Unajua ukitaka kula pesa pesa ya serikali ni lazima uanzishe ka-activity fulani ka ku-justfy malipo. Wengine wanaanzisha visemina kwa mamilioni ya pesa na wengine wanaanzisha zoezi la kutengeneza pesa mpya japo hazihitajiki ki vile ilimradi tuu mchakato huo utapelekea malipo fulani. Ndiyo maana unaambiwa uongozi serikalini ni mtamu ndugu yanguHela mpya hazikidhi ubora, zina ghushiwa kirahisi na zina ubora hafifu.
Pesa za zamani ni bora kuliko mpya
Kuna makosa kidogo ya kiufundi yalifanyika kwa mfano yule mjusi kwenye noti kuonekana kwa uwazi sana. Lakini marekebisho yanafanyika ikiwa ni pamoja na kuongeza ukubwa, uzito, harufu etc. Habari nyingine ni za kiintelejesia zaidi kwahiyo siwezi kuziweka hapa.
Unajua ukitaka kula pesa pesa ya serikali ni lazima uanzishe ka-activity fulani ka ku-justfy malipo. Wengine wanaanzisha visemina kwa mamilioni ya pesa na wengine wanaanzisha zoezi la kutengeneza pesa mpya japo hazihitajiki ki vile ilimradi tuu mchakato huo utapelekea malipo fulani. Ndiyo maana unaambiwa uongozi serikalini ni mtamu ndugu yangu
Ni heri wabadilishe noti ya sh elfu kumi iwe ktk mfumo wa sarafu na sarafu ya sh 200 iwe ndo noti vivyo hivyo kwa noti ya sh elfu tano na elfu mbili natumai hapo uchakachuaji utakwisha.Kwa sababu haitakuwa rahisi kugushi sarafu ya sh elfu kumi na pia mtu hawezi kujiangaisha kwa ajili ya kugushi noti ya sh mia mbili. Ni mtazamo wangu.
<br />Hawa viongoz ni wapuuz sana. Lkn watakuwa wamesaidia nchi kuingia kwenye historia ya kutumia currency mbili tofauti at once.
Kiukweli noti mpya ni balaa tupu. Hata kaisari hawezi zipokea
Mara nyingi tumekuwa wagumu kuelewa somo. Umeambiwa pesa hizi zina ubora zaidi na zina security features ambazo haziwezi kughushiwa kiurahisi lakini hatuelewi. Au mtu akivaa sarawili ya kitambaa kizito ndo anakuwa amevaa nguo yenye ubora. Hizi hela niza kisasa zaidi isipokuwa matumizi yetu ndo mabaya. Mfano; mnaenda kanisani kutoa sadaka mmekunja noti, mnaficha noti sehemu za siri zinapata ukungu, wengine wanachimbia pesa chini ya shimo, wengine wanazikunja kwenye pembe za kanga, hatutumii wallet, mikono yetu inakuwa na unyevu wa maji na jasho lakini tunashika pesa. Hayo ni baadhi tu ya matumizi mabaya ya pesa zetu. Ukiangalia American Dollar---huwezi kuikunja kwa sababu unajua inaweza kukataliwa either na benki au ikagoma kupita kwenye mashine ndo maana mnazitunza vizuri.
Mie nakubaliana na Ndullu kabisa kuwa hizo noti ni bora kabisa kuliko zote zilizowahi kutoka hapa TZ.