Joel Johansen
JF-Expert Member
- May 12, 2016
- 242
- 319
Wana JamiiForums, nawasalimu,
Note: Nadhani maelezo yangu yatakuwa marefu, lakini kama huwa husomi habari ndefu, hebu leo jisomee, nahisi unaweza kujifunza jambo au ukaona tu jinsi maisha yalivyo kwa baadhi ya watu duniani.
Naamini maneno yangu hayatasikiwa na Bots but Humans ambao ni watanzania wenzangu. Siandiki ili kukutisha au uhuzunike kutokana na hali yangu, kwasababu mimi sio mtu wa kwanza kupitia mazingira niliyonayo sasa.
Juzi nilipokea ujumbe kutoka Benki ya Exim. Ujumbe unaonyesha kuwa salio langu la mshahara kwa mwezi huu ulioisha juzi (Juni 2016) ni Tshs elfu 20 na senti kadhaa. Hii ni kinyume na makubaliano na Bosi wangu kwasababu take-home yangu inapaswa kuwa Tshs laki 9 (baada ya makato yote). Nilipomuuliza akadai kuwa ameamua kukata mkopo wote kwa pamoja (alinikopesha Tshs laki 7 kwa matumizi ya kodi ya nyumba, nauli na uhamiaji maana alinihamisha kutoka mkoani).
Anadai sababu iliyopelekea yeye kukata mkopo huo kwa pamoja kutoka kwenye mshahara wangu ni biashara yake kutoenda vizuri. Nilipomuuliza jambo hilo linahusiana vipi na utendaji kazi wangu, akadai kuwa kwenye utendaji niko vizuri, ila yeye ni msimamizi tu, kwahiyo asilaumiwe kwa maamuzi anayoyachukua.
Ndugu zangu, sikupanic kwenye kikao…lakini baada ya kuondoka (leo ni Jumamosi, tumetoka saa 7 mchana), nilihisi kuchanganyikiwa. Kwasababu ndio mshahara wangu wa kwanza na akiba yangu iliishia kwenye maandalizi ya makazi mapya maana nilijua I will settle here in this town.
Kwenye kikao chetu, nilijenga hoja nyingi kumwonyesha kuwa uamuzi wake sio sahihi maana I just got in the City (mwanza to arusha)…jibu lake ni moja tu, “He’s just doing his job, he can’t be responsible”!
Wana JF, nilipokuwa njiani kurudi kutoka kazini kuelekea nyumbani, nilihisi ni kama ninatembea kwa mguu kutoka Arusha kurudi Mwanza. Muda huu ninavyoandika, nimesimama mbele ya mashamba ya mahindi, nikiyaangalia yalivyostawi, na kulia sana, nikisema ni kheri ningekuwa mmoja wa mahindi yale. Maana tangu niokotwe kwenye mlima wa Kitangiri jijini Mwanza (nikiwa na umri wa miezi miwili tangu mama mzazi anitelekeze pale), na kulelewa kwenye Orphanages kibao ambazo kupitia wafadhili wake, niliweza kufika chuo na kujipatia taaluma, sijawahi kukumbana na mtihani mzito kama huu; nimelala nje, nimekula dampo, nimeomba omba barabarani…lakini sijawahi fikia level hii ya kuwa ugenini, as a father, as a husband, bila kuwa na cha kuwalisha wanangu (mwanangu na mke wangu wote huwa nawaita wanangu).
because, ndani hamna kitu, and there’s no way I will survive by Tshs 20 thousands. Maana kiasi hicho cha fedha huisha dakika moja tu mwanetu akipata homa usiku. Hii baridi ya Arusha ni janga kwa kichanga wetu.
Ikumbukwe kwamba wiki kadhaa zilizopita, nilileta uzi hapa jukwaani kuhusu nia ya kuitelekeza familia yangu ili nianze maisha upya, maana nilidhani pengine wao ndio chanzo cha mimi kukosa maendeleo licha ya kujituma kwa kadri ya uwezo wangu. Mlicomment sana, na wengi mlisema kwamba kuna uwezekano mkubwa kuwa mimi sijalelewa na wazazi ndio maana sina utu, hivyo sioni shida kumwacha mke na mtoto. Ni kweli mimi sikuwa na malezi ya familia, lakini maoni yenu yaliuvunja vunja moyo wangu na kufanya nimpigie magoti Abigael na kumuomba msamaha kuhusu tabia nilizokuwa nimeshaanza kuzionyesha za kutaka kuwatoroka yeye na mwanae.
Nyie niliwapa mrejeshi kwamba ninaprocess taraka, No, kwakweli nilishindwa kuimagine misha bila ya hawa wanangu…nilihisi kupotea kabisa, so nikaghaili mchakato wa taraka). Haikupita muda ndio tukawa tumehamia Arusha kwa h-ii ofa ya kazi.
Ndugu zangu, nina majuto makali, kwamba iweje nipoteze maisha ya utoto wangu kwenye uyatima, nipambane hadi niwe na familia, angalau na mimi niwe na watu wa kuita ndugu zangu…ili tu mwisho wa siku nije nidharirike ugenini, mbele ya macho ya mwanangu, kwamba nimeshindwa kumpa chakula? Mbele ya Abigael wangu, kwamba nimeshindwa kumhudumia kama jinsi nilivyomzoesha? Nina majuto makuu ambayo maneno yamdomo na kalamu hayatoshi kuyaelezea. Kama gharama ya kutua msalaba Calvary ni mauti, mimi nipo tayari kufa. I can’t hold any longer.
Update:
Watu wananidhihaki, wananiita muongo, wanasema nataka kutapeli. Kosa langu ni nini I ndugu zangu, kuandika yanayonisibu? Kuandika moto ninaopitia? Niliandika nikiwa kwenye msongo wa mawazo mkuu na hali ya kukata tamaa....ila kwa ufupi ni kwamba nimekatwa mshahara wote na sina cha kufanya...mwanetu ana homa kali tangu usiku wa jana...Abigael hanielewi, ananilaumu kwanini nimewaleta waje wafie Arusha. Ndugu zangu, moyo wangu unavuja damu