BoT: Huu ni Upuuzi Mkubwa!!! | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

BoT: Huu ni Upuuzi Mkubwa!!!

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Mdau, Jan 1, 2011.

 1. Mdau

  Mdau JF-Expert Member

  #1
  Jan 1, 2011
  Joined: Mar 29, 2008
  Messages: 1,771
  Likes Received: 251
  Trophy Points: 180
  Share14

  [​IMG]
  Benki kuu ya Tanzania imetoa toleo jipya la noti za shs 500, 1000, 2000, 10,000. Noti hizi zitaingizwa katika mzunguko tarehe 1 Januari 2011. Noti za zamani bado ni fedha halali na zina thamani sawa na zile mpya.

  Zitaendelea kutumika na kuwepo katika mzunguko sambamba na hili toleo jipya la noti mpaka hapo hizo za zamani zitakapotoweka taratibu na hatimaye kwisha kabisa kwenye mzunguko. Hivyo basi, wananchi wanashauriwa kuendelea kuzipokea na kuzitumia noti za zamani bila shaka au wasiwasi wowote kuhusu uhalali wake hadi hapo zitakapokwisha na kutoweka kabisa katika mzunguko.
  Vilevile ieleweke kuwa hakutakuwa na ubadilishaji wa kupeleka noti za zamani benki na kutaka kupewa mpya.
  Toleo hili la noti mpya lina taswira inayozingatia mandeleo ya uchumi na jamii. Tumefanya mabadiliko kidogo katika toleo jipya kwa kuweka picha za waasisi wa taifa letu. Hayati Mwalimu Julius Kambarage Nyerere anaonekana kwenye noti ya shilingi elfu moja na Hayati Sheikh Abeid Amani Karume kwenye noti ya shilingi mia tano. Noti tatu zilizosalia yaani elfu mbili, elfu tano na elfu kumi zitaendelea kuwa na picha za wanyama pori ambao wanapatikana kwa wingi kwenye hifadhi na mbuga zetu za wanyama. Hata hivyo, kutokana na kupunguza ukubwa wa noti hizi mpya tumeweka picha za vichwa vya wanyama hao badala ya wanyama wazima kama ilivyo kwenye noti za zamani.
  Ili kupambana na uhalifu wa kughushi na kuongeza muda wa noti hizi kukaa katika mzunguko kwa muda mrefu kabla ya kuchakaa, toleo hili limeongezewa ubora kwa kuweka alama maalum mpya za usalama na kutumia taaluma mpya ya kuziimarisha. Alama mbali mbali za usalama zimeboreshwa na kwa mara ya kwanza kabisa alama ya "motion" ambayo ni rahisi sana kutambulika kwa macho imetumika katika noti hizi.
  Ili kuelimisha wananchi kuhusu alama za usalama zinazotambulisha uhalali wa noti zetu, tumetoa matangazo na vipeperushi ambavyo vitasambazwa sehemu mbali mbali za nchi. Taarifa ya alama za usalama za noti pia zipo kwenye tovuti ya Benki Kuu kwa anwani Bank of Tanzania (BOT): Home Page : Benki Kuu ya Tanzania
  Ni muhimu kwa umma kufahamu alama za usalama ili uweze kutofautisha noti halali na bandia kwa urahisi. Hata hivyo Benki Kuu inapenda kutahadharisha watu wawe waangalifu na kuzichunguza noti zote wanazopokea hasa kwenye giza ili kuhakikisha kwamba ni noti halali. Uchunguzi ufanywe kwa noti zote zilizopo kwenye mzunguko pamoja na za zamani. Endapo wana mashaka warejee kwenye mabango na vipeperushi vilivyotolewa na Benki Kuu au tawi lolote la Benki Kuu.
  Gavana
  Benki Kuu ya Tanzania


  Mtizamo wangu...............

  Hivi wachumi wote waliojaa pale BoT wameshindwa kutafakari ni namna gani ya kuboresha thamani ya shilingi ya Kitanzania, matokeo yake mnatuletea uboreshaji wa sura ya noti?? Ni uvivu wa kufikiri au akili zimedumaa?? Maisha ya Mtanzania wa kawaida, tabu na madhila yote anayopata ni msalaba wenu huo, hamtauepuka kwa kusaliti taaluma zenu na kushirikiana na wanasiasa kufisadi tenda...
   
 2. Kiresua

  Kiresua JF-Expert Member

  #2
  Jan 1, 2011
  Joined: May 13, 2009
  Messages: 1,202
  Likes Received: 30
  Trophy Points: 145
  Mdau, asante kwa uzi huu, kwa mtizamo wangu kukua kwa uchumi hakutegemei wachumi wa BOT pekee, kubadisha muonekano wa Noti wametekeleza jukumu lao. Ni proposal ngapi za BOT kwa serikali ziko kwenye mashelfu hazifanyiwi kazi?

  Uchumi wa Tz pamoja na kuongezeka kwa thamani ya fedha ya TZ pamoja na kwamba BOT wanaregulate, inategemea sana na utashi wa kisiasa, kama Raisi ansema atajenga machinga complex (A.K.A. Wachuuzi Accademy) badala ya kutuambia mbinu za kukuza secta ya viwanda ili tuzalishe zaidi tulete dola hapa nchini, tupunguze mfumuko wa bei, tukuze ajiza za uhakika, Unategemea nini!? BOT waongeze value ya Noti? no way dude!!! Wanasiasa wetu wanajigamba kuongeza ajira 2,000,000 = mkuu wa nchi alitumbia eti ukifungua baa lazima ulete ajira kwani atakayeleta bia au soda na mkokoteni, amepata ajira, atakaye kuwa naokota visoda kwa ajili ya kuuza kama chuma chakavu naye kupitia baa yako amepata ajira (akatoa mfano wa zile baa pale Kinondoni makaburini) Kwa kweli nilishtuka sana kama kweli tuna mawazo finyu namna hii!!!
   
 3. Mujuni2

  Mujuni2 Senior Member

  #3
  Jan 1, 2011
  Joined: Jun 11, 2008
  Messages: 142
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  Serikali inaposhindwa kukusanya kodi, inachapisha pesa na kuweka kwenye mzunguko. Angalia value ya Tsh imeshuka kwa kiwango cha kutisha, hii ni danganya toto, wamechapisha noti sababu hawana vianzo vya mapato.
   
 4. tzjamani

  tzjamani JF-Expert Member

  #4
  Jan 1, 2011
  Joined: Oct 9, 2010
  Messages: 997
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 0
  Siasa mbovu ndio inayoharibu TZ wasomi wameamua kuingia kwenye siasa za ufisadi baada ya serikali kupoteza mwelekeo. Familia isiyo na kiongozi imara awe baba au mama haina mwelekeo watoto wana lala njaa, hawaendi shule, .........................

  TZ Hatuna uongozi!
   
 5. m

  mzambia JF-Expert Member

  #5
  Jan 1, 2011
  Joined: Dec 31, 2010
  Messages: 885
  Likes Received: 19
  Trophy Points: 35
  Shame bot shame upon you
   
 6. K

  KIBE JF-Expert Member

  #6
  Jan 1, 2011
  Joined: Nov 23, 2010
  Messages: 943
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Sijaona sababu za msingi za kubadilisha note zilizokuwepo kuletwa mpya. Bot ndio wanaolinda mzunguko wa fedha na thamani ya yake.
  Makusanyo ya kodi ya serikali yameshuka sana sana na matumizi yamekuwa makubwa kuliko mapato.
  Mtazamo wangu hiyo ni danganya toto tu ,ni ukweli wanaongeza fedha katika mzunguko lengo likiwa ni kupunga gap lililopo mana bila hivyo nchi inakwenda kubaya sana.
   
 7. Lokissa

  Lokissa JF-Expert Member

  #7
  Jan 1, 2011
  Joined: Nov 20, 2010
  Messages: 7,079
  Likes Received: 154
  Trophy Points: 160
  kama Rais wetu ni mchumi lakini hajui kwanini tanzania ni maskini hivi mwategemea atakuwa na mawazo ya kiuchumi? na mashaka na GPA yake hata kama alifaulu vzr atakuwa alidesa kwenye UE. Tujiulize ni kiasi ghani kimetumika ktk kubadilisha hizi noti mpya.thamani ya sh bado iko chini tutabaki kuwa maskini labda hiki kizazi kinachotuongoza chenye miaka 50 na kuendelea kitakapotokomea chote ndo uchumi wa Tanzania utabadilika.
   
 8. C

  Caroline Danzi JF-Expert Member

  #8
  Jan 1, 2011
  Joined: Dec 19, 2008
  Messages: 3,629
  Likes Received: 56
  Trophy Points: 145
  Kaka zangu tangu ufisadi umeingia hakuna taaluma popote pale, wana interest zao za ufiisadi wachumi wanapelekwa kama maboya. Unafikiri hata wakishauri chochote kitakubalika kama mtu ameshaona kuna ulaji hapo? Tutaendelea kuburuzika mpaka siku tunaingia kaburini. Wengi wamekuwa wakiachia nafasi zao pale wanapoingiliwa kwenye taaluma zao, anaona bora kukaa nyumbani acheze na watoto wake kuliko kukubaliana na ushauri nje ya taaluma zao. Je ni wangapi wako tayari kufanya hivyo na njaa iliyowajaa? Lets pray for our Nation kweli tunakoelekea Mungu atutie nguvu
   
 9. Mdau

  Mdau JF-Expert Member

  #9
  Jan 1, 2011
  Joined: Mar 29, 2008
  Messages: 1,771
  Likes Received: 251
  Trophy Points: 180
  Kwenye bolded phrases........

  1. Kama proposals hazifanyiwi kazi, kwa hiyo inahalalisha wao kukaa kama sanamu tu?? Si watoke kisha waseme??

  2. Basi hakuna wanacho-regulate kama utashi wa kisiasa ndio jibu la mwisho, BoT IFUTWE!!
   
 10. K

  KunjyGroup JF-Expert Member

  #10
  Jan 1, 2011
  Joined: Dec 7, 2009
  Messages: 352
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 33
  Uchumi wa Tz unaendeshwa wit de wind. There's no BoT nor Ministry of Finance. Mumewahi sikia lini wakitoa mikakati ya kukuza uchumi (yenye mashiko) au kupandisha thamini ya Tsh. na wakafanikiwa? Wapo wapo tu. Eti uchumi unakuwa kwa 6%, upuuzi mtu!
   
 11. N

  Nonda JF-Expert Member

  #11
  Jan 1, 2011
  Joined: Nov 30, 2010
  Messages: 13,222
  Likes Received: 1,957
  Trophy Points: 280
  Kwenye nchi ambayo kuanzia mfagiaji wa ofisi hadi mkuu wa nchi anafikiria tumbo,mfuko wake tu.unategemea ana muda wa ubunifu wa mkakati wa kukuza uchumi na kuu-diversify ?
  Kwenye nchi ambayo siasa ndio njia pekee ya kupata utajiri wa haraka unategemea maendeleo ya nchi?
  Kwenye nchi ambayo rushwa ni jambo la kawaida na linakubalika kwa kila mtu unategemea nini,mkuu ?

  Nchi ambayo inaongozwa kisiasa siasa tu. Tena siasa za kipuuzi na ufisadi, unafikiri watu wana muda na nafasi ya kufikiria mustakabali wa Taifa ?

  Tatizo ni uongozi, hatuna viongozi wenye uchungu na nchi yao. Wanatembea katika nchi za watu wanaona lakini hawajiulizi kwa nini nchi hizo zinapiga hatua mbele na wala hawana hamu ya kujifunza hayo.

  Sisi kama wenye nchi, siku tukiamua kuwa yametutosha basi tutaacha ukondoo na heshima ya woga na kulazimisha uwajibikaji kwa viongozi wetu.
   
 12. Husninyo

  Husninyo JF-Expert Member

  #12
  Jan 2, 2011
  Joined: Oct 24, 2010
  Messages: 23,814
  Likes Received: 583
  Trophy Points: 280
  umeongea kweli mkuu. Hivi isingewezekana kuongeza hiyo mijihela kwa noti zile zile za zamani?
  Naona wakati wa kubeba hela kwenye gunia nikapate lunch unakaribia.
   
 13. Mzuvendi

  Mzuvendi JF-Expert Member

  #13
  Jan 2, 2011
  Joined: Apr 28, 2009
  Messages: 431
  Likes Received: 12
  Trophy Points: 35
  Sometimes new bank notes are released in order to increase security features. There are people out there who produce fake notes that have adverse impact to our economy. Therefore, it's imparative for the bank to ensure that illegal notes are removed from circulation, and the effective way to do that is to issue new bank notes. By doing so every old note that goes to the bank doesn't allowed to come back.

  This procedure is not new. Even the US Federal reserve bank does that, and I don't see the reason why The BOT shouldn't use the same approach.
   
 14. Mzito Kabwela

  Mzito Kabwela JF-Expert Member

  #14
  Jan 2, 2011
  Joined: Nov 28, 2009
  Messages: 17,515
  Likes Received: 1,685
  Trophy Points: 280
  kwa wote wanaoipinga BOT kwa kubadilidha noti mkitoa vigezo vya uchumi nawashauri mkasome maana ya fisical policy na monetary policy. Kisha msome roles za central bank (kwa tanzania ni roles za benki kuu) kwenye kuregulate economy ndipo mtaelewa mnachopinga ni hoja mwafaka au la. Mnaweza mkawa sahihi lakini vigezo mnavyovitoa havina maana kitaalam
   
 15. Mzito Kabwela

  Mzito Kabwela JF-Expert Member

  #15
  Jan 2, 2011
  Joined: Nov 28, 2009
  Messages: 17,515
  Likes Received: 1,685
  Trophy Points: 280
  inawezekana ukawa sahihi lakini kwa angle nyingine sio hii ya kuchapisha note. Kusema ukweli noti hizi zinazobadilishwa zimekaa muda mrefu kwenye mzunguko na kwa ukuaji wa teknolojia hivi sasa upo uwezekano wa note fake kuwa kwenye cirulation na kusababisha inflation na velocity of money kuwa juu ndo mana utakuta mtu analalamika akichange elfu kumi tu basi haikai lisaa, ishaisha. Lakini kwa hili la kubadili note ni sawa kabisa halina tatizo, kama limefanyika kwa dhamira njema.
   
 16. Mzito Kabwela

  Mzito Kabwela JF-Expert Member

  #16
  Jan 2, 2011
  Joined: Nov 28, 2009
  Messages: 17,515
  Likes Received: 1,685
  Trophy Points: 280
  wakati mwingine indicators za kukua kwa uchumi sio lazima uzi feel waziwazi, kuna factors nyingi za kudetermine economic growth. Lakini pia political willingness ina mchango mkubwa kwenye kukua kwa uchumi. Kwa hili la note tutakachopaswa kuhoji ni jinsi tender ya kuchapa hizo note ilivyofanyika,kiasi alicholipwa mzabuni, mchakato wa ulupaji, value for money etc...lakini ukuaji wa uchumi wakati mwingine ni calculations zisizoreflect hali halisi mija kwa moja
   
Loading...