BoT waruhusuni/wapeni muongozo Benki kuongeza kiwango cha kutoa pesa ATM

Yoda

JF-Expert Member
Jul 22, 2018
37,634
46,278
Hiki kiwango cha sasa cha laki nne katika ATM ambacho kipo karibia miaka 10 kimekaa muda mrefu sana bila mabadiliko, pia ni kidogo sana kukidhi hali ya sasa ambapo bidhaa zimepanda bei maradufu kwa kipindi cha miaka 5 iliyopita na bei bado zinaonekana kuzidi kupanda tu.

Kwa sasa ATM angalau watu waweze kutoa hadi milioni 1 kwa mkupuo na hadi milioni 5 kwa siku kutoka ATM. Pia itasadia wateja kutopoteza muda kwa kushinda ATM kutoa pesa au kuingia ndani ya benki kutoa dirishani.
 
Inawezekana
Tundu la kutolea noti laweza kutoa noti 40 tu kwa mara moja ndio maana huwezi kutoa zaidi ya laki 4 kwa mpigo mpaka urudie tena. Labda benki kuu ichapishe noti ya denomination kubwa zaidi shs 10 000
 
Inawezekana kufanyika programming ikatoa hata milioni 10 wakitaka.
 
Crdb tundu la ATM linatoa noti 60 ambayo ni laki 6.
Nadhani sio ATM zote za CRDB. Upande mwengine itakuwa ni issue ya faida kwasababu kila muamala unakuwa na makato, ukitoa nyingi kwa mara moja inapunguza hiyo faida, DTB mwisho laki tatu.. Ukitaka 1.2m inabidi utoe mara nne badala ya tatu...
 
Hiki kiwango cha sasa cha laki nne katika ATM ambacho kipo karibia miaka 10 kimekaa muda mrefu sana bila mabadiliko, pia ni kidogo sana kukidhi hali ya sasa ambapo bidhaa zimepanda bei maradufu kwa kipindi cha miaka 5 iliyopita na bei bado zinaonekana kuzidi kupanda tu.

Kwa sasa ATM angalau watu waweze kutoa hadi milioni 1 kwa mkupuo na hadi milioni 5 kwa siku kutoka ATM. Pia itasadia wateja kutopoteza muda kwa kushinda ATM kutoa pesa au kuingia ndani ya benki kutoa dirishani.
Pia amount ya kutoa kwa siku iongezeke. Badala ya 2mil waruhusu kutoa hadi 5mil

Hela yenyewe imepoteza sana thamani
 
Tundu la kutolea noti laweza kutoa noti 40 tu kwa mara moja ndio maana huwezi kutoa zaidi ya laki 4 kwa mpigo mpaka urudie tena. Labda benki kuu ichapishe noti ya denomination kubwa zaidi shs 10 000
Amana bank unatoa laki sita kwa mkupuo
 
Ile nafasi ya kutolea hela haitoshi kutoa noti 1000 kwa mpigo, nadhani wazungu wamezidesign kwaajili ya hela zao ambazo noti chache zina thamani kubwa.
Kuna kampuni nyingi za kutengeneza na kutoa huduma za ATM sio za wazungu peke yake, waende hata China.
 
Tatizo sio bank au BoT, hizo ATM nyingi zimekua designed kutoa noti 40 at a time. kuhusu limit ya siku hayo ni maamuzi ya bank husika, mara nyingi wanakua na kadi zenye privileges tofauti tofauti mfano mm nayo kadi ya NBC ambayo naweza toa hadi 3M kwa siku
 
Amana bank unatoa laki sita kwa mkupuo
Kumbe kuna machine zingine zinatoa zaidi ya noti 40? Nilikuwa naelewa hivyo tangu zamani kumbe si kweli, kwani ukikuta machine zimewekwa noti za elfu 5, huwezi kutoa zaidi ya laki 2. Sorry sikuwa najua hivyo kwa Amana Bank ATMs.
 
Tatizo sio bank au BoT, hizo ATM nyingi zimekua designed kutoa noti 40 at a time. kuhusu limit ya siku hayo ni maamuzi ya bank husika, mara nyingi wanakua na kadi zenye privileges tofauti tofauti mfano mm nayo kadi ya NBC ambayo naweza toa hadi 3M kwa siku
Kutoa hadi milioni moja iwe kiwango cha lazima kwa benki zote, zaidi ya hapo ndio iwe privileges.

Design za ATM zinaweza kubadilishwa muda wowote, huwezi kusema tutakuwa tunaendelea kutoa lakini nne kwa miaka 20 ijayo.
 
Sidhani kwa sababu za kiusalama, alafu wanaacha ivyo ili ufanye miamala mingi wapate faida
 
Hiki kiwango cha sasa cha laki nne katika ATM ambacho kipo karibia miaka 10 kimekaa muda mrefu sana bila mabadiliko, pia ni kidogo sana kukidhi hali ya sasa ambapo bidhaa zimepanda bei maradufu kwa kipindi cha miaka 5 iliyopita na bei bado zinaonekana kuzidi kupanda tu.

Kwa sasa ATM angalau watu waweze kutoa hadi milioni 1 kwa mkupuo na hadi milioni 5 kwa siku kutoka ATM. Pia itasadia wateja kutopoteza muda kwa kushinda ATM kutoa pesa au kuingia ndani ya benki kutoa dirishani.
Watu wanajitahidi kuelekea cashless wewe unataka mabulungutu yatoke kwenye ATM tu, shida ni idadi ya noti zinazoweza kutolewa na mashine mara moja. Ila ukitaka zaidi unatoa kwa mafungu na ndio hutaki kupoteza hizo dakika chache kutoa kwa mafungu.
 
Sidhani kwa sababu za kiusalama, alafu wanaacha ivyo ili ufanye miamala mingi wapate faida
Haya mabadiliko yataakisi uhalisia wa hali halisi ya sasa, thamani ya elfu kumi ya sasa labda ni sawa na elfu tano ya miaka 10 iliyopita. Elfu kumi miaka 10 iliyopita ulikuwa unapata sukari hadi kilo 7 sasa hivi unapata kilo 3 tu.
 
Back
Top Bottom