Bora serikali ya kikoloni kuliko serikali ya awamu hii

Bora serikali ya kikoloni kuliko serikali ya awamu hii

hakuna tofauti na ukoloni kama serikali inataka watu wake waishi kama mashetani kila kitu cha kawaida tuu kinaonekana anasa kwa raia wake...
 
hakuna tofauti na ukoloni kama serikali inataka watu wake waishi kama mashetani kila kitu cha kawaida tuu kinaonekana anasa kwa raia wake...
nenda Nigeria ukapambane na Boko Haram. Hapa si unasema kuna ukoloni? Acha ulofa wewe!
 
Haya unayoyasema leo hayawezi kueleweka kwa wote maana siyo wote wenye Vichwa wana akili, haya maneno yako yatakua ya kishujaa baada ya karne moja.
Lol kubadili watu ni kazi ngumu ukilinganisha na kuitafuta dollar million moja kwa njia sahihi....

Binadamu tujitambue...

Word mkuu
 
nenda Nigeria ukapambane na Boko Haram. Hapa si unasema kuna ukoloni? Acha ulofa wewe!
Matusi ya nini mkuu mimi situkani hata ufanyeje umri huo nishapita kitaambo huko kote nishaenda taja Nchi nyingine labda...
 
Mtoa mada ndio kwanza ana miaka 27,halafu anatuambia bora mkoloni,unamjua mkoloni wewe?
Labda amesoma vitabu....

Na imani kwamba books shapes us because we need knowledge to live...

the vice versa is also true; determinant factor is who you wanna be!
 
NIMEWAHI kujadili umuhimu wa kuwa na mtazamo wa mbali, na kufanya mipango yetu kwa kuamini kwamba taifa letu litakuwapo baada ya sisi tuliopo kutoweka.

Hii ina maana ya kuachana na mtindo wa kulipua na kufanya kazi kwa njia za zimamoto. Ina maana ya kupanga miradi mikubwa ndani ya programu pana zinazoangalia upeo wa karne kadhaa zijazo.

Kila nikitathmini utendaji wetu, na hasa utendaji wa wakuu wa serikali, sioni mtazamo wa aina hiyo. Ninachoona ni kufanya mambo ‘ad hoc,’ haraka haraka, kwa ajili ya leo au kesho tu, halafu tutaangalia. Tunalipua, hatuna mtazamo wa kimkakati, kana kwamba muda si mrefu ujao tutakuwa hatupo tena.

Kutokana na hali hii, tumezalisha ‘viongozi’ wengi wanaodhani kwamba kuchapa kazi maana yake ni kupiga kelele majukwaani, kutoa amri kwa watendaji kupitia kauli za majukwaani na kupitia televisheni.

Leo hii, kila ‘kiongozi’ anashindana na mwingine kwa kujaribu kutoa amri nyingi kuliko mwingine. Matokeo yake ni kwamba hatuna mipango ya muda mrefu wala mipango iliyoratibiwa kuhusisha nchi nzima na sekta zote. Kila amri inajitegemea na kila ‘kiongozi’ ana mipango yake.

Hii ndiyo staili ninayoiita u-Mrema kutokana na staili aliyoianzisha Augustine Mrema alipokuwa waziri aliyehusika na mambo ya usalama wa raia.

Naamini kwamba Mrema alichukua staili ya kutoa matamko mengi hadharani ambayo mengi yalikuwa ni amri kwa watu aliowataka wafanye hili au lile, kwa sababu hakuwa na uwezo wa kutambua ni vipi Serikali inatakiwa kufanya kazi, akidhani kwamba waziri mchapa kazi ni yule anayekwenda mwenyewe kukamata walanguzi wa pombe na wafanya magendo ya kahawa.

Kinachotusumbua leo, ni kwamba Mrema alifanikiwa mno katika juhudi zake za kupata umaarufu, kwani wananchi wa kawaida ambao nao hawajui ni jinsi gani serikali inatakiwa ifanye kazi yake, walimuona kama shujaa.

Wananchi wa kawaida waliziona zile amri za ‘siku saba’ kama ushahidi wa waziri anayefanya kazi yake bara bara. Wala hawakuhoji ni kwanini mara kadhaa aliwataka wafanyabiashara walioonekana kama wasio waaminifu wamfuate kijijini kwake Moshi.

Wananchi pia hawakuhoji ni kwa nini Mrema alikuwa na ujasiri wa kuwalaumu mawaziri wenzake hadharani kwa kusema kwamba walikuwa wanamzuia kufanya kazi yake kikamilifu kwa kuwa walikuwa si waaminifu kwa wananchi.

Bila shaka walikuwapo mawaziri walioona kwamba utendaji kazi serikalini haukupaswa kuwa jinsi Mrema alivyokuwa akifanya, na bila shaka walisema hivyo katika vikao vya Baraza la Mawaziri, lakini wakaonekana kama wasio na maana.

Katika utaratibu wa serikali inayoendeshwa kama Serikali, ilitakiwa Rais Ali Hassan Mwinyi (wakati huo wa Mrema) amuondoe serikalini mapema asubuhi kwa kukiuka utaratibu wa Serikali.

Badala yake akampandisha cheo na kumfanya Naibu Waziri Mkuu, huku akiendelea kuwa Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, mamlaka makubwa mno mikononi mwa mtu aliyekuwa ametia fora katika kuvuruga utaratibu wa utendaji serikalini. Sababu zake ni nini? Nitajaribu kueleza.

Utawala unaokabiliwa na malalamiko mengi ya wananchi bila kuwa na maelezo ya kuridhisha, utakumbatia kila aina ya ubabaishaji alimradi unashabikiwa na wananchi, kimsingi kwa sababu ushabiki wa wananchi unaonekana kuujengea uhalali na Mrema alionekana hivyo.

Wala hakuwa wa kwanza, kwani hata Edward Sokoine alikuwa na muonekano huo wakati wa kile kilichojulikana kama ‘Uhujumu Uchumi.’ Maana yake ni nini? Mfumo uliochoka na ulioshindwa kutafuta majibu sahihi kwa maswali ya wananchi, utaegemea juhudi za kiimla za mtendaji mmoja mmoja, kama Sokoine chini ya Mwalimu Nyerere na Mrema chini ya Ali Hassan Mwinyi, na hawa tunaowashuhudia chini ya Rais Jakaya Kikwete.

Maana yake ni kwamba ni rahisi zaidi kuachia watu wawili au watatu wakapita wakifoka na kutoa amri, badala ya kujenga mifumo ya utekelezaji iliyosimama juu ya misingi ya kisera na kisheria, ambayo inasumbua akili, inahitaji usimamizi makini na inahitaji uratibu ulio makini wa sekta zote zinazohusika na zinazoingiliana. Hiyo ni kazi ngumu zaidi kuliko kutoa amri za kiimla.

Lakini ni staili dhaifu na isiyo endelevu, haina mashiko ya kiutekelezaji, haina uwezo wa kuenea kote nchini na inatoweka mara tu anapoondoka madarakani waziri au mkuu yeyote aliyeianzisha. Ni moto wa kifuu unaowaka sehemu ulipowashiwa, lakini usiosambaa sehemu nyingine yo yote, na baada ya muda mfupi tu kitakachosalia ni majivu baridi.

Wale wanaopendelea staili hii wanapaswa wajiulize, iwapo waziri ametembelea wilaya moja ambako amekuta matatizo ya utendaji mbovu na akaona jawabu ni kutoa amri ya kumsimamisha mtendaji au kusitisha zoezi fulani, je; ni wilaya ngapi anaweza kujua zinaendeshawa vipi, zina matatizo yapi, na ni ngapi anaweza kuzitembelea katika kipindi cha miaka mitano, na ni amri ngapi anaweza kutoa na kufuatilia utekelezaji wake?

Tatizo linalojitokeza katika wilaya moja linaweza kuwa ni ishara kwamba kuna matataizo ya aina hiyo hiyo katika wilaya zote nchini. Watu wetu wanazo tabia zinazofanana, mazoea ya utendaji yametufanya tujenge utamaduni unaoshabahiana, na mara nyingi tunaambukizana udhaifu kama vile wizi, ubadhirifu, uzembe na kutokujali.

Hivyo, matatizo yetu yanaweza kupatiwa majawabu ya jumla iwapo tutaketi na kuyajadili kama nchi na kuyatafutia dawa badala ya kutegemea amri za kiimla.

Ukoloni ulikuwa ni mfumo wa hovyo, wa nchi moja kuitawala nyingine, lakini pamoja na maovu yao yote, wakoloni walituachia utaratibu wa utendaji serikalini ambao uliwafaa wao wakati wakitutawala na ungeweza kutufaa sisi pia, tukifanya marekebisho kidogo. Cha kustaajabisha, ni kwamba yale maovu ya wakoloni tumeyakumbatia, wakati yale machache mazuri tumeyatupilia mbali.

Hebu tuirejee, tuiangalie mifumo yetu ya utawala, tuirekebishe. Tusifanye ‘fasta fasta’ kwani bado tupo hapa kwa karne kadhaa zijazo, miaka milioni kadhaa. Tunakimbilia wapi; tunakimbilia nini
Inaonekana ww ulizoea shotikati sasa umebanwa zaizi na kuanza kulilia
 
Yaani sijakuelewa unamaanisha, wakati mtumishi amekutwa anafanya madudu kama ilivyo desturi yake, na wanachi wakisaga meno, aachwe kupewa tamko ikiwa ni ujumbe pia na kwa wengine wenye kufanya kama yeye,halafu serikali iangalie tatizo hilo kwa ujumla wake!!!!!!!!!!!!

Nichelee kusema,wewe hukuwahi kuwa mtanzania wa kawaida kabisa anayezijua kero za uongozi mbovu.

Mtanzania masikini aliyechoshwa na matakataka ya watendaji mbali mbali,umwambie hizi habari zako mtaelewana wapi kwa mfano?????

Mimi binafsi nilimhitaji mtu kama jpm, ili angarau niwe najulikana kama nastahili kutendewa vyema.
Ha ha ha kuna ukweli lakini katika maneno yako....

Naye ana angle yake ya kuongea hayo labda afafanue amekerwa wapi hasaa...

Maisha ngumu muda wote
 
@assadsyria Ahsante kwa hoja madhubuti sana yenye kuonesha njia na namna bora ya kuendesha serikali.
Usijali comment za baadhi yetu humu wengi tumebaki kuponda na kutukana wanapo ona hoja haiendani na mahaba yao. Mara nyingi wanashindwa kujenga hoja kujibu au kusahihisha. Lakini hio ndio mfumo wetu ulivo jengwa... kila awamu inakua na wapiga debe ambao ni wana macho lakini hawaoni na wana masikio lakini hawasikii.
Ukitoa hoja nzito yenye faida kwa taifa utaambiwa fisadi ooh tuna soma bure. Tatizo la bure ndio hili la kuzalisha viongozi wasio.
Ni kweli kabisa tuna matatizo kabisa kabisa katika kuendesha mambo yetu..kama taifa tuji tathmini upya...na hili halipo ssrikalini tu hata huku nje tunako endesha taasisi zetu za kiraia na hata vyama vya siasa.
Mfano kama taifa tunatakiwa tujiulize kwa nini waajiri na seriious companies nyingi zinapendelea kuajiri watu kutoka nje ? Kwa nini waingie gharama kubwa sana wakati vijana wetu graduates wapo nje wengi tu na hawana kazi? Tatizo ni nini ? Tumekaa tukatafakari na kufanya utafiti ? Zamani tuliona kuwa labda ni wahindi au wazungu ndio wana penda kuajiri MaTx lakini sasa mpaka makampuni ya Watanzania Wafrika wenzetu nao wanapenda kuajiri Tx.kwa nini ?
Uamunifu ?
Kiwango cha elimu yetu
Uwajubikaji
Hatupo creative?
Nini hasa sababu? Laiti kama sio kwa serimali kuweka vikwazo na tungekua free labour country basi kila secta wangeleta mhindi na mkenya.
Huu ni ukweli japo mchungu...sasa mambo kama haya ndio ya kuyafanyia uchunguzi ..na kuja na silution...kama ni mfumo wetu wa elimu au mentality ya vijana wetu . Cha kushangaza zaidi wale wachache ambao ni wachapa kazi hasa huwa wanahama wapo wengi njee ya nchi.
Mimi nadhani mind set yetu ina hitaji kywa reset..kampeni na siasa za umarx zimetu athir sana.
China walilifahamu hili na walubadilisha mfumo mawazo ya wachina . Kuna Deng xiaping na green revolution ilisaidia kuwajenga wa china kutoka katika mfumo ule wa kuabudu mtu mmoja na kuwapa matumaini kuwa wanaweza kufika mwezini pia.
Mfumo wa kimarx unatia woga na uvivu..unakufanya ufante kazi kwa kengele.
Korea ya kaskazini nao wameathirika sana na mfumo huu... na bahati mbaya bado wanao na hawa jamaa watakua na kazi kweli kuja kuwa taifa huru na lenye fukra huru. Wamezoea kufanya kazi kwa kengele na kuimba sifa kwa mtu mmoja tu.
Tubadilike. Ujerumani baada ya ku fall ukuta wa Berlin waluweza nao kuirejesha Ujerumani Mashariki kwenye uhuru wa fikra na kutoa viongozi bora kutoka ujerumani na kuachana kabisa na kansa ya umarx leo Cansela wa Ujerumani Bibi Merkel ni mzaliwa wa Ujerumani mashariki na ameiingoza Ujerumani kuwa na uchumi imara ..ni mmoja kati ya viongozi makini ..Utandu ule wa kupandikizwa umemtoka..
 
Magufuli mpaka atamaliza miaka 5 yake hakuna hata moja atakuwa katimiza kwa 100% kwa sababu serikali hii haina mipango wala dira, wala hatujui tunataka kufanya nini kwa wakati gani,
 
[emoji19] kama kamba vile

Sent from my LG-D855 using JamiiForums mobile app
Mkuu nimefanya kazi ya utafiti wa aina za Samaki kwa miaka karibu minne baharini nilipokua nabeba box Cape town mother City,Oil Rig ndio kabisa nimeacha mwenyewe kazi huko na base yangu kibiashara ni Hong kong, Singapore na South Africa...
 
mimi hushangaa pale rais wa nchi mwenye PHD anapotoa matamko ya kimtaani...
"HUYO MNGEMTUMBUKIZA KISIMANI.."

na vipi yeye anaejitapa kwa kauli za kibaguzi eti "HAKUNA MPINZANI ATATIA MGUU KWENYE SERIKALI YANGU.."
mbona kodi za wapinzani anazitaka ?
kwani mpinzani hana haki ya kulitumikia taifa lake na kuonja matunda ya nchi ?

ni vibaya kubaguliwa na wakoloni..
ni aibu kubaguliwa na negro mwenzako !!
Mpaka akiondoka Taifa liko vipande vipande, sikiliza hotuba ya pemba na kwingine, utajua kama hatuna mtu mwenye nia ya kutuunganisha kama Taifa licha ya misimamo yetu ya vyama, Tuna mtu mwenye nia ya kutuchonganisha tu na kuleta ubaguzi Kati yetu
 
Kilichonishtua hapa sio habari bali mleta habari.Huyu si alikuwa mwenyekiti wa ccm JF,leo hii tena bora serikali ya kikoloni kuliko hii aliyoipigania kwa nguvu zake zote kuingia madarakani???Read the number brother
 
Kilichonishtua hapa sio habari bali mleta habari.Huyu si alikuwa mwenyekiti wa ccm JF,leo hii tena bora serikali ya kikoloni kuliko hii aliyoipigania kwa nguvu zake zote kuingia madarakani???Read the number brother
Ukiona manyoya.......................[emoji1] [emoji1]

Huyu ndio mkandarasi, anakandarasi inji.
 
Back
Top Bottom