Bosi NHC, EWURA, wakana kulipwa milioni 36

Salary Slip

JF-Expert Member
Apr 3, 2012
48,704
149,938
Wakurugenzi wa Taasisi hizi wamekana kulipwa kiwango hicho cha mishahara walipokutana na Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Uwekezaji wa Mitaji(PIC) huku kila mmoja wao akishangazwa na taarifa hizi.

Mkurugenzi wa NHC,Nehemia Mchechu amesema mshahara wake haufiki hiyo milioni 36 kwa mwezi.

Kwa upande wake, Mkurugenzi Mkuu wa Ewura, Felix Ngamlagosi amesema yeye mshahara wake haufiki hata nusu ya hiyo milioni 36 kwa mwezi.

Chanzo:HabariLeo online

Kwa taarifa hizi,ina maana Raisi alidanganywa?Je, hapa tumwamini nani?Au kuna maboss tofauti na hawa wanaolipwa hiyo milioni 36?

Na sasa sisi huku mitandaoni tunajadili nini?

Mbona haya ni mambo ya ajabu sana?!

============================

MABOSI wa mashirika mawili ya Serikali nchini, wanaodaiwa kulipwa mshahara wa Sh milioni 36, wamekanusha madai hayo, huku wakielezea kushangazwa na taarifa hizo wakati hata nusu ya fedha hizo, hawapati.

Akizungumza mbele ya Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Uwekezaji wa Mitaji ya Umma (PIC), mwishoni mwa wiki jijini Dar es Salaam na Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Nyumba la Taifa (NHC), Nehemia Mchechu, halipwi mshahara huo.

Akijibu hoja za wajumbe wa kamati hiyo kuhusu taarifa ya utekelezaji na utendaji wa shirika hilo kwa mwaka 2014/15, Mchechu alisema shirika hilo pamoja na kutekeleza majukumu yake, bado lina changamoto za uhaba wa fedha.

“Katika ujenzi wa nyumba zetu, Serikali haigharamii masuala ya miundombinu kama vile maji, umeme, barabara hilo ni jukumu letu na linatugharimu fedha nyingi. “Sasa nashangaa wako watu wanasema mimi nalipwa mshahara mkubwa, sielewi wametoa wapi huo mshahara kwa sababu silipwi mshahara huo, mimi nalipwa chini ya huo walioutaja,” alisema Mchechu.

Kwa upande wake, Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Udhibiti wa Huduma za Nishati na Maji (Ewura),Felix Ngamlagosi aliiambia kamati hiyo kwamba mamlaka hiyo ina changamoto nyingi ikiwemo uhaba wa watumishi na maslahi duni. Alisema wakati maslahi ya wafanyakazi ni duni, ameshangaa kusikia vyombo vya habari vikisema yeye ni miongoni mwa wakurugenzi wanaolipwa Sh milioni 36 kwa mwezi.

“Jamani hapa tunazungumzia maslahi duni ya watumishi wetu, nashangaa kusikia naambiwa nalipwa milioni 36, mshahara wangu haufiki hata nusu ya hizo fedha,” alisema Ngamlagosi. Nyumba nafuu Awali wajumbe wa kamati hiyo baada ya kupitia taarifa hiyo ya NHC, waliiomba Serikali kuharakisha kuwepo kwa sera ya nyumba ili kurahisishia mashirika yanayohusika na masuala ya ujenzi wa nyumba kujenga nyumba za bei nafuu kwa wananchi.

“Yapo malalamiko kutoka kwa wananchi kwamba NHC mnauza nyumba kwa bei kubwa, huku mkitoa matangazo kuwa nyumba hizo ni bei nafuu,” alihoji mjumbe wa Kamati hiyo, Mbunge wa Ushetu, Elias Kwandikwa. Akijibu hoja hiyo, Mchechu alisema nyumba zinazojengwa na NHC zinauzwa kuanzia Sh milioni 30 hadi 250 kwa fedha taslimu na kwamba mnunuzi atatakiwa kulipa kodi.

Aliongeza kuwa kama mnunuzi hatakuwa na fedha taslimu, benki washirika wanatoa mikopo kwa ajili ya ununuzi wa nyumba hizo, ila wanunuzi watatakiwa kulipa riba za benki husika. Baada ya majibu hayo, wajumbe hao walitaka Serikali iangalie jinsi ya kupunguza mzigo kwa shirika hili na ikiwezekana waondolewe kodi ya uingizaji vifaa vya ujenzi ili kusaidia nyumba hizo kuuzwa kwa bei nafuu, kwa lengo la kuwanufaisha wananchi hasa wale wa kima cha chini.

Akizungumzia hoja hizo, Naibu Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Angelina Mabula alisema shirika hilo, linapaswa kuwasiliana na watendaji katika maeneo husika ya ujenzi wa nyumba hizo, ili wawasaidie kubeba gharama ndogondogo.

“Serikali na wizara zinafanya kazi kwa ushirikiano na NHC, na hili la gharama za miundombinu, kila halmashauri nchini ambayo ujenzi wa nyumba hizo unafanywa, inaweza kuangalia jinsi ya kusaidia gharama za miundombinu, ili nyumba hizo ziuzwe kwa bei nafuu zaidi kwa wananchi,” alisema Mabula.
 
Hawa jamaa hivi hawajui kwamba Rais ana data za TISS.Kukataa ni kuzidi kumuudhi.Ingekuwa busara kwao kama wangenyamaza kimya.
Wakurugenzi wa Taasisi hizi wamekana kulipwa kiwango hicho cha mishahara walipokutana na Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Uwekezaji wa Mitaji(PIC) huku kila mmoja wao akishangazwa na taarifa hizi.

Mkurugenzi wa NHC,Nehemia Mchechu amesema mshahara wake haufiki hiyo milioni 36 kwa mwezi.

Kwa upande wake, Mkurugenzi Mkuu wa Ewura, Felix Ngamlagosi amesema yeye mshahara wake haufiki hata nusu ya hiyo milioni 36 kwa mwezi.

Chanzo:HabariLeo online

Kwa taarifa hizi,ina maana Raisi alidanganywa?Je, hapa tumwamini nani?

Na sasa sisi huku mitandaoni tunajadili nini?

Mbona haya ni mambo ya ajabu sana?!
 
Raisi wetu ni mwongo
Eti mtu anapokea mishahara 17 khaaaaaaa
 
Wakurugenzi wa Taasisi hizi wamekana kulipwa kiwango hicho cha mishahara walipokutana na Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Uwekezaji wa Mitaji(PIC) huku kila mmoja wao akishangazwa na taarifa hizi.

Mkurugenzi wa NHC,Nehemia Mchechu amesema mshahara wake haufiki hiyo milioni 36 kwa mwezi.

Kwa upande wake, Mkurugenzi Mkuu wa Ewura, Felix Ngamlagosi amesema yeye mshahara wake haufiki hata nusu ya hiyo milioni 36 kwa mwezi.

Chanzo:HabariLeo online

Kwa taarifa hizi,ina maana Raisi alidanganywa?Je, hapa tumwamini nani?

Na sasa sisi huku mitandaoni tunajadili nini?

Mbona haya ni mambo ya ajabu sana?!
Alidanganywa vipi hao mabosi wanatakiwa wasema wanalipwa kiasi gani, Magufuli yeye kasema mshahara wa juu utakuwa milioni 15 hakutaja jina la mtu.
 
Wataalam wa mambo ya utumishi tusaidieni hapa:Je,allowances anazozipata mtu nazo zinahesabika ktk mshahara au ni ile basic pay ndiyo inayotambulika?Hao wanaokataa usikute ukijumlisha na allowances ndio vinafika viwango hivyo kwa mwezi.
 
Kwani Magufuli alisema ni boss wa NHC ama EWURA ndio wanaolipwa hiyo 40m ????
 
Tanzania my country tatizo speculations zinakuwa nyingi kupita maelezo. Haya wacha movie iendeleee......
 
Wataalam wa mambo ya utumishi tusaidieni hapa:Je,allowances anazozipata mtu nazo zinahesabika ktk mshahara au ni ile basic pay ndiyo inayotambulika?Hao wanaokataa usikute ukijumlisha na allowances ndio vinafika viwango hivyo kwa mwezi.
Ina maana Raisi hajui tofauti ya mshahara na malipo mengine?

Binafsi hata mimi nawaza huenda hili ndio tatizo lakini unaposema mtu analipwa mshahara kiasi fulani inaeleweka huo ni mshahara pasipo marupuru.
 
Magazeti ndiyo yalileta habari za wakurugenzi NHC,EWURA nk.kulipwa pesa ndefu. Mshahara wa mtu ni siri hatahivyo, tumwache Rais atajua nani wa kukatwa ama la kuanza kutajana tajana bila uhakika ni kiherehere na kurukia mambo
 
Back
Top Bottom