BoT yapiga marufuku uuzaji noti chakavu

beth

JF-Expert Member
Aug 19, 2012
3,877
6,326
Benki Kuu (BoT) imepiga marufuku biashara ya kuuza fedha chakavu ikizitaka benki na taasisi za fedha kutoa fedha safi na kurudisha kwao zilizo chafu ili ziondoke kwenye mzunguko

Meneja wa benki hiyo anayeshughulikia noti na sarafu, Ilulu Ilulu, alitoa agizo hilo jana wakati wa semina kwa waandishi wa habari za uchumi na biashara inayoendelea mjini Mtwara.

Alisema katika maeneo ya masoko na minada kumekuwa na watu ambao wananunua fedha chakavu kwa bei pungufu na kwenda kubadilisha BoT kwa bei kamilifu kwa kuwa kwa mujibu wa sheria, fedha inabadilishwa kwa fedha kamili.

"Hairuhusiwi kuuza fedha chafu, tunataka wananchi kutoa taarifa, fedha inabadilishwa kwa fedha. Tuna sera ya kuhakikisha tunatoa noti na sarafu chafu kwenye mzunguko na kuhakikisha safi zinapatikana.

"Taasisi za fedha zinajua, zinapaswa kuja BoT kuchukua noti safi na kurudisha chafu ambazo tuna jukumu la kuziharibu kisheria," alifafanua.

Alisema wanachofanya wauzaji, wanazikusanya kwa bei pungufu, akitolea mfano noti ya Sh. 10,000 wanazinunua kwa Sh. 9,000, hivyo wakizifikisha BoT, wanapata faida ya Sh. 1,000 kwa kila noti.

Chanzo: IPP Media
 
Ni Vizuri, lakini BoT wanatakiwa sasa wawe na watu wao maalum kwaajili ya kukusanya hizo pesa mbovu mitaani.

Maana sioni uwezekano wa mtu kutoka Nanjilinji mpaka Bank au BoT kupeleka "buku" lake chakavu.
Bot wachukue hii point
 
Ni Vizuri, lakini BoT wanatakiwa sasa wawe na watu wao maalum kwaajili ya kukusanya hizo pesa mbovu mitaani.

Maana sioni uwezekano wa mtu kutoka Nanjilinji mpaka Bank au BoT kupeleka "buku" lake chakavu.
Ndo hapo sasa wanatoa agizo,badala ku kupendekeza utaratibu wa namna gani hata mtu alieko vjjn au kata,anaweza kubadilishiwa fedha chakavu kwa galama ile wanayoitoa wao bot. otherwise bado wamefeli
 
Benki Kuu (BoT) imepiga marufuku biashara ya kuuza fedha chakavu ikizitaka benki na taasisi za fedha kutoa fedha safi na kurudisha kwao zilizo chafu ili ziondoke kwenye mzunguko

Meneja wa benki hiyo anayeshughulikia noti na sarafu, Ilulu Ilulu, alitoa agizo hilo jana wakati wa semina kwa waandishi wa habari za uchumi na biashara inayoendelea mjini Mtwara.

Alisema katika maeneo ya masoko na minada kumekuwa na watu ambao wananunua fedha chakavu kwa bei pungufu na kwenda kubadilisha BoT kwa bei kamilifu kwa kuwa kwa mujibu wa sheria, fedha inabadilishwa kwa fedha kamili.

"Hairuhusiwi kuuza fedha chafu, tunataka wananchi kutoa taarifa, fedha inabadilishwa kwa fedha. Tuna sera ya kuhakikisha tunatoa noti na sarafu chafu kwenye mzunguko na kuhakikisha safi zinapatikana.

"Taasisi za fedha zinajua, zinapaswa kuja BoT kuchukua noti safi na kurudisha chafu ambazo tuna jukumu la kuziharibu kisheria," alifafanua.

Alisema wanachofanya wauzaji, wanazikusanya kwa bei pungufu, akitolea mfano noti ya Sh. 10,000 wanazinunua kwa Sh. 9,000, hivyo wakizifikisha BoT, wanapata faida ya Sh. 1,000 kwa kila noti.

Chanzo: IPP Media
Huko BOT wanakoenda kubadilisha hao wanunuzi wa noti chakavu, huwa hawatumii nauli?

Huo muda wa kutoka makwao kuja BOT kuanga foleni ya kubadilisha pesa wasingeweza kufanya shughuli zingine? Sasa kwanini wasioate faida?

Hata mimi, kuliko niunguze mafuta kwenda benki kubadilisha 10k ni bora anipe 9k tu niokoe pesa na muda
 
Kuna usumbufu flan hasa hela ikiharibika...kuna muda hata uende shell ambapo tunaamini wanapokeaga nao wanazikataa...BoT wana branch chache sana hata bank nazo kuzipata baadhi ya maeneo ni shida.
Kuwe na utaratibu wa kukusanya hizo hela
 
Nimejizuia kukebehi,....mkuu kila tawi la benk, NBC, Benki ya Posta nk wanatoa huduma hiyo ya kubadili noti chakavu na kukupa mpya hata kama sio mteja wao!
 
Ni kweli kwamba mwananchi wa kwaida mwenye pesa chakavu anahaki ya kuitumia pesa yake kwa thamani ile ile, lakini je, ni utaratibu gani waliouweka ili mwananchi huyo aweze kuwafikia kwa urahisi?

Kwa sababu wakati mwingine unaweza kukuta gharama za kuwafikishia wao hiyo pesa chakavu ni kubwa kuliko hiyo pesa yenyewe.

Sasa kwa nini asiiuze mtaani.
 
Benki Kuu (BoT) imepiga marufuku biashara ya kuuza fedha chakavu ikizitaka benki na taasisi za fedha kutoa fedha safi na kurudisha kwao zilizo chafu ili ziondoke kwenye mzunguko

Meneja wa benki hiyo anayeshughulikia noti na sarafu, Ilulu Ilulu, alitoa agizo hilo jana wakati wa semina kwa waandishi wa habari za uchumi na biashara inayoendelea mjini Mtwara.

Alisema katika maeneo ya masoko na minada kumekuwa na watu ambao wananunua fedha chakavu kwa bei pungufu na kwenda kubadilisha BoT kwa bei kamilifu kwa kuwa kwa mujibu wa sheria, fedha inabadilishwa kwa fedha kamili.

"Hairuhusiwi kuuza fedha chafu, tunataka wananchi kutoa taarifa, fedha inabadilishwa kwa fedha. Tuna sera ya kuhakikisha tunatoa noti na sarafu chafu kwenye mzunguko na kuhakikisha safi zinapatikana.

"Taasisi za fedha zinajua, zinapaswa kuja BoT kuchukua noti safi na kurudisha chafu ambazo tuna jukumu la kuziharibu kisheria," alifafanua.

Alisema wanachofanya wauzaji, wanazikusanya kwa bei pungufu, akitolea mfano noti ya Sh. 10,000 wanazinunua kwa Sh. 9,000, hivyo wakizifikisha BoT, wanapata faida ya Sh. 1,000 kwa kila noti.

Chanzo: IPP Media
Tatizo ni kumfanya mtu wa hali ya chini kuzidi kwenda chini, vijana wamejiajiri kupunguza umasikini kwa kuuza chenji lakini mnawamaindi hata kwa hicho kidogo!
 
Back
Top Bottom