Bosi Simba: Manzoki sawa, Bobosi hapana

BANDOKITITA

JF-Expert Member
Oct 4, 2022
1,177
2,281
MENEJA wa Habari na Mawasiliano wa Simba, Ahmed Ally amefichua ni kweli kuna mipango inafanyika kumhusu Cesar Lobi Manzoki raia wa DR Congo, lakini akaweka wazi kuwa mpaka sasa hakuna lolote kati yao na Bobosi Byaluhanga raia wa Uganda.

Manzoki na Bobosi wamekuwa kwenye rada za Simba tangu kipindi cha usajili wa dirisha kubwa ambapo kwa Manzoki, tayari walifikia makubaliano naye binafsi na kusaini mkataba wa awali wa miaka miwili kabla ya Vipers kuweka ngumu kwenye dau la usajili na straika huyo kutimkia China.

Ally alisema: “Kumekuwa na taarifa nyingi kuhusu mipango yetu ya usajili na tayari baadhi ya wachezaji wamekuwa wakihusishwa moja kwa moja na Simba, wakiwemo Manzoki na Bobosi.

“Kuhusiana na Manzoki ni kweli nafahamu uongozi umekuwa kwenye mipango ya kuhakikisha anakuwa mchezaji wa Simba, licha ya kuwa ni mapema kuzungumzia hili.

“Lakini Bobosi mpaka sasa nachojua hakuna mpango wowote wa kumsajili, labda kama kutakuwa na taarifa mpya kuhusu mahitaji ya kocha lakini kwa sasa niwaombe Wanasimba kuwa watulivu na kusubiri taarifa rasmi ya klabu.”
 
Back
Top Bottom