BoT waelezeni bodi ya bima ya amana iache upotoshaji

fbmetz

New Member
Nov 11, 2017
1
3
KUMEKUWEPO na upotoshaji mkubwa na wa makusudi unaofanywa na maafisa wa Bodi ya Bima ya Amana (DIB) kuhususiana na kwa nini wateja wa iliyokuwa benki ya FBME walichelewa kulipwa amana zao zilizopo katika benki hiyo kufuatia benki hiyo kufutiwa leseni yake ya biashara na kuwekwa chini ya DIB kwa ajili ya ufilisi.

Kuanzia katikati ya mwezi Mei,wateja waliokuwa wakifuatilia amana zao walijibiwa ya kuwa wangeanza kulipwa baada ya siku 30 lakini ikapita miezi mitatu bila ya kulipwa chochote. Na ilipofika mwanzoni mwa mwezi wa Agosti, wateja waliokuwa wakienda ofisi za DIB zilizopo katika majengo ya Benki Kuu ya Tanzania (BoT) au kupiga simu kufuatilia amana zao walikuwa wakijibiwa ya kuwa hawataweza kupewa amana zao kwa wakati ule kwa sababu wafanyakazi wa iliyokuwa benki ya FBME wamegoma kuendelea na kazi hivyo kusababisha zoezi zima la kuwalipa amana zao kukwama.

Maelezo hayo ya DIB hayakuwa ya kweli, yalikuwa ni upotoshaji mkubwa na wa makusudi wenye lengo la kuwachafua waliokuwa wafanyakazi wa FBME, ambao walikuwa na ushirikiano mzuri na wateja wao kwa takribani zaidi ya miaka 14 tangu kuanzishwa kwa benki hiyo hadi ilipopokonywa leseni yake ya biashara tarehe 8 mwezi Mei mwaka huu.

UKIWA MWONGO UNATAKIWA UWE NA KUMBUKUMBU NZURI
Hatimaye kuanzia tarehe mosi ya mwezi huu (Novemba), DIB walianza kulipa amana ya shilingi milioni moja na laki tano (1,500,000) kwa wateja waliokuwa na amana zaidi ya kiasi hicho na waliokuwa na pungufu ya kiasi hicho wanalipwa yote, kama sheria inavyotaka. Ifahamike ya kuwa DIB wameanza kulipa wateja PASIPO NA KURUDI KAZINI KWA HAO WAFANYAKAZI ambao kwa mujibu wa wao DIB waligoma kufanya kazi, je wale wateja mliokuwa mnawaambia hawawezi kulipwa kwa sababu wafanyakazi wamegoma wawaeleweje?

Haikuwa vyema kwa DIB kusema na kueneza uongo dhidi ya waliokuwa wafanyakazi, cha kushangaza MNAENDELEA kuwaambia wateja ya kuwa wafanyakazi bado wamegoma ndio maana zoezi linasuasua na litachukua muda mrefu kukamilika, tena mnaeneza na uwongo ya kuwa wafanyakazi wanadai mabilioni ili wateja wasipate amana zao.

Tungependa DIB mfahamu ya kuwa baada ya BoT kuiweka FBME chini ya uangalizi wake kuanzia tarehe 26 Julai 2014, kuna wateja walihamisha amana zao na kwenda benki nyingine, lakini wengine wakarudi baada ya miezi michache tu kutokana na ukweli kwamba huko walikokwenda walikosa huduma bora za kibenki kama walizokuwa wakizipata FBME, ukiwemo uhusiano mzuri baina ya wateja hao na wafanyakazi. Na kwa miaka mitatu ambayo FBME ilikuwa haifanyi miamala ya nje, wateja hao bado walituunga mkono wakiamani ipo siku huduma zitarejea kama hapo awali.

DIB mtambue ya kuwa sisi tuliokuwa wafanyakazi wa FBME tuna deni kubwa sana kwa wateja wetu kwa kutuunga mkono na kuendelea kubenki na sisi kipindi chote ambacho tulikuwa tumewekewa vikwazo vya kufanya biashara na FINCen, zaidi tungependa kuwa na mahusiano nao mazuri nao hata huku tuliko nje ya FBME, sasa mnapo waambia ya kuwa ‘KUGOMA’ kwetu kulisababisha mchelewe kuwalipa, je wakati huu mnaofanya malipo unatofauti gani na wakati ule ilhali hakuna wafanyakazi waliorejea kazini?

Hatukutegema hili kutoka kwenu hasa kwa wakati huu ambapo bado kuna shauri linasikilizwa mbele ya Tume ya Upatanishi na Usuluhishi (CMA) baina yetu na DIB, hivi hata hilo shauri litakapoisha mnategemea kupata ushirikiano wa aina gani na waliokuwa wafanyakazi? KUMBUKENI ya kuwa kwa sasa mnafanya malipo hayo kwa kutumi EXCEL SHEETS na sio mfumo (system) halisi wa benki, na bado mmekuwa mkiwaomba waliokuwa wafanyakazi wanaokuja kuchukua amana zao wawasaidie kutafuta mafaili au kuwatambua wateja (AJABU SANA), mtu anakuja kuchukua amana yake kama mteja mwingine, nyie mnamuomba awasaidie kuwatafutia mafaili? HAMKUJIPANGA?

UKWELI ULIVYO
Ni kwamba Julai 22, DIB kwa ridhaa yake na kama sharia inavyotaka, iliwaachisha kazi wafanyakazi wote wa iliyokuwa benki ya FBME, kwa ufupi kuanzia Julai 23 hakukuwa na mfanyakazi wa iliyokuwa FBME benki,wafanyakazi wote walipewa barua za kuachishwa kazi zikionyesha baadhi ya stahiki zao watakazolipwa. Tusingependa kueleza zaidi kwa sababu shauri tayari lipo kwenye mikono ya sheria, yaani CMA kwa ajili ya utatuzi.

Baada ya DIB kukabidhi barua za kuachisha kazi wafanyakazi wote, wakataka kukabidhi barua za MIKATABA MIPYA YA AJIRA za mikataba kwa baadhi ya wafanyakazi ili waendelee kufanya kazi na DIB ya ufilisi (kuwalipa wateja amana zao na/au kukusanya madeni ya benki inayowadai wateja). Barua za mikataba mipya zilikataliwa na wote waliotakiwa kubaki kazini. Walikuwa na sababu zenye mashiko za kukataa kuendelea na kazi, kwanza ni HIARI ya mtu kuendelea au kutoondelea na kazi, pili kutokana na madai waliyokuwa nayo hawakuona sababu ya kuendelea kufanya kazi na DIB.

Kwa hiyo ifahamike ya kuwa KISHERIA hakuna hao wafanyakazi ambao DIB wanasema WAMEGOMA, kusema hivyo ni kuwavunjia heshima na kutaka kuwakosanisha na wateja na jamii kwa ujumla. Ukimpa mtu mkataba wa kumuomba kufanya kazi naye ni HIARI ya mtu huyo kukubali au kukataa, sasa utasemaje wafanyakazi wamegoma?

Mwisho tunawatakia kila la kheri katika mchakato wenu wa kuwalipa wateja kwa kutumia EXCEL SHEETS. Tunatumai ‘balances’ za wateja zilizo kwenye hizo EXCEL SHEETS mlizokaa nazo kwa miezi mitano, zina shabihiana na ‘balances’ za wateja kama zilivyokuwa kwenye systems mpaka tarehe tarehe 8 Mei 2017.
 
Wa Tanzania sijui kwanini hatupendani...mtu anafurahia kabisa mwenzie apate majanga. Tulitegemea taasisi kama DIB na BOT kuwa kuna professionals wazuri wangetumia busara na utu kulitatua tatizo hili dogo..sasa nimeamini kuwa hata usome vipi bado roho mbaya na ubinafsi hautoisha kwa baadhi ya wa TZ..

Yaani hawa DIB ni wapuuzi kweli...si wawafukuze kazi basis hao wanaowaita wafanyakazi waliogoma.Umuachishe MTU kazi kwa sheria ya Tanzania wakati aliajiliwa kwa sheria ya kimataifa?!Mungu you pamoja nanyi Ex~FBME staff.
 
Back
Top Bottom