Bora elimu na sio elimu bora | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Bora elimu na sio elimu bora

Discussion in 'Uchaguzi Tanzania' started by Jatropha, Sep 21, 2010.

 1. Jatropha

  Jatropha JF-Expert Member

  #1
  Sep 21, 2010
  Joined: Apr 9, 2009
  Messages: 1,152
  Likes Received: 144
  Trophy Points: 160
  Wakati Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe Mizengo Pinda, jana tarehe 19 Septemba 2010 alipokea Tuzo kutoka Umoja wa Mataifa kwa mafanikio Tanzania iliyopata katika uandikishaji wa watoto wengi zaidi kujiunga na Darasa la Kwanza hapa nchini. Inakadiriwa kuwa zaidi ya 95% ya watoto wote wanaotakiwa kwenda shuleni waliandikishwa kujiunga na Darsala Kwanza hapa nchini

  Tarehe 20 Septemba 2010, Taasisi inayohusika na masuala ya Kielimu hapa nchini iitwayo TENMET, katika mkutano wa ELIMU KWA WOTE imetangaza matokeo ya utafiti wa sekta ya Elimu ya Msingi. Utafiti huo unaonyesha kuwa ubora wa elimu inayotolewa hapa nchini ni ya kiwango cha chini sana, ambapo zaidi ya 50% ya watoto wanaomaliza Elimu ya Msingi (Darasa la Saba) hawawezi Kusoma na Kuandika Kiswahili, Kiingereza na Hisabati.

  Utafuiti huo umeendelea kubainisha kuwa idadi hiyo ya watoto hawawezi kushinda mitihani ya masomo hayo ya Darasa la Pili.

  Hali hii inaripotowa wakati ambapo Tanzania ipo katika kipindi cha Kampeni kuelekea Uchaguzi Mkuu wa mwaka 2010, na tayari vyama viwili vya CHADEMA na CUF vimeahidi kuboresha sekta ya Elimu kwa kutoa Elimu ya Bure kwa watoto wote kutokea Darasa la Kwanza hadi Kidato cha Sita; na Chuo Kikuu.

  Na wasemaji mbali mbali wa chama tawala CCM wameipinga ahadi hiyo, na kudai kuwa suala hilo haliwezekani kutokana na hali ya kiuchumi ya Tanzania.

  Vyama vinavyoahidi kutoa Elimu bure vinadai kuwa Serikali iliyoko madarakani inawekeza kidogo sana katika sekta ya Elimu hivyo kushindwa kuwapatia waalimu mazingira na mahitaji muhimu ya kufundishia kama vile nyumba za waalimu, vutabu vya kiada, vifaa vya kufundishia n.k; na kuwapatia wanafunzi mazingira huduma muhimu za kuwawezesha kusoma na kupata elimu inavyotakiwa kama vile vyumba bora vya madarasa, madawati, vitabu, waalimu wa kutosha n.k.

  Sababu mbali mbali zintajwa kuifanya Serikali iliyoko madarakani kushindwa kuwekeza ipasavyo katika sekta ya Elimu ikiwemo kuwa na matumizi makubwa sana yasiyokuwa na tija kwa wananchi walio wengi, kutoa misamaha mingi na mikubwa ya kodi kwa wawekezaji hususan kwa sekta ya madini. Inadaiwa kuwa mfano hai ni Ripoti ya Mkaguzi wa Hesabu za Serikali inazoonyesha kuwa Serikali iliyoko madarakani kila mwaka inatoa misamaha ya kodi inayofikia Shilingi Bilioni 700, hali ambayo huchangia kwa kiwango kikubwa kushusha mapato ya Serikali na hivyo kushindwa kuwapatia wananchi huduma za kijamii ikiwemo Elimu.

  Vile vile vyama vinavyoahidi kutoa Elimu bure vinadai kuwa Serikali iliyoko madarakani imeweka kiwango kidogo cha mrahaba kwa wawekezaji wa sekta ya madini cha 3% tu, wakati ambapo nchi ya Afrika ya Kusini inakusanya mrahaba wa 12% kutoka kwa wawekezaji hawa hawa na kwa madini ya aina hiyo hiyo. Na nchi ya Botswana badala ya kuchukua viwango vidogo vya mrahaba, inaingia ubia na wawekezaji wa sekta ya madini na hivyo kupata mapato makubwa sana.

  Ni nini maoni yako?

   
Loading...