BOT Inashirikiana na wezi kuua mabenki?

domokaya

JF-Expert Member
Apr 22, 2010
3,545
1,719
Benki Kuu ya Tanzania ndio taasisi yenye usimamizi wa taasisi za kifedha zifanyazo kazi nchini zikiwemo mabenki.

Moja ya jukumu la Benji Kuu ya Tanzania ni kui endorse maafisa wakuu wanaotaka kuajiriwa na benki hizo.

Jukumu hili Benki Kuu imeonekana kutolitilia maanani na badala take kuwapitisha ma CEO wenye sifa ya wizi na ubadhirifu tena wenye 'cartel' ya maofisa wezi ambao CEO mwizi akienda Benki fulani basi atafanya juu chini aende na 'watenda kazi' wake.

Utendaji wa Ma CEO wa aina hii Mara nyingi ni wa upigaji dili kupitia ununuzi wa mikopo ambayo baadae hufanyia re categorization na kuifanya black debts. Mikopo hii ni yao kupitia kwa ndugu na jamaa zao.

Kuna hila nyingi za kibenki timu ya kazi huzifanya haraka haraka pindi waingiapo ili kuwahi udongo ungali maji.

BOT haina budi sasa iyapitie mabenki yote ambayo imepitisha ma CEO wake hivi karibuni kuona utendaji wao.

Mabenki kama Advans na mingineyo ya hivi karibuni yafaa yatupiwe jicho LA haraka kama BOT haihusiki na mpango wa kuyafilisi na kuyaua haya mabenki.

Ikiwa kuyamaliza haya mabenki, kuwatia hasara watanzania na taiga kiujumla ndio lengo, basi lengo linaelekea kutimia.
 
Back
Top Bottom