Salahan
JF-Expert Member
- Sep 10, 2014
- 2,963
- 3,675
Pamoja ya kwamba kunabaadhi ya mambo unamfanyia mume wako kwa nafasi yako kama mke, pamoja na kwamba unampa unyumba japo kwa manati lakini kunavijitabia vidogovidogo unaweza usivione ni shida lakini vinaonyesha jinsi ambavyo haujafunzwa kwenu na kwenye kitchen party yako uliambulia rice cooker tu na sio mafundisho. Mke uko nyumbani au umewahi kurudi kabla ya mumeo, mumeo anafika home uko bize na simu, labda anakukuta chumbani umeng'ang'ana na simu wala jicho humwangalii zaidi ya kutoa sauti yaubize "pole" huku macho yako kwenye simu, utadhani unaongea na fundi wako wa nguo kumbe mumeo. Halafu jamaa akipoteza ladha ya kuwahi kurudi nyumbani unaanza kupiga tarumbeta kumbe wewe ndio kimeo. Ndoa sio kujua kupika na kukatika pekeyake. Hata jongoo anajua huomchezo. Show some repect. Shauri yako.Ni mtazamo wa fikra pevu tupo kujenga sio kubomoa