeshaji taasisi zao.

“Taasisi za fedha ziwekeze sasa katika tafiti ili kuweza kuvumbua huduma mpya hususani za kidigitali zitakazoendana na teknolojia, huduma hizi zihakikishe usalama wa wateja wenu na wananchi kwa ujumla,”alisema.

Aliipongeza Benki ya Letshego kwa kuanzisha huduma ya malipo kwa mfumo wa kadi ya viza. Alieleza kuwa elimu ya matumizi ya kidijitali katika mifumo ya malipo ni muhimu ikazingatiwa, kwani teknolojia inakua kwa kasi na watu wana haki ya kupata elimu ya matumizi mapya ya huduma za kifedha.

“Nawapongeza Letshego kwa maendeleo haya makubwa kwenu na sekta ya uchumi nchini, naendelea kuwasisitiza mtoe elimu na chachu ili watu waweze kutumia huduma hizi mpya za kifedha kwa ufasaha zaidi bila usumbufu, hii iende kwa taasisi zote za fedha na benki nchini,”aliongeza.

Akizungumza katika uzinduzi huo, Mkurugenzi wa Benki ya Letshego, Andrew Tarimo alisema uzinduzi wa huduma hii ni mwendelezo wa uvumbuzi wa matumizi ya teknolojia katika mifumo ya utoaji huduma za Benki ya Letshego.

Akizungumza kwa niaba ya Mwenyekiti wa Bodi ya Letshego, Noel Sangiwa, alisema wateja wa benki hiyo waendelee kuwa wavumilivu, kwani mabadiliko ya kiteknolojia yatakuwa mengi katika taasisi hiyo, ambayo bado inapanua wigo wa huduma zake za kifedha.
 
Riba haziwezi kupungua kama gharama nyingine za mikopo bado ziko juu.Mfano kwa sasa ,mikopo chechefu ni mingi kwasababu wateja wa mikopo wapo kwenye wakati mgumu wa kufanya marejesho kwa wakati, kwahiyo, inawagharimu benki kufuatilia mikopo iliyo kwama kwa wateja, hivyo riba inayo tozwa inagharimia pia gharama za ufuatiliaji.
 
Lengo la jiwe ni kuua benki zote. Anataka ibakie NMB tu. Jiwe akili yake anaijua mwenyewe.

"Tanzania iliuvaa mkosi 2015".
 
1) Ameagiza au ametoa mbinu?

2) kupunguza gharama za uendeshaji ni pamoja na kupunguza wafanyakazi?

3) Kama jibu la swali No 2 ni NDIO, ni akina nani wanaenda kuwa wateja wa bidhaa zitakazozalishwa na hao wateja wa benk ili warudishe mikopo?
 
Hata NMB saiv hatak ndugu yangu, saiv anataka TPB tu
Kweli tumeuvaa mkenge. Hajui kwamba anapoteza ajira za watanzania kibao waliokuwa wameajiriwa kwenye haya mabenki ambayo kila uchwao anaya-frustrate? Jiwe, jiwe, jiwe!!! Aaaah!..
 
Back
Top Bottom